ISMAIL MKIMBIZI
Senior Member
- Jan 13, 2013
- 192
- 23
Hakika ni kweli CHADEMA Kasulu kunafuka moshi na wakati wowote moto utalipuka. Mwenyekiti wa CHADEMA Kasulu BW Rajabu Bujoro amekuwa akifanya maamuzi yake binafsi kwa matakwa yake bila kufuata taratibu za kikatiba.
Ni ukweli usiopingika, mwenyekiti huyo hatoi Demokrasia ndani ya chama, mfano tazama aliwahi kuteua wagombea udiwani mwaka 2010 kwa mapenzi yake mwenyewe bila kufuata taratibu zozote. Aliwateua makada wawili kutoka CCM kazi ambayo sio ya kwake ambapo kwa kawaida kikatiba wenye mamlaka ya uteuzi wa wagombea kata na jimbo nafasi za udiwani na ubunge huteuliwa na Kamati Tendaji ya Jimbo husika.
Aliwateua makada hao wa CCM ambao ni Bw Mwononyi wa Kabanga kugombea kata ya Msambara na Bw Bomoa kugombea kata ya Kasulu mjini kitu ambacho kilipelekea CHADEMA kushindwa vibaya sana katika nafasi hizo.
Baadaye aliyekuwa kada wa NCCR MAGEUZI Bw. Haruna Kwasakwasa alihamia CHADEMA akamteua kuwa katibu wa chama bila kufuata taratibu za kikatiba nafasi nyeti ambayo sio ya kumpatia mtu baki ambaye hajaiva KI - ITIKADI ZA CHADEMA na hajakitumikia chama.
Kwa kuwa Bw Kwasasa amekalia kiti muhimu na uwezo wake ni mdogo na hajaiva kiitikadi za CHADEMA amekuwa akiendesha mambo ovyo ovyo ikiwa ni pamoja na kutengeneza mifarakano baina ya viongozi na wanachama. Na hii sio siri amekuwa akiropoka yeye na mwenyekiti hadharani akipiga vita baadhi ya wanachama na viongozi.
Tarehe 18.12.2012 Jimbo liliomba kibali katika kituo cha polisi cha wilaya Kasulu ili kufanya mkutano wa hadhara tarehe 22.12.2012 wakakubaliwa. Tarehe 19.12.2012 Jimbo wakatoa taarifa kwa barua kwa uongozi wa ngazi ya wilaya kuwataarifu kuwa kutakuwa na mkutano wa hadhara tarehe 22.12.2012 na mgeni rasmi atakuwa mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Mkoa Kigoma Bw. Jafari Kasisiko. Barua aliipokea Katibu wilaya Bw Haruna Kwasakwasa.
Maandalizi hayo yalifanywa kikamilifu na Jimbo, ajabu na kweli mwenyekiti Bujoro na katibu wake Haruna Kwasakwasa walifanya juhudi za kuzuia mkutano huo usifanyike. Tarehe 21.12.2012 walikimbilia kituo cha polisi wilaya kutoa taarifa ili mkutano uzuiliwe usifanyike, ambapo Mkuu wa Polisi Kasulu aliwaandikia barua Jimbo wafike kituo cha polisi 22.12.2012 saaa 03:00 asubuhi.
Jimbo waliitikia wito wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jimbo Bw Pindu, akifuatana na katibu wa Jimbo Bw. Lukas , Katibu Mwenezi wa Jimbo Bw. Kaijage, Kamanda wa Vijana Bw. Masoud Bigangika pamoja na Katibu wa Baraza la Wazee Bw. Juma Vuruga. Upande wapili wa walalamikaji alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya Kasulu na Katibu wake Bw. Kwasakwasa.
Baada ya vuta ni kuvute mjadala ulifikia mahali ukategemea hekima za Mkuu wa Polisi Kasulu aliyekuwa akisaidiwa na Mkuu wa Upelelezi kushauri mkutano ufanyike na tofauti nyingine zikajadiriwe baadaye katika vikao vya ndani vilivyo halali kikatiba. Mkutano ulifanyika lakini cha ajabu Bw Bujoro na Bw Kwasakwasa hawakuhudhuria japokuwa walialikwa na badala yake walionekana wakilandalanda mitaani wakisikilizia kwa mbali.
Amaa kweli ukistaajabu ya MUSA utaona ya FILAUNI. Tatizo kubwa Bw Bujoro huwa hashauriki. Aliwahi kutamka mwenyewe kwa kauli ya kichochezi juu ya uchomaji wa makanisa. Akihojiwa alisema "... makanisani sio mahali patakatifu, wanaruhusu mabinti kuingia wakiwa uchi ... hivyo ni a halali yachomwe moto.." Aliendelea kuhojiwa ni vipi kiongozi wa chama kutoa matamshi kama hayo huoni ni kosa? Alijibu kuwa anatetea imani yake ya kiisilam.
Moja ya wafanyabiashara waliokuwapo KAHAWANI alimwambia kama anataka kutetea imani yake aachie kiti aende akawe Imamu au Shehe wa msikiti kwa kuwa CHADEMA haina UDINI, UKABILA, RANGI wala JINSI. Sijui Bw. Bujoro kichwa chake kina nini kiasi cha kutojua atamke nini miongoni mwa wanajamii ambapo kuna watu wenye imani tofauti na mitazamo tofauti. Alipoambiwa kuwa amefanya kosa kubwa na afute kauli yake alisema hajakosea kwa kuwa amelisema KAHAWANI na sio JUKWAANI.