CHADEMA watangaza bendera zake nchi nzima kupepea nusu mlingoti kufuatia kifo cha Mzee Ndesamburo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
upload_2017-6-1_12-9-1.jpeg


CHADEMA: yatangaza kupeperusha bendera yake nusu mlingoni ktk matawi yake nchi nzima kufuatia kifo cha Mbunge wa zamani, Philemon Ndesamburo

Kuhusu kukamatwa Yericko Nyerere CHADEMA yasema lipo chini ya ufuatiliaji wa chama. kwa sasa wanasimamia msiba wa Mzee Ndesamburo .

CHADEMA: Mzee Ndesamburo alitoa gari mbili kwa mara ya kwanza ilipoanzishwa CHADEMA .

CHADEMA: Mzee Ndesamburo ndiye aliyefadhili chama kwa mara ya kwanza kwa kukipatia ofisi yake maeneo ya Kisutu.

Naibu Katibu Salimu: Kwa mzee Ndesamburo nilijifunza "determination", alijitoa kwa kila kitu kuijenga CHADEMA.

Naibu Katibu Salimu: Wafanyabiashara wa leo ukiwaambia wapiganie mapinduzi wanaruka mia 100, ila Mzee Ndesamburo hakuwa hivyo.

Naibu Katibu Salim: Mzee Ndesamburo alikitoa chama cha Chadema toka wabunge 3 hadi sasa 72.

Naibu Katibu Salimu: Mzee Ndesamburo aligombea ubunge si kwa kupata fedha bali kutumikia watu.

Naibu Katibu Salimu: Mzee Ndesamburo hadi umauti unamkuta alikuwa ameshika kalamu kusaini hundi kwa Lucky Vincent. Mzee alikuwa mtu wa watu.

Katibu Mkuu CHADEMA: Mzee Ndesamburo alikuwa mfanyabiashara huku akifanya mapinduzi katika siasa.

Katibu Mkuu CHADEMA: Maisha aliyoishi mzee Ndesamburo yalilenga kutujenga katika Umoja kama taifa.
 
Muda huu viongozi wa Chadema wanaongea na waandishi wa habari. Tutawaletea yanayojiri kwenye mkutano huo.

Naibu Katibu Salimu: Kwa mzee Ndesamburo nilijifunza "determination", alijitoa kwa kila kitu kuijenga CHADEMA.

Naibu Katibu Salimu: Mzee Ndesamburo aligombea ubunge si kwa kupata fedha bali kutumikia watu.

Naibu Katibu Salim: Mzee Ndesamburo alikitoa chama cha Chadema toka wabunge 3 hadi sasa 72.

Naibu Katibu Salimu: Mzee Ndesamburo hadi umauti unamkuta alikuwa ameshika kalamu kusaini hundi kwa Lucky Vincent. Mzee alikuwa mtu wa watu.

[HASHTAG]#CHADEMA[/HASHTAG]: Mzee Ndesamburo ndiye aliyefadhili chama kwa mara ya kwanza kwa kukipatia ofisi yake maeneo ya Kisutu.

CHADEMA: Mzee Ndesamburo alitoa gari mbili kwa mara ya kwanza ilipoanzishwa CHADEMA .
CHADEMA wametangaza bendera zake nchi nzima kupepea nusu mlingoti mpaka pale mzee Philemon Ndesamburo atakapozikwa.

Katibu Mkuu CHADEMA: Maisha aliyoishi mzee Ndesamburo yalilenga kutujenga katika Umoja kama taifa.

Katibu Mkuu CHADEMA: Mzee Ndesamburo alikuwa mfanyabiashara huku akifanya mapinduzi katika siasa

tmp_19119-IMG_20170601_1217051390145147.jpg
tmp_19119-IMG_20170601_1214001233743763.jpg
 
Kufuatia msiba wa mmoja wa waasisi wa CHADEMA, Mzee Philemon Ndesamburo, Katibu Mkuu wa Chama, Dokta Vincent Mashinji ametangaza kuanza kwa maombolezo nchi nzima ikiwa ni pamoja na bendera za chama kupepea nusu mlingoti kama ishara ya kuenzi na kuthamini mchango wa mwasisi huyo katika harakati za kuanzisha, kujenga Chadema na mageuzi nchini.

