Plato
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 420
- 94
Jana ilikuwa siku ya ile kesi ya Lwakatare na Ludovick. Gazeti la Mtanzania limeanza kuchapisha mfululizo wa mahojiano liliyofanya na Ludovick kuhusu kuhusishwa kwake na mambo mbalimbali ikiwamo ugaidi.linaendelea jumapili ijayo. sasa chadema kwa hofu yao kuwa yawezekana ametoboa siri kuu ya uongo wa chadema kuwa mkanda wa video ya Lwakatare ulikuwa kweli na ni yeye aliurekodi, walikuwa wanaomba mahakama isuie gazeti la Mtanzania liache kuchapa mahojiano yake na Ludovick.
Hakimu, Mh. Mchauru akakataa ombi hilo na kusema kwa kuwa CHADEMA wanaongelea kuwa gazeti linachapisha mambo yanayomhusu mtuhumiwa namba mbili Ludovick na kwa kuwa wao siyo mawakili wa Ludovick, basi waache Ludovick mwenyewe alalamike kwani anao mdomo. na akasema anawaekeza kuacha kuingilia mambo ya mtuhumiwa namba mbili,Ludovick kwani wao siyo mawakili wake.
Ludovick alipoulizwa kama ana la kuongea, hakuongelea mambo ya gazeti, jambo ambalo liliwaumbua sana upande wa Lwakatare. hakika iko siku uongo wao utaanikwa tu.