CHADEMA what is the next move? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA what is the next move?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gollocko, Jan 9, 2012.

 1. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  Kwenu CHADEMA

  Mimi kama kijana wa kitanzania, naona mambo hayaendi kabisa ndani ya nchi yangu ambayo nitake nisitake bado ndo hatma ya maisha yangu ilipo. Na si mimi tu bali vijana wengi nao wapo katika mkumbo ule ule wa kuganga njaa kila kukicha na si kutafuta ziada kwa ajili ya maendeleo yawe binafsi au ya kitaifa.
  Kutokana na misukosuko hii vijana wengi na matabaka mengine (wapenda mabadiliko) wamejikuta wakiwekeza imani yao kwa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) nami nikiwa mmoja wao. Ingawa sina kadi ya chama chochote ila matumaini yangu yapo kwenye chama hiki ambacho kianoneka na mtazamo sahihi wa kulikomboa Taifa letu hasa kwa jinsi kinavyokabili baadhi ya matatizo ya kitaifa.Jambo ninalotaka kufahamu hapa ni kipi kinafuata kwetu sisi kama wafuasi wa chama hiki na wale waliowekeza imani yao katika chama hiki. CCM ni chama kilichopoteza mwelekeo kabisa, kilichobaki kwao ni kutumia fedha na vyombo vya dola katika kujibakiza madarakani, hivyo hapa panahitajika nguvu ya ziada katika kutetea maslahi ya nchi hii ambayo yako mikononi mwa wachache tu na walio wengi wakihangaika wasijue wafanye nini.

  Katiba Mpya

  Suala la kudai katiba mpya lilianza zamani ingawa msukumo mkubwa ulikuja baada ya CHADEMA kulivalia njuga hasa katika uchaguzi uliopita. Huko nyuma vyama vya NCCR Mageuzi na CUF walijitahidi bila mafanikio mpaka maandamano makubwa (ya CHADEMA) ya mwezi January 2011 ndiyo yaliyomsukuma mweshimiwa rais kujitokeza na kuahidi suala hilo kulipatia ufumbuzi(Ingawa ni kisanii zaidi) . Nasema ni kisanii kwani chama chaake cha CCM , katiba mpya haikuwa sera yake hivyo waliibeba tu kupoza joto lilikuwapo kipindi kile. Lakini tukumbuke lengo kuu la katiba mpya pamoja na mambo mengine lilikuwa ni Tume huru ya uchaguzi, maana hii iliyopo ni ya CCM kwani inateuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho na mfumo tulionao hauwezi kutofautisha ni wakati gani rais ni rais wanchi na wakati gani ni mwenyekiti wa CCM, maana utaskia raisi anahutubia wazee wa Dar es Salaam halafu unakuta wazee wote ni makada wa CCM na ukumbini ni Uniform za CCM tu ndo zimejaa. Hapa ndipo tunaposema tume ya uchaguzi ni ya CCM kwani imechaguliwa na Mwenyekiti wa chama hicho.Baada ya chama tawala kuiteka hoja hii (Kuunda Katiba Mpya) sasa imeanza kupoteza mwelekeo, kwani inaelekea katiba yote itaundwa kwa matakwa ya wanaCCM na siyo kwa matakwa ya wananchi walio wengi. Hapa yaonekana nguvu zote za chama na serikari zitatumika kuisupport hii inayoitwa katiba mpya ya serikali na chama chake. Na hapa nabashiri bado kuatakuwa na madai ya katiba mpya hata baada yahii kutengenezwa upya kama mchakato unaoendelea sasa hivi utaachwa uchukuwe nafasi kwani, vyombo vyote vya dola hasa vinavyogusa maisha ya watu ya kila siku vitatumika kuilazimisha katiba hii ipite.

