Chadema Wasitumiwe na Wafadhili wa nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema Wasitumiwe na Wafadhili wa nje

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Jan 15, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Miaka ya sitini Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "Let the people make their own decisions, including their own mistakes". Sijachambua kama kweli alitekeleza maneno yake mwenyewe katika utawala wake.

  Mwaka jana Paul Kagame wa Rwanda alisema, "While more than US$ 300 billion in aid has apparently been disbursed to our continent since 1970, there is little to show for it in terms of economic growth and human development". What is the case for Tanzania, is aid working?

  Frantz Fanon, miaka ya sitini aliwahi kusema katika kitabu chake Wretched of the Earth kwamba viongozi wanaopigania uhuru Africa (wakati huo) hawana malengo sawa na ya umma. Kwamba umma unataka mabadiliko na maendeleo wakati viongozi wao wanataka waingie madarakani ili wapate fursa ya kula kama wazungu, kuendesha magari ya kizungu,kuongea kizungu, kulala nyumba za kizungu na ikiwezekana kulala na wanawake (wanaume) wa kizungu.

  Mwaka 2008 Kardinali Pengo aliwahi kuhoji kama makamanda wanaopiga vita ufisadi wanafanya hivyo kwa sababu wanachukia ufisadi au kwa sababu wanawachukia mafisadi.

  Najua sasa hivi unajiuliza mbona huyu gurudumu anakwenda zigzag?

  Tumefikia kiwango hiki cha umasikini, kiasi kikubwa, kwa sababu ya kutegemea wafadhili. Wanatuambia nini tufanye, lini tusifanye na tufanye vipi. Hufanya hivi kwa kuweka mifumo ya kufanya maamuzi ambayo sisi huikubali na kutekeleza.

  Kuna dude linaitwa MKUKUTA na linguine JAST. Wengi wenu hapa janvini mnajua zaidi kuliko mimi. Lakini kuna kamati ambazo hukutana karibu kila mwezi kuratibu shuhuli katika kila wizara. Zaidi ya nusu ya wajumbe wa mikutano hii huwa ni wazungu, wako makini na kila kinachoandikwa (huandika wao) na kupitishwa. Hufadhili safari za nje, semina na magari ya kifahari kwa maafisa wetu wa serikali kama incentive ya kuwatawala.

  Kikwete alitangaza kwenye kampeni zake za uchaguzi kwamba serikali yetu inapendwa na wafadhili kwa sababu ya sera nzuri, amani na utulivu. Wiki iliyopita aliwaita mabalozi akawaomba radhi kutokana na mauaji ya raia Arusha. Wananchi?

  Kisha nikaona jinsi wananchi walivyojitolea katika tukio la kuwazika mashujaa wetu wapigania uhuru waliouawa na polisi kule arusha. Kwa hali na mali, kwa moyo wote kabisa. Nikaamini kwamba kumbe inawezekana kupanga mambo yetu wenyewe, kuyagaramia na kuyatekeleza.

  Kwa hiyo nikaamini kwamba viongozi wa chadema wasipotiwa najisi na wafadhili, watatekeleza matakwa ya umma, siyo ya wafadhili. Kwamba tutapata maendeleo ya kweli badala ya maendeleo ya takwimu kwenye makaratasi.

  Hivyo, Chadema please, changisheni wananchi badala ya kutembeza bakuli kwa wafadhili. Hata wafadhili wakiwabemb eleza vipi, please kataeni. Kwani ukimuona ngiri anakukimbilia meno nje usidhani anakuchekea, ndivyo meno yake yalivyo, kwamba anafuata huo mguu wako! Mguu wetu ni rasilimali zetu.
   
 2. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mada yako ni nzuri,you are right,na mimi nasema nchi hujengwa na wenye nchi,hali ya kutegemea misaada ndio imetufikisha hapa,na kufikia maskini wa kutupwa,,,nawapongeza chadema maana mara zote wamekuwa wakijiendesha kwa michango ya watanzania maskini,bila kutegeme wafadhili wa nje,,na naamini hivyo maana kama wangekuwa wanapata ela za nje ni wazi kuwa baada ya kuchakachuliwa kwa slaa kwenye uchaguzi wa urais wafadhili wangepiga kelele kama wanavyofanya kule ivorcost,,,strugle continues
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono thread! Tufanye kama mbayuwayu?
   
