KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,153
Kamati kuu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imetangaza kutambua na kuridhishwa na kazi iliyofanywa na tume ya mabadiliko ya katiba ambapo pia imejadili maudhui yaliyomo kwenye rasimu ya katiba tayari kwa kuyatolea mapendekezo.
Kuhusu maamuzi ya kikao cha kamati kuu iliyoketi Dar es salaam July 6 -7 2013, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema mbali na kuainisha mapendekezo yanayostahili kuboreshwa, wamezikataa taarifa na kuzikanusha kwamba wamemtaka mmoja wa wajumbe ambae ni mwanachama wao Profesa Mwesiga Baregu kujiondoa ndani ya tume ya mabadiliko ya katiba.
Namkariri Freeman Mbowe akisema "tumeona mambo mengi yenye maslahi ya taifa, bado tumeona kuna mambo yanakwaza haki na demokrasia katika taifa ila hayo yote tusingependa kuchanganya na haya matukio mengine ya unyama…. hayo yote tutayatolea msimamo pamoja na vitabu na nini CHADEMA tunakwenda kufanya kwa nchi nzima kuhusiana na mchakato wa katiba"
NUKUU MUHIMU:"If I'm told to choose between my party and my country, I will choose my country"-PROF BAREGU