  Polisi

  Jeshi hili la polisi limekuwa kama jumuiya ya nne ya chama cha mapinduzi (Ukiacha jumuia ya wanawake, wazazi na ile ya vijana) kwani limekuwa likitumika wazi wazi kuibeba CCM (rejea kwenye matukio uchaguzi mkuu uliopita na maandamano ya UVCCM ya Arusha na yaliyomkuta bw.Lema). Inajulukana wazi CCM haitaki harakati za wananchi kudai haki zao. Wabunge wake walikuwa mstari wa mbele kupinga maandamo ya CHADEMA mwaka uliopita na mara zote bungeni na kwenye vikao vya chama wamekuwa wakitoa maagizo kwa polisi kuhakikisha inazibiti maandamano hayo yawe kwa shari au kwa kheri. Na serikali na chama chake vimekuwa vikilikumbatia jeshi hili hata pale linapofanya makosa ya waziwazi (Kumbuka mauwaji ya Tarime na Arusha).Katika ripoti ya mwaka jana (2011) ya taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) ilionyesha kuwa Jeshi la polisi ndilo liaongoza kwa vitendo vya rushwa kuliko taasisi zote za serikali, lakini cha kustaajabisha si rais.serikaili wala chama tawala vilivyoingilia kushughulikia swala hilo. IGP (Ambaye mi namwona kama mwenyekiti wa jumuia ya polisi katika CCM) naye yupo kimya kama jambo hilo ni la kheri. Kwa kifupi hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Unafikili ni kwasababu gani? Ni kwasababu haina madhara kwa serikali wala chama tawala bali kwa wananchi ambao sio muhimu kwao.Ukiuliza utaambiwa jeshi linafata sheria na taratibu zilizopo(ingawa ni kwa upande mmoja wa watawaliwa). Sheria na taratibu tumezinukuu kutoka Uingereza lakini tujiulize, Ulishawahi kusikia nchini Uingereza polisi wakatawanya maandamano kwa kuua bila kuadhibiwa? Je, polisi Uingereza wanakamata waharifu kwa makofi bila kuchukuliwa hatua?. Ukitazama kwa makini utendaji wa leshi letu utagundua linaendeshwa kama la kikoloni hasa kipindi cha mwingereza na siyo kama taasisi ya wananchi kama inavyodaiwa na watawala, maana kubambikiza kesi,kuua na kuzima harakati za kiraia kwao ndiyo kazi yao.Hapa utagundua jeshi hili litatumika na watawala kuzima harakati zozote za wananchi kuipinga mawazo ya viongozi wa serikali na chama tawala katika mchakato mzima wa katiba mpya. Hii tumeiona katika maandamano ya kiraia, ambapo tunaambiwa hayaruhusiwi kwa sababu ya tishio la Al shabaab, cha kushangaza huko Kenya ambao wanapambana na kikundi hicho hakuna marufuku hayo, huku sijui inakuwaje sisi tusiopambana nao na tuko mail nyingi kutoka kwao. Kwa hiyo kwa kutekeleza maagizo ya CCM leo polisi wamepata pa kushikilia! Lakini tujiulize, kundi la Al shabaab lipo kwa muda sasa na litakuwepo kwa muda mrefu ujao( Maana juhudi za kulitokomeza ni dhaifu) . Je, watanzania tutaendelea kusitisha harakati zetu mpaka lini? Maana kundi hilo si leo wala kesho kwamba litatoweka?. Na Je, jeshi letu halina uwezo wa kulinda raia wake dhidi ya vitisho vya kundi hili mpaka lizuie harakati za raia wake?

