Chadema wateswa na CCM

Ni kata ngapi CCM imefanikiwa kuzirejesha toka kwa wapinzani wao wakuu CHADEMA?? Hapa unafanisha na mfano huu:

"Mtu ana watoto 29 kwa bahati mbaya watoto 5 wanafariki eti ataona hakuna tatizo kwa sababu bado wapo wengine 24 " Mchungaji mzuri ni yule anaye jikagua kwa nini kondoo mmoja tu anapotea

Bado katika mtazamo wangu naona CHADEMA wamefanya vizuri tu tukizingatia kuwa wapinzani wa CHADEMA si CCM tu bali wapo wengi including CUF !!!
 
Kitakwimu ccm wamepoteza na chadema wameongeza! lkn jambo la msingi kwa chadema nikuendeleza harakati na kujipanga zaidi
 
Wanapiga propaganda sana mbaya zaidi ni watu wa media mtabaki kulia kuibiwa kura ccm wako vizuri sana ngazi zote chadema hawataki kukosolewa
 
kukishakuwa na chaguzi nyingi kwa wakati mmoja nafikiri huwa inakuwa tatizo kwa CDM ukifananisha na kukiwa na chaguzi moja. mfano uchaguzi mkuu uliopita na huu wa madiwani utaona akina Dr. Slaa na Mbowe ndiyo wanasubiliwa kila kona wakafanye kampeni. nafikiri suala linalotakiwa (sijui uchaguzi ndani ya CDM unafanyika lini) ni kuwa na viongozi wengi wenye uwezo na wanaoamini kila kona ya nchi ili wasaidie katika mapambano. huko nyuma lilishazungumzwa hili kwamba wawepo viongozi wa kitaifa wasio wabunge badala ya kuwarudikia vyeo akina Zito, Mnyika nk
 
Back
Top Bottom