CHADEMA yabwagwa Mwibara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yabwagwa Mwibara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAFILILI, Nov 23, 2011.

 1. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya pingamizi uchaguzi wa ubunge Jimbo la Mwibara mkoani Mara, iliyofunguliwa na mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

  Mahakama hiyo imemtangaza rasmi mgombea wa CCM, kwamba alishinda kihalali katika uchaguzi huo.

  Kesi hiyo Namba 7 ya mwaka 2010, ilisajiliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza na kupangiwa kusikilizwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Songea, Noel Chocha, ambapo ilipangwa kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa mjini Musoma.

  Mgombea wa Chadema, David Chiriko, alifungua kesi hiyo akimshitaki mgombea wa CCM, Kangi Lugola, maarufu kwa jina la Kangi Bomba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi Bunda.

  Katika madai yake mgombea wa Chadema, alidai kuwa taratibu za uchaguzi zilikiukwa, ikiwa ni pamoja na mgombea wa CCM, kuanza kampeni mapema, vitendo vya rushwa, kutumia gari la ubalozi, kutishia wananchi kwa kuwafyatulia risasi na msimamizi wa uchaguzi hakufuata taratibu za uchaguzi huo.

  Akisoma hukumu hiyo iliyochukua zaidi ya saa nne, Jaji Chocha alisema hakuna ushahidi wowote unaojitosheleza wa kutengua matokeo ya uchaguzi jimbo hilo, kwani mgombea wa CCM alishinda kihalali.

  Alisema katika hoja zote zilizotolewa na upande wa mashitaka, ikiwemo hoja ya rushwa, mashahidi wote walioletwa hawakuziunga mkono moja kwa moja hoja hizo, na pia ushahidi wao ulipingana, ikiwa ni pamoja na wengine kutokujiamini, hali iliyoashilia kuwa huenda ulikuwa wa kupangwa.

  Alisema kwa jinsi hiyo anaamini kuwa wananchi wa Jimbo la Mwibara, walitumia demokrasia yao vizuri kwa kuchagua mbunge waliyemuona kwamba anawafaa kuwaletea maendeleo na hivyo kuifungua kesi mahakamani ni kuwacheleweshea maendeleo yao.

  Alisema katika maelezo ya mashahidi wote akiwemo shahidi namba moja ambaye ni mlalamikaji, hakuona kama gari la ubalozi lilikuwa na makosa kwani picha zilizopigwa kama kielelezo zilionesha gari hilo likiwa limesimama, hivyo haamini kama gari hilo lilikuwa kwenye kampeni ya mgombea wa CCM, kama ilivyodaiwa.

  Kuhusu rushwa, Jaji Chocha wakati wa kesi inaendelea, hakuna shahidi ye yote aliyethibitisha moja kwa moja rushwa hiyo, aliipokea nani na hata waliopewa hawakufika mahakamani kuthibitisha hilo.

  Source: Gazeti la Habari Leo

  Poleni CDM
   
 2. P

  PETER NYAMWERO Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya ila kwa hili naenda tofauti na mahakama ni ya CCM ushaidi uliotolewa unadhihirisha taratibu hazikufuata maana naliisikia kec mwanzo mwisho ushahidi wa utetezi haukutosha kwa na amini Advocate Nyange na Kweka wataappeal kuhakikisha haki inatendeka.
   
 3. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kesi ya mbuzi kaliwa na simba kisha hakimu fisi. ulionaga wapi?
   
 4. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mahakam zetu na haki zao
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hayo ni mambo yakutazamiwa kabisa kwani kesi ya nyani kwamwe huwezikumpelekea ngedere, angalizo kwa ccm wajue muda wao utapita na ukishapita ktk kushikilia dola basi wajue ndo chama kimekufa kwani walio wengi wanajifanya kuwasapot kwavile wameshikia dola wakilia dola wakiachia ndo watayajua hayo kwa vitendo
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu nimeipenda hiyo
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ni wakati wenu wa mwisho magamba kutesa teseni sana kwakutofuata sheria mlizoziweka wenyewe kwani mwisho wenu upo karibu, nadhani sheria watakazoweka wenzenu watakaoshika dola ndo mtaweza kuzifuata na mkishindwa ni rais kuwalazimisha
   
 8. r

  robert palice Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama FFU ni CCM ije kuwa Mahakama!
   
 9. CtVKiLaZA

  CtVKiLaZA JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kangi alichakachua ila raia wameogopa kutoa ushahidi.
   
Loading...