Dokta Mashinji amesema maombolezo hayo yanaanza mara moja na kwamba chama kinatoa fursa kwa wanachama wake, wapenzi na wote walioguswa na msiba huo kufika Makao Makuu ya Chadema Kindondoni Jijini Dar es salaam kutoa salaam zao za pole na kusaini kitabu cha maombolezo.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo, Katibu Mkuu Dokta. Mashinji amesema “kutokana na msiba huu mzito wa Mzee wetu ambao tumeupokea kwa mshtuko mkubwa katika kuonesha kuguswa sio tu kwa Chadema bali wote wanaopenda mabadiliko nchini, bendera zetu zitapepea nusu mlingoti hadi safari ya kumpumzisha katika makazi yake ya milele itakapokuwa imekamilika.”

Akimzungumzia Mzee Ndesamburo, Katibu Mkuu Dokta Mashinji amemtaja kama mmoja wa waasisi na kiongozi wa kisiasa aliyesimamia kwa vitendo sera za Chama chake za kutaka maendeleo ya kijamii na kubakia kuwa mfano wakati wote wa uhai wake kwa kuweka mbele msukumo wa umoja wa kitaifa.

“Alishiriki kuhakikisha nchi yetu inaongozwa kidemokrasia. Mwaka 1995 kuelekea uchaguzi mkuu alikuwa mmoja wa waanzilishi wa UDETA (Umoja wa Demokrasia Tanzania), baadae alikuwa sehemu ya kuanzisha UKAWA, mwaka jana amekuwa sehemu ya kuanzisha UKUTA. Haya yote unayaona ni maisha ya kuhakikisha umoja katika taifa letu,”ameongeza Dokta Mashinji.

Katibu Mkuu Dokta Mashinji amesema kuwa taarifa zaidi kuhusu msiba huo, hasa ratiba ya mazishi, zitaendelea kutolewa kwa kushirikiana na kushauriana na familia.

Akimzungumzia Mzee Ndesamburo namna atakavyokumbukwa hasa na vijana na viongozi wa kisiasa wa wakati huu, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Zanzibar, Salum Mwalim amesema kuwa Mzee Ndesamburo atabakia kuwa kielelezo cha dhamira ya dhati ya mpigania mageuzi aliyejitoa kwa hali, mali na nafsi yake yote.

“Dhamira yake ilikuwa ya kweli na ya dhati kabisa, alishiriki kuanzisha Chama, akapigania na kuwa mshirika wa hatua zote za mafanikio ya chama na mageuzi nchini. Hakukata tamaa wala hakukinai mafanikio ambayo yamekuwa yakipatikana kwani kwake jambo kubwa lilikuwa ni kuona Chadema inashika dola na inawapatia Watanzania mabadiliko ya kweli,” amesema Mwalim.

Mwalim aliongeza, “alikuwa na kila sababu ya kukaa pembeni au kuwa tu mchangiaji lakini aliweza kuunganisha nguvu zake za kiuchumi na dhamira yake ya mageuzi iliyolenga kuleta mabadiliko katika maisha ya watu na imekuwa hivyo hadi mauti yalipomkuta akiwa katika hatua za kusaidia wafiwa wa shule ya Lucky Vincent huku akiwa Mwenyekiti wa Chama Mkoa.”

Kwa upande wake mmoja wa waasisi wa chama, Mzee Victor Kimesera, ambae amekuwa na Mzee Ndesamburo tangu wakati wa kukianzisha Chadema, amemwelezea Mzee Ndesamburo kama mtu aliyechangia mawazo na fedha kukifikisha Chadema kilipo hivi sasa.

Mzee Kimesera amesema haikuwa rahisi kwa wakati huo kwa mfanyabishara wa ngazi ya Mzee Ndesamburo kujiweka wazi kudai mabadiliko huku akitoa mali zake, lakini yeye alifanya kwa kuwa aliamini katika kuwapatia Watanzania mabadiliko kupitia mfumo wa vyama vingi huku akijua kufanya hivyo kungeweza kuhatarisha biashara zake.

*Imetolewa leo Alhamis, Juni 1, 2017 na;*

*Tumaini Makene*

*Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano*
*CHADEMA*
 
Back
Top Bottom