CHADEMA watua ICJ, kupeleka mashitaka ya uchaguzi Mkuu

CHADEMA watua ICJ, kupeleka mashitaka ya uchaguzi Mkuu

Status
Not open for further replies.

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
12,489
Reaction score
39,969
Wanasheria mahiri wa CHADEMA wakiongozwa na Tundu Lissu wamefika katika mahakam ya kushughulikia mashitaka dhidi ya haki ya ICJ kupeleka rasmi mashitaka yao dhidi ya hujuma na udhalilishaji juu ya uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015.

Wanasheria hao ndiyo wanaosubiriwa na uongozi wa Chadema/UKAWA kuleta mrejesho kabla ya kuchukua hatua zaidi dhidi ya tume na Chama Cha Mapinduzi kutokana na hila zilizofanyika.

=======================

Updates:

Tumaini Makene said:

Salaam wapiganaji

Ziko habari zimezushwa, kuenezwa na sasa zinakuzwa kuwa mgombea urais wa CHADEMA na chama kwa ujumla kimefungua shauri Mahakama za Kimataifa, kuhusu ubakwaji wa demokrasia na hujuma dhidi ya Watanzania uliofanyika kwenye Uchaguzi (uchafuzi?) Mkuu uliofanyika Oktoba 25.

Itoshe tu kusema kuwa hadi kwa hatua ya sasa habari hizo si za kweli. Ni uzushi.

Watawala, wanaotuhumiwa kupoka haki ya Watanzania ya kuchagua viongozi wanaowataka, wanajua dhambi waliyowafanyia wananchi ni sawa na ile hadithi ya Mzee Mvuvi kwenye Vitabu vya Alfu Lela Ulela, aliyefungulia jini kutoka kwenye chupa. Dhambi inawawinda. Mzimu wa walichokifanya unawaandama. Maana safari hii ukatili (kuvuruga uchaguzi) ulikuwa wazi wazi mno.

Wanajaribu kuchokonoa kujua ukimya wa Ndugu Edward Lowassa, kama mgombea chaguo la watu, CHADEMA, UKAWA na wapenda mabadiliko unaweza kuwa na kishindo gani! ICJ, ICC au wapi hasa!

Hivyo wanatunga tunga mambo na kusambaza wakitaka kupima hisia, fikra za wanamabadiliko waliotapakaa nchi nzima wakilia kilio cha kudhulumiwa haki katika uchaguzi, zinawaza nini! Maana hata wao wanashuhudia namna nchi ilivyokumbwa na msiba tangu walipotangaza matokeo yasiyooana na uhalisia wa hisia za wapiga kura na matakwa ya waliyo wengi katika demokrasia.

Tumelazimika kufafanua kuhusu uvumi huo kwa sababu umezidi kuenezwa kiasi cha vyombo vya habari kuanza kuulizia ukweli wake.

Baadhi ya watu waliotajwa kwa majina katika uvumi huo wako hapa nchini, wakiendelea na majukumu, hususan vikao vya Kamati Kuu ya dharura, ambayo imekuwa ikikutana jijini Dar es Salaam.

Chama kilipoandika barua kwenda Jumuiya ya Kimataifa, kuhusu hatari iliyokuwa inawekwa na watawala katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kupitia kauli za vitisho, matendo yao ya kujiandaa kuharibu uchaguzi, BVR, mfumo wa ujumlishaji matokeo n.k, tuliutaarifu umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari na njia zingine za upashanaji habari. Kwa sababu si siri.

Ukifanywa uamuzi mwingine wowote ule kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania kupigania haki yao iliyoporwa katika uchaguzi mkuu, umma wa Watanzania ambao ndiyo wenye mamlaka katika nchi, utashirikishwa.

Makene.
 
yani shamra shamra hakuna as if kuna msiba ivi kilichotarajiwa sicho kilichotokea watu wamekata tamaa kabisa
 
I expected the same.

Tuwapongeze kwa vile wamechagua njia ya ki diplomasia badala ya short cut.
 
SAfiiiiiiii... safinaaaaa...!!! 👏👏👏✌✌🙌🙌🙌🙌🙌

Naanza KUTABASAMU...!!!

ICC wajeeeeee...wajeeeee...!!
 
Hilo ni jambo la maana sana.

Support yangu mnayo. Uhuni huu wa ccm lazima ufike mwisho.
 
hakuna kitu hapo hatuwezi kumpa nchi LOWASSA.
 
Hata wakienda I.C.U mwisho wa siku watarudi bongo na Magufuri ndo rais wetu ..mkaamia maji daima hayanywi.
 
Nafikiri hiyo ni busara na Hekima ya viongozi wa UKAWA.
 
Naomba mtu anielekeze vizuri.. Anifafanulie.. Kwamba hawa jamaa huko ICC kuna faida gani? Ina mana ICC ndio wana uwezo wa kushighulika na matokeo ya ndani ya nchi?
 
kwa nini watuchagulie magufuli ambae hatukumchagua?huu ni uhuni uliotukuka
 
Hahahahhaha...watanzania bana..wanadhanani kila kitu kinakubalika ICC...we are living in a crazy world!
 
Tena, This case they can WIN IT... kwa hoja rahisi tu, ya VOTE RIGGING...!!! Sbb copies za MIKOA yote Matokeo ya UCHAGUZI wanazo..!!!

Na Lowassa, Chadema, kapata 10.2 Mil. Votes...!!!

So, NEC watakipata...!! 👏👏✌✌
 
Kila la kheri makamanda. Pambano halijafika mwisho, ila ICC inaweza kuleta haki?? Nlidhani wanahuzika na mashitaka ya makosa ya kivita zaidi. Sijui lakini, ila nilitamani kama wangeenda kwenye nchi wahisani na marafiki ili waisusie Tz. Nsema, sijui. Haya ni mawazo yangu tuu
 
Siamini kama itasaidia chochote kwani Tanzania ni nchi huru yenye uwezo wa kujiamuria mambo yake wenyewe bila kuingiliwa na mataifa ya nje.

Hii ni njia nzuri ya kusaidia kupunguza hasira ya watu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom