CHADEMA wazidi kuigaragaza CCM Njombe

CHADEMA wazidi kuigaragaza CCM Njombe

inachekesha, chadema siku hizi wanashinda mahakamani ikija kwenye kapu la kura less than 10%. JITATHIMINI.

Wewe si mmoja wetu hivyo mawazo yetu na maono yetu kwa vyovyote vile yatatofautiana na yako
 
Hizi kesi ufunguliwa nyingi wakati wa uchaguzi kupoteza attention ya wagombea pinzani na kuwakatisha tamaaa ktk harakati za ukombozi na zakimaendeleo.

Imagine muda na rasilimali zilizotumika kwa kesi zote kabla na baada ya chaguzi mbalimbali hapa nchini zilizofunguliwa na maccm! Kuna pepo la umaskini linaizingira hii nchi kupitia maccm (mifumo ya siasa za ccm). I hate it!
 
MAHAKAMA ya Wilaya ya Njombe imetupia mbali kesi iliyokuwa ikiwakabili viongozi wa CHADEMA mkoani hapa, ya kutishia kummwagia tindikali Mbunge wa Njombe Kaskazini, Deo Sanga (CCM) maarufu kama Jah People.

Sanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe, alidai kukumbana na tishio hilo wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Njombe mjini.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Malya, alisema kesi hiyo iliyokuwa chini ya Hakimu Augustino Rwizele, ilitupiliwa mbali kwa kutumia kifungu cha 91 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Alisema kuwa shitaka la kwanza lililokuwa likiwakabili viongozi hao ni lile lililotokea Februari 3, mwaka huu, ambapo washitakiwa Ali Mhagama, Robert Shejamabu na Award Kalonga walidaiwa kuvamia kikao cha CCM na kutishia kummwagia tindikali mbunge huyo.

Shitaka la pili lilimhusu Emmanuel Mwasongwe ambaye ni msaidizi wa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Jeshi la Polisi mkoani Njombe.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa, viongozi wa CHADEMA waliviomba vyombo vya dola pamoja na mahakama kuendelea kufanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi zao ili kila mwananchi apate haki yake.

Katibu wa CHADEMA Kata ya Njombe Mjini, Ali Mhagama aliwataka wananchi kuwa makini katika chaguzi mbalimbali zijazo kwa kuchagua viongozi ambao watajali maslahi ya umma.

"Tunamshukuru Mungu kwa kushinda kesi hii, na endapo tungepatikana na hatia leo hii, bila shaka kungekuwa na pengo kubwa katika utendaji wa kazi za chama," alisema Mhagama.

Kalonga, alisema pamoja na kupigwa katika tukio hilo kiasi cha kuvunjwa taya, alishangaa kupelekwa polisi na kufunguliwa mashitaka huku akiwa ana maumivu makali.

"Siku hiyo nilivunjwa taya, baada ya hapo tulikimbia na kujifungia, lakini jambo la kushangaza ni kwamba tulipelekwa polisi na wakatufungulia mashitaka," alisema Kalonga.

Akizungumza mara baada ya hukumu hiyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe, Clemence Mponzi, alikiri kuwa chama chake kilishindwa kwenda kutoa ushahidi na hivyo kuifanya mahakama itoe uamuzi wake.

Katika uchaguzi huo mdogo uliofanyika Februari 9, mwaka huu, CHADEMA ilishinda kupitia mgombea wake Joseph Mtambo, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Lupyana Fute.

Chanzo; Tanzania Daima
 
Viva Chadema, hakuna kulala..

Maccm kazi kufungua makesi yasiyo na kichwa wala miguu.
 
kuwafunga wafuasi wa cdm ni sawa na kumfunga chokora, watu wenyewe hawaelewek na chama chao naona hakimu kawaonea huruma
 
Wewe si mmoja wetu hivyo mawazo yetu na maono yetu kwa vyovyote vile yatatofautiana na yako
haya mkuu. nilikuwa nashauri tu lakini. mimi niko kiuhalisia zaidi wakati wengine ukiwemo wewe mko biased. kwa hiyo huwezi ona upande wa pili hata siku moja.
 
Back
Top Bottom