 4. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Naomba kwa heshima na taadhima nikwambie kuwa kwa sisi wazamani thread yako ina message moja muhimu. KUJITEGEMEA. Vilaza waliomfuata Nyererei.e Mwinyi, Mkapa, Kikwete waliingia kutekeleza hoja ya "Frantz Fanon" tena kwa msaada wa wafadhili.


  Mwinyi = RUKSA kufanya chochote bila misingi ya dira ya kujitegemea


  Mkapa = UBINAFSISHAJI mali za umma kwa "wawekezaji hata feki" = ongezeko la umasikini kwa watanzania wa kawaida = takwimu za kimataifa (wafadhili) uchumi umekuwa (NBC, TCC, TBL kampuni zenye faida kuhamishiwa mikononi mwa ... zingine Kiwira, Tazara, TRC zijifie kifo cha mende haziwahusu wakubwa) waliofaidika Patels, Manjis, Azams, RA, Anna Mkapa and family etc


  Kikwete = MAFISADI IPTL,epa, Richmond, Dowans, Uchakachuaji uongozi usio pamoja, udini, woga neno kujitegemea halipo kwenye msamiati wao.


  Maeneo ya kujitegemea Kilimo (hatuwezi kujilisha, 1972 tulikuwa tunajilisha) Elimu (wanaopata elimu bora ???), afya haipatikani kwa kila mtu maradhi ya kawaida kama malaria yanatamba, Kipato cha mkulima na mfanyakazi ???.

  Kutembeza bakuli (Kama mwisho wa upeo wa kufikiri) kwa wafadhili lazima una udhaifu uliokithiri. Kwa upande mwingine wananchi wanahitaji kuongozwa kutumia rasilimali za kitaifa ili wajitegemee (kinachofanyika hakuna uongozi kuna utawala wenye maslahi yao binafsi)

  "Chadema please, changisheni wananchi badala ya kutembeza bakuli kwa wafadhili" Hawahitaji kuchangishwa wanahitaji kuonyeshwa njia watachangishana na kujishirikisha wenyewe(Mazishi Arusha).

  KUJITEGEMEA = KILA KITU PAMOJA NA THAMANI YA UTU, HESHIMA NA NEEMA
   
 5. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena vema,nakubaliana nawe....watz tuko tayari kuchangia harakati zote zinazolenga kustawisha taifa letu!
   
 6. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160


  Nakubaliana na wewe sana,ni muhimu kwa watanzania kuamua wenyewe wakiwa na uelewa wa kutosha kile wanachokitaka.Kuhusu wafadhili,kuna aina nyingi za ufadhili,nafikiri kinachopaswa kuangaliwa na CHADEMA ni kwamba hiyo misaada ina CONDITIONS za namna gani,je ni ambazo ziko kwa maslahi ya watanzania au kwa maslahi yao??japo kuwa tendency ni kuwa wanakuambia au kufanya suggestion za content za katiba,its not always the case.....Ninajua kuna wafadhili ambao ni wazur,i kazi ni kuchuja tu na kuwekana clear mwanzoni kuwa wasitegemee mapenzi yao yatimizwe kwa kile watakachokitoa bali mapenzi ya watanzania.Kuhusu kutembeza bakuli nafikiri ni idea nzuri na italeta hali ya wananchi kuona wao ndo wamiliki na wawezeshaji wa mchakato huu.....Asante kwa hoja nzuri.
   
 7. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Asanteni, lakini sasa hata hamgongi thanks jamani? mnajua inachukua muda kuanzisha ka thread kama haka eh?
   
 8. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nchi ina rasimali za kumwaga, kwa maana ya watu, ardhi na vilivyomo tunakosa maadili ya kitaifa, matokeo yake tunaweka viongozi amabao wanakuta hakuna cha kuwazuia (Maadili ya Uongozi) wanageuka kuwa mafisadi. Tunahitaji viongozi vichwa ngumu kama akina Hugo Chavez ili tujitegemee na kutegemea kidogo sana toka nje.
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hehe utagongewa tu labda wamesahau!Nwyz asante kwa mawazo mazuri...ni kweli kabisa mara nyingi mtu asiejitegemea hua anaburuzwa na anaemsaidia!Hopefully CDM hawatadondokea kwenye kundi hilo ili wabaki kua na mawazo endelevu yanayojitegemea!!Thanks inakuja soon!
   