  Usalama wa Taifa

  Hii idara nayo inaonekana kama ni jumuia ya tano ya CCM, licha ya kufanya kazi zake kwa siri, lakini malalamiko mengi yapo kwa idara hii kutumiwa na chama tawala( Rejea madai ya Dr. Slaa katika uchaguzi uliopita juu ya idara hii). Wizi wa kura, njama za mauaji kwa wapinga ufisadi(Rejea ripoti ya Dr. Mwakyembe) na taarifa za kiinteligisia za kuibeba CCM( Zile za maandamano ya Arusha) pamoja na matukio mengi yanayoiichafua idara hii. Maelekezo mengi ya kiinteliginsia hutolewa kutoka idara hii na bahati mbaya yote yapo kuibeba CCM tu(Rejea maelezo ya mchungaji Msigwa bungeni). Bahati mbaya kwa idara hii hufanya kazi zake kwa siri hivyo sio lahisi kujitokeza hadharani kukanusha lakini ishara zinaonyesha watatumiwa vilivyo na watawala kuahakikisha katiba ijayo ianakuwa kwa matakwa ya CCM.

  Amani

  Amani hii tunayohubiliwa wanaifaidi wachache tu, nao ni watawala na ndugu na jamaa zao wa karibu. Amani inahubiliwa sana na watawala kuliko watawaliwa kwanini? Sababu ni moja hawajali watu wengine wanachojali ni familia zao, biashara zao na mali zao kwani itokeapo vita zitatoweka na hawatarithishana madaraka wanao au ndugu zao. Lakini tujiulize ni kweli watu wa Manzese wanahitaji amani ya kuona wenzao wa Oyestabey wakipata huduma zote za jamii na wao wakibana kwenye vibanda ambavyo wao wanaita nyumba? Mgao wa umeme uswahilini, matatizo ya maji uswahilini, barabara mbovu uswahilini, vibaka uswahilini, je, hawa somo la amani linapanda kweli? Hapana! labda kwa wale wa Masaki na Oyesterbay ndio somo hili liatapanda kwani kwao ni raha tu na ikija vita au machafuko raha zote zitapotea.

  Nini cha kufanya

  Hapa sasa ndipo ninapokiomba CHADEMA kwa kuwa ndio chenye wafuasi wengi wanaotaka kuona mabadiliko ya kuhakikisha keki ya taifa inaliwa kwa usawa kutupa wayforwad ya nini kifanyike, maandamano yamezuiwa, kukosoa mchakato wa katiba ambayo tuliona ndio tumaini jipya unakwenda jela, sasa hapa nini cha kufanya? Maana katiba mpya sio kuiondoa CCM madarakani na kuiweka CHADEMA, bali kuwapa uwezo wananchi kuchagua na kuwawajibisha viongozi wao pale wanaposhindwa kutekeleza waliyowaagiza bila kuingiliwa na watu wanje au kupangiwa nini cha kufanya badala ya wanachi wenyewe kupanga nini cha kufanya.Mwisho nawaomba viongozi wa CHADEMA kutafuta kwa haraka suluhisho la wizi wa kura kwa kuhakikisha mara uchaguzi unapofanyika kura zinalindwa kwa nguvu zote, vinginevyo watu watakata tamaa ya kupiga kura, kwani watajua hata wakikesha kwenye mistari ya kupiga kura usalama wa kura zao ni mdogo au haupo. Kumbukeni NCCR Mageuzi walipendwa lakini walishindwa kilinda kura zao, ikaja CUF nao wameshindwa kulinda kura zao. Sasa hili liwe somo kwenu ili muwe tofauti, malalamiko tu kwenye vyombo vya habari haisaidii kwani wameweka watawala pamba maskioni na madaraka ni matamu kwao

  Dr. Slaa,Mnyika,Mtema au kiongozi yeyote hapo chamani hebu tupeni mwongozo tafadhali!

  Adios wanajamvi!
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  unamwamini sana slaa na mchungaji feki msigwa ee?kijana unaonekana umesoma lakini hujaelimikan yaani ulikuwa una desa sana hukuwa unaishughulisha bongo yako.uwe unaangalia na upande wa pili wa shilingi utaifaidi siasa kaka.
   
 4. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  Huo upande unaosema umeangaliwa sana kwa miaka hamsini na hausomeki
   
 5. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  Haa yaani wewe hapa ndo umeiona hayo ya mgomo wa madaktari tu ndo ufumbuzi wa yote? Acha kutumia masaburi!
   
Loading...