CHADEMA wandamana kupinga mgawanyo wa mbolea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wandamana kupinga mgawanyo wa mbolea

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 24, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  CHADEMA wandamana kupinga mgawanyo wa mbolea


  Na Joseph Mwambije,Songea

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kimefanya maandamano ya amani kushinikiza Mkuu wa Wilaya ya Songea, Bw. Thomas Sabaya ajiuzulu
  kutokana na utaratibu mbaya wa ugawaji wa mbolea ya ruzuku na kusabababisha wananchi wa kata saba za wilaya hiyo kuikosa.

  Maandamano hayo yalianza kwenye ofisi ya Chama hicho Wilaya ya Songea katika Kata ya Mfaranyaki na kuzunguka maeneo ya Mjini na kuishia kwenye uwanja wa Malori katika kata ya Majengo.

  Katika maandamano hayo ambayo yalipambwa na polisi wengi vijana ambao walikuwa wakikimbia kimbia kuhakikisha hakuna vurugu, waandamanaji walitanguliwa na gari ambalo lilifungwa vipaza sauti vikitangaza kuwa Mkuu wa Wilaya anatakiwa ajiuzulu kwa ugawaji mbovu mbolea.

  Matangazo hayo, yalisema vigogo waliokamatwa na vocha za mbolea za ruzuku wameonewa na kwamba mwenye makosa ni Bw. Sabaya.

  Katika Uwanja wa Malori viongozi wa chama hicho walihutubia mkutano wa hadhara ambao ulihudhuliwa na umati mkubwa wa watu kutoka maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Songea.

  Akihutubia kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mjini, Bw. Joseph Fuime alisema Mkuu huyo wa wilaya amefanya hujuma na kuzinyima mbolea kata saba, tano kati ya hizo zikiwa zinaongozwa na madiwani wa CHADEMA.

  Bw. Fuime alisema hali inaonyesha kuwa Mkuu wa Wilaya ameshindwa kazi kwa kushindwa kusimamia mbolea ya ruzuku na anapaswa kujiuzulu.

  Kwa upande wake mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA, Wakili Edson Mbogoro akizungumzia sakata la Dowans alisema Serikali inafanya mchezo na maisha ya Watanzania kwa kuwabebesha mizigo isiyo wahusu kwa kupandisha gharama za umeme kufidia ulipaji wa Dowans.

  Alisema kuwa hali inaonesha kuwa CCM inafikia ