CHADEMA waweka mkazo Serikali za majimbo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
12 APRIL 2012



Na Raphael Okello, Bunda

CHAMA cha Demokrasia na Mae n d e l e o (CHADEMA) kimesisitiza kuwepo kwa serikali ya majimbo ambapo kimewaomba wananchi kuzingatia suala hilo watakapotoa maoni wakati wa mchakato wa uandikaji wa Katiba Mpya.

Akiwahutubia mamia ya wananchi mjini Bunda mkoani Mara hivi karibuni Mbunge
wa Jimbo la Nyamagana Bw. Ezekiel Wenje aliwataka Watanzania kuingiza katika Katiba Mpya ijayo utawala wa majimbo kwa kuwa ndio njia pekee itakayowawezesha wananchikufaidi uwepo wa rasilimali ya nchi.

"Hatuwezi kufaidi rasilimali ya nchi kama mfuko wa taifa utaendelea kuwa mmoja...kwa kuwa wapo viongozi wajanja wanaotumia vibaya mgao huo ambapo fedha nyingi huishia katika mfuko wao huku wananchi wakitaabika," alisema Bw. Wenje.

Alisema zipo kanda ambazo zina rasilimali nyingi lakini hazina maendeleo ambapo alitoa mfano kwa Kanda ya Ziwa ambapo alisema kanda hiyo inamiliki rasilimali nyingi ya taifa ikiwa ni pamoja na rasilimali watu, madini,ziwa, wanyamapori, samaki na zao la pamba lakini kanda hiyo bado iko nyuma katika huduma za jamii na kwamba haina hata Chuo Kikuu kimoja cha Serikali.

Aliwataka wakazi wa Kanda ya Ziwa na kanda zingine kuhakikisha kuwa ajenda hiyo inakuwa ni ya kikatiba na si ya chama cha siasa kwa kuwa inagusa utaifa.

"Idadi ya Watanzania inakadiriwa kufikia milioni 45 na kati ya hao milioni 15 wanatoka kanda ya ziwa...na katika nchi hii mgombea yeyote wa kiti cha urais lazima atafute kupata ukubali kutoka Kanda ya Ziwa ili apate uhakika wa kushinda," alisema Bw. Wenje.

Kwa mjibu wa Bw. Wenje kupitia mgawanyo wa mapato ya rasilimali katika serikali ya majimbo ni asilimia 20 ya mapato yote ndio itakayowasilishwa katika mfuko wa pamoja wa taifa ili kufidia majimbo yenye rasilimali kidogo na shughuli za jumla za umoja wa kitaifa.



 
Wenye 'akili' zilizopevuka ndio wanaweza kuliona hili.
Utawala wa majimbo ni namna mojawapo ya msingi yakupiga maendeleo.
I support that.
 
Utawala wa majimbo ndo suluhisho kwa uchumi kilema kama wa nchi yetu, utawezesha ukusanyaji rahisi wa kodi, utaleta ufanisi stahiki ktk miradi ya kimaendeleo, utapunguza na kuondoa mzigo wa idadi kubwa ya viongozi usio na tija, utawezesha ulindaji wa raslimali za eneo husika
 
Utawala wa majimbo ndo suluhisho kwa uchumi kilema kama wa nchi yetu, utawezesha ukusanyaji rahisi wa kodi, utaleta ufanisi stahiki ktk miradi ya kimaendeleo, utapunguza na kuondoa mzigo wa idadi kubwa ya viongozi usio na tija, utawezesha ulindaji wa raslimali za eneo husika
Haya yote yalisemwa kuhusu serikali za mitaa.
 
Na ndiyo itakuwa suluhisho la kupeana vyeo kienyeji!! Inshu nyingi zitakwenda sawa, ingawa ni mwanzo pia wa kuanza kufikiria kujitenga kwa jimbo moja kuwa nchi.
 
Ukisha kuwa gamba hata uelezwe vipi mambo ya msingi uwezo wa kufikiri ni zero..
Na ukishakuwa gwanda kila jambo litalosemwa na mitume wenu mnaona ndiyo suluhisho.Hivi unafikiri kanda ya ziwa ina rasilimali nyingi kuliko kanda ya kusini?
hovyoooo!!!
 
Wenje kanena kwa wanofuatilia hatua alizokuwa anapitia nyerere katika uongozi wake utagundua kuwa aliwahi ku-apply utawala huu pale aliposema utawala na maendeleo mikoani.Wao cdm wanakwenda mbali zaidi kwa ku-consolidate baadhi ya mikoa na kuwa state.Hapo state kwa state zitainuana kwa kushindana.Big up Wenje, umenifurahisha sana katika harambee yako ulipowahusisha wazoefu wa harambee kutoka kenya.Raila Odinga no mtoto wa Mwanza yuleeeeeeeeee, mnajua hiloooo??????
 
Haya yote yalisemwa kuhusu serikali za mitaa.

wewe una lako jambo. serikali za mitaa ni tofauti sana na serikali za majimbo.

1. serikali za mitaa, mkuu wa mkoa, wilaya, mkugenzi, RAC, na viongozi wengine wa mikopa na wilaya wana harufu ya uchama, na hawawajibiki kwa wananchi bali kwa aliyewateua, lakini serilai za majimbo, kama mkuu wa mkoa=gavana, wilaya atatokana na kura za watu, hivyo atawajibika kwa watu waliomchagua na akienda kinyume na matakwa ya watu anaondoshwa.

2. na kwa habari ya watendaji wa serikali, wataajiriwa na majimbo na hivyo kuwajibika kwa majimbo yao na si vinginevyo
 
Hii imekuwa sera ya cdm tangu mwaka 2000. Tatizo letu watz ni kuchukua muda mrefu kuelewa jambo!
 
Na ukishakuwa gwanda kila jambo litalosemwa na mitume wenu mnaona ndiyo suluhisho.Hivi unafikiri kanda ya ziwa ina rasilimali nyingi kuliko kanda ya kusini?
hovyoooo!!!

ok. wote wana rasilimali na zimekuwa zikitumika kwa miaka 50 ya uhuru. wanajivunia kuwa nazo kuwa zimewasaidia?
 
Hii sera ianzange haraka na kwa vile cdm wanakuanga calculative mambo itakua ok at the end.....
 
Na ukishakuwa gwanda kila jambo litalosemwa na mitume wenu mnaona ndiyo suluhisho.Hivi unafikiri kanda ya ziwa ina rasilimali nyingi kuliko kanda ya kusini?
hovyoooo!!!

kobello tokea mwanzo umeonesha uelekeo wa kupingana na uwepo wa mfumo wa serikali za majimbo na kwa mbali umeonesha kuunga mkono serikali za mitaa....lakini kwa hii post yako ya hapo juu naona km nawe kwa jinsi fulani unakubaliana na uwepo wa majimbo hata umegundua kuwa upande wa kusini nako kuna rasilimali za kutosha
 
Back
Top Bottom