mkafrend
JF-Expert Member
- May 12, 2014
- 3,047
- 1,503
WanaJf, salaam!
Ni vigumu kuamini hili lakini pia ni aibu kwa chama kikubwa kama CHADEMA kuanza kusaka anwani na namba za simu za makada waliokuwa wanagombea ubunge ndani ya CCM na kwa bahati mbaya hawakuweza kuteuliwa. Nia ya viongozi hao kusaka mawasiliano yao ni kutaka kuanza kuwarubuni ili wahamie kwao.
Ninachowashauri ndugu zangu mliokuwa mnagombea kura za maoni kaeni njia kuu bila kubabaika kwa kuwa Mhe. John Pombe Magufuli asingeweza kumteua kila mmoja kushika uongozi wa nchi hii; naamini kuwa kazi bado zipo nyingi na MUNGU atawasimamisha kwa wakati aupendao. Lakini pia katika mazingira yenu endeleeni kukihubiri CCM ili kijijenge zaidi na kuongeza idadi ya wafuasi.
Lakini katika vita ya kusaka ubunge endeleeni kujiweka sawa kwa kuwa miaka haikawii kuisha - jiimarisheni na kushiriki na wananchi kwa mambo mbalimbali ya kijamii ili wananchi wawakumbuke. Changieni madawati, CHIF, na kutatua kero za wananchi kama bodaboda n.k
Nachowathibitishia ni kuwa hata Mhe. Dkt. John Magufuli alipoanza siasa mara ya kwanza Biharamulo alianguka na hakuteuliwa kushika nafasi yoyote nchini wala hakuhama chama.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!!!!!!!