Chadema washington dc yapata uongozi mpya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


_DSC1129.JPG

Mwenyekiti mpya wa Chadema Washington Cosmas Wambura akipeana mikono ya pongezi na Katibu mpya Ndugu Isidori Lyamuya.



_DSC1127.JPG

Kutoka kushoto Katibu mpya Isidory Lyamuya, Mwenyekiti mpya Cosmas Wambura, Katibu aliyemaliza muda wake Liberatus Mwang'ombe na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kalley Pandukizi.

********************************************************************************
Tawi la Chadema Washington DC limepata Viongozi wapya walioshika nafasi za waliokwa Viongozi wa muda.


Katika Uchaguzi huo Cosmas Wambura amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda Kalley Pandukizi.



Nafasi ya Katibu imechukuliwa na Isidori Lyamuya aliyechukua nafasi ya Liberatus Mwang'ombe aliyekuwa Katibu. Nafasi ya Mweka hazina imechukuliwa na Ludigo Mhagama na nafasi ya katibu mwenezi imechukuliwa na Hussein Kauzella. Nafasi nyingine zilizogombewa ni Wenyevitina Makatibu wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.



Pia kulikuwa na nafasi ya Afisa Habari wa Chama. Akiongea baada ya Uchaguzi Mwenyekiti aliyechaguliwa ndugu Cosmas Wambura amesema atatoa ushirikiano mkubwa katika kuendeleza shughuli mbalimbaliza kukijenga Chama. Pia Katibu mya amesema watashirikiana na Mwenyekiti na wanachama wengine wote kuhakikisha Chama kinzidi kuwa Imara na kupata wanachama zaidi.





_DSC1154.JPG

Baadhi ya wanachama wa Chadema walioshiriki zoezi la Uchaguzi la kupata Viongozi wapya wa Chadema Washington DC.

_DSC1160.JPG

Mzee Emmanuel Muganda pamoja na Mkewe wakiwapa mawili matatu Uongozi mpya wa Chadema Washington DC. SOURCE: Swahili Villa Blog.







 
Safi sana ma kamanda kwa kufanya uchaguzi na kupata viongozi wapya, Bongo tunpambana na nyie huko endelezeni mapambano mpaka kieleweke, nje ndani tutashinda...MUNGU ibariki CHEDEMA Washington DC, Mungu ibariki TZ
 
Vizuri Chadema; Angalau Mmefanya Uchaguzi wa CCM DC walibebana na kuchaguana kumuona Rais kiupendeleo

Kama kawaida ya Chama Cha Matajiri
 
Back
Top Bottom