 10. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mkuu nashukuru umemtaja kamanda wangu Chavez, napenda sana msimamo na utekelezaji wa misimamo yake. Lakini tunakwenda mbali, tunaye Kagame, ingawa ana mapungufu yake ya kudhibiti demokrasia lakini pia amedhibiti ufisadi. halafu kuna Botswana ambayo siri ya kuendelea kwake kwa kasi ni kuchmoa mirija yote ya misaada kutoka nje. hata JK alipoingia madarakani alituma maafisa wake Botswana kujifunza namna ya kuboresha mikataba ya madini. Sijui kama walitekeleza walichojifunza huko?
   
 11. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ungejua wafadhili wanavyojua kutongoza na kutumia makuwadi walafi walio ndani ya chama? watalinda na kupanua maslahi yao katika utawala wowote ule. Jiulize kwa nini karatasi za kura ziliamuliwa na Bunge zichapishwe hapa tz na serikali ilishanunua mitambo lakini dakika za mwisho zikachapishwa nje ya nchi. Ulikuwa ni uamuzi wa nani na kwa nini?. Unadhani maslahi yao yangekuwa hatarini wangekuwa bado wako kimya kuhusu mauaji ya arusha? asante kwa thanks!
   
 12. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  gURUDUMU

  you are very correct! dunia ya sasa hivi ni tya kuviziana. hata jana nilikuwa naangalia CNN jinsi wamarekani wanaluitolea macho dili la urusi kwa iran.........

  ni ni chaleenge namba moja kwa kila kiongozi na hasa wa nchi zetu. shida ni kwamba sisiemu ina viongozi vilaza wenye pentium 1 ambao ikiingia software mpya inafikiria mara mbili!!

  lakini tujiulize, unategemea nini kama majibu mazito ya kitaifa yanakuwa pprovided na kina Dar es salaam, Zomba, Kishongo et. al? wao badala ya kujiuliza kwanini wananchi wanaichukia CCM wanapewa lap top na modem za kuja kuchafua hali ya hewa hapa jamii forums? HAWA NDIO THINK TANKS WANAOONGOZA INCHI HII!!! NDIO HUMWAMBIA KIKWETE AWAAMBIE MABINTI ZETU KUWA MIMBA ZA UTOTONI NI KIHEREHERE CHAO!!!
   
 13. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  asante michelle, lakini, kwa nini watusaidie? wao wananufaika na nini kutusaidia? halafu kwa nini tusaidiwe? rasilimali zetu hazitoshi kupiga hatua kidogo kidogo kwa uaminifu na dira ya pamoja?
   
 14. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mkuu,unadhani kikwete na makamba wanajua kama kuna kitu kinaitwa JF?
   
 15. S

  Subira Senior Member

  #15
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mimi naogopa sana hapa kwetu, labda tuanzishe mfumo mpya kabisa wakuchagua maraisi wa kila chama ndo wote watawale kwa wakati mmoja wakae ikulu pamoja, na priviledge zote ziwe sawa ndo tutapata maendeleo kama kuondoa jembela mkono, shida za maji na umeme,
   
 16. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hi subira, unajaribu kusema kuwe na rais zaidi ya mmoja? kwamba kama wagombea wetu ni kumi basi wote waende ikulu? hebu nifafanulie hoja yako kidogo please
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wameshaonja tamu za Bilion za Sabodo watakataa vipi za wengine?

  Wewe umetokea wapi arawa? hakuna pesa haramu bwashe hata kama ni mauti shee!
   
 18. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sabodo si mtanzania? ndo mfano wa namna watanzania wanatakiwa kuchangia mabadiliko ya nchi yao. kwani sabodo anachangia ili aendelee kuinyonya nchi yetu?

  lakini mkuu pia sina uhakika kama nilisema pesa za wafadhili ni haramu, hebu nisaidie kidogo, pesa haramu ni nini?
   
 19. T

  Topical JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hujui pesa haramu? mfano wake ni kama za Sabodo au RA

  Anakuwa mfano wa kuigwa akichangia cdm (yuo guys are not serious)

  Yes pesa za kufadhiliwa ni haramu kwa nchi, kwa mtu pia...
   
 20. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mkuu, usinizungushe tafadhali, naomba uniambie fedha haramu ni nini? ili hatua ya pili ndo tuweze kutathmini kama hizo za sabodo ni haramu
   
Loading...