CHADEMA wataka 'Babu wa Loliondo' ashitakiwe

babumapunda

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
4,644
Reaction score
3,328
May 09, 2013 | HabariLeo

KAMBI rasmi ya upinzani imeibua upya hoja ya tiba ya asili maarufu kama Kikombe cha Babu wa Loliondo, ikihoji kwamba Serikali haijatoa kauli wala kuchukua hatua dhidi ya Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapile aliyekuwa akitoa tiba hiyo.

Msemaji Mkuu wa kambi hiyo, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Antony Mbassa alihoji jana bungeni katika hotuba yake kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2013/14.

Alisema kwa mujibu wa aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda, watu 116 walifariki dunia kutokana na sababu mbalimbali wakiwa kijiji cha Samunge, ilikokuwa ikitolewa tiba hiyo na mchungaji Mwaisapile.

"Mpaka leo Serikali haijasema chochote kuhusu uchunguzi wa dawa ya babu. Mpaka leo Serikali haijatoa kauli yoyote wala kuchukua hatua yoyote dhidi ya Mzee Mwaisapile ambaye Februari hii alitoa kauli nyingine juu ya ugunduzi wa dawa nyingine," alisema Mbassa.

Kwa mujibu wa Mbassa, timu ya uchunguzi iliyoundwa mpaka Machi 2011 ilikuwa imeandaa kukamilisha taratibu , ili kufuatilia maendeleo ya kiafya ya wagonjwa 200 ambao wamekubali kwa ridhaa yao kushiriki katika utafiti huo kuona maendeleo yao kiafya baada ya kunywa dawa hiyo.

Wakati huo huo, kambi hiyo ya upinzani imeishauri Serikali kutoa taarifa rasmi kwa wananchi juu ya dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs) makopo 4,000, ambazo hazijakusanywa ili kuwaondolea mashaka na kuwajengea imani watumiaji.

Kambi hiyo imesema sakata la kuwepo ARVs bandia lililochukua miezi minane sasa, limekuwa na sura tofauti hususan juu ya nani anahusika moja kwa moja baada ya kiwanda cha Tanzania Pharmaceticals Industry (TPI), kukanusha kuhusika wakati Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Bohari Kuu (MSD ) wakisisitiza zimetoka kiwandani hapo.

"Wakati taratibu za kitaalamu na kisheria zikiendelea tunaishauri Serikali kutoa taarifa rasmi kwa wananchi juu ya dawa ambazo hazijakusanywa. Je, ziko vituoni au zilishatumiwa na wananchi? Kama zilishatumiwa, je, serikali ina taarifa zozote juu ya waliozitumia dawa hizo? Je, kuna madhara yoyote waliyoyapata kutokana na kuzitumia," alisema.

Kulingana na taarifa ya kambi ya upinzani, jalada la kesi ya ARVs bandia limepokewa na linashughulikiwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili kupata mwelekeo wa nani ahusishwe na kwa kosa gani kabla ya kuachia mamlaka husika jukumu la uchunguzi wa kina.

Taarifa hiyo ya kambi inasema ofisi ya DPP ilitoa maelezo kwamba suala hilo limechukua muda mrefu wa zaidi ya miezi miwili tofauti na muda wa kawaida wa siku 14 unaotumiwa na ofisi hiyo kushughulikia kesi mbalimbali zinazofikishwa kutokana na uzito na unyeti wa suala hilo.
 
Yule mzee ni mwelevu mno alishasema kuwa mwenye imani tu ndio dawa itamponya sasa hata wakimshitaki mbona jibu lipo wazi kuwa wote ambao hawakupona hawakuwa na imani?
 
PakaJimmy,

Pole sana naona Chadema wanataka kumuonea mzee wetu.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu kwa kweli hata mimi huyu mzee namkubali kwa kuwa Genius,yani hapo alimaliza kila kitu.Maana yake kama mtu hakupona,imani yake ni haba.Mzee wa watu sasa hivi maisha safi
 
Ha! Ha! Ha! Ha! Babu mbona utawataja waliokutuma kuleta Uzushi ! Binafsi , namtilia Mashaka Steven Wasira kuhusika kwenye mchongo huu .
 
kuna kusoma habari na kuelewa na kuna kupitia habari na kutokuelewa na kujifanya kuwa umeielewa DR MBASA HAJASEMA MZEE MWAISAPILE AKAMATWE ILA ALIKUA ANAULIZIA UCHUNGUZI ULIOFANYWA NA SERIKALI KUHUSU DAWA YAKE.

RIP CCM.
 
Babu aliwatibu viongozi wengi mpaka magogoni walienda usiku ili kuua soo, itakuwa vigumu kuwajibishwa wakati 25% viongozi walishiriki
 
Kamata madabida fungulia kesi, babu ni mganga tu ni hiyari ya mtu kwenda...........cha kulaumu serikali iliratibu safari za loliondo,Pinda,Kikwete,magufuli na wenzao wamekunywa kikombe dhumuni lilikuwa ni kuwasahaulisha wananchi na ishu za dowans nk
 
May 09, 2013 | HabariLeo

KAMBI rasmi ya upinzani imeibua upya hoja ya tiba ya asili maarufu kama Kikombe cha Babu wa Loliondo, ikihoji kwamba Serikali haijatoa kauli wala kuchukua hatua dhidi ya Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapile aliyekuwa akitoa tiba hiyo.

Msemaji Mkuu wa kambi hiyo, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Antony Mbassa alihoji jana bungeni katika hotuba yake kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2013/14.

Alisema kwa mujibu wa aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda, watu 116 walifariki dunia kutokana na sababu mbalimbali wakiwa kijiji cha Samunge, ilikokuwa ikitolewa tiba hiyo na mchungaji Mwaisapile.

"Mpaka leo Serikali haijasema chochote kuhusu uchunguzi wa dawa ya babu. Mpaka leo Serikali haijatoa kauli yoyote wala kuchukua hatua yoyote dhidi ya Mzee Mwaisapile ambaye Februari hii alitoa kauli nyingine juu ya ugunduzi wa dawa nyingine," alisema Mbassa.

Kwa mujibu wa Mbassa, timu ya uchunguzi iliyoundwa mpaka Machi 2011 ilikuwa imeandaa kukamilisha taratibu , ili kufuatilia maendeleo ya kiafya ya wagonjwa 200 ambao wamekubali kwa ridhaa yao kushiriki katika utafiti huo kuona maendeleo yao kiafya baada ya kunywa dawa hiyo.

Wakati huo huo, kambi hiyo ya upinzani imeishauri Serikali kutoa taarifa rasmi kwa wananchi juu ya dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs) makopo 4,000, ambazo hazijakusanywa ili kuwaondolea mashaka na kuwajengea imani watumiaji.

Kambi hiyo imesema sakata la kuwepo ARVs bandia lililochukua miezi minane sasa, limekuwa na sura tofauti hususan juu ya nani anahusika moja kwa moja baada ya kiwanda cha Tanzania Pharmaceticals Industry (TPI), kukanusha kuhusika wakati Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Bohari Kuu (MSD ) wakisisitiza zimetoka kiwandani hapo.

"Wakati taratibu za kitaalamu na kisheria zikiendelea tunaishauri Serikali kutoa taarifa rasmi kwa wananchi juu ya dawa ambazo hazijakusanywa. Je, ziko vituoni au zilishatumiwa na wananchi? Kama zilishatumiwa, je, serikali ina taarifa zozote juu ya waliozitumia dawa hizo? Je, kuna madhara yoyote waliyoyapata kutokana na kuzitumia," alisema.

Kulingana na taarifa ya kambi ya upinzani, jalada la kesi ya ARVs bandia limepokewa na linashughulikiwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili kupata mwelekeo wa nani ahusishwe na kwa kosa gani kabla ya kuachia mamlaka husika jukumu la uchunguzi wa kina.

Taarifa hiyo ya kambi inasema ofisi ya DPP ilitoa maelezo kwamba suala hilo limechukua muda mrefu wa zaidi ya miezi miwili tofauti na muda wa kawaida wa siku 14 unaotumiwa na ofisi hiyo kushughulikia kesi mbalimbali zinazofikishwa kutokana na uzito na unyeti wa suala hilo.

Kile Kikombe kilikuwa ni kipimo Cha Mambo yafuatayo:
1. Kimepima idadi ya Waathirika wa Ukimwi nchini
2.Kimepima vigogo wa serikali wanaosumbuliwa na magojwa sugu ukiwemo ukimwi
3.Kimepima idadi ya viongozi wa serikali wanao amini Uchawi
4.Kimepima Wachungaji feki wanao amini uchawi na kumwacha Mungu aliyehai
NB Utawala wetu unakumbatia ushirikina na ndio maana kuna udini!!!
Watawala wanasema serikali haina dini huku wao wanakumbatia ushirikina na majini
Watawala wanaungana na wachungaji wote waliunga mkono Kikombe Cha Shetani na Kuwapinga waliohubili kweli
 
Back
Top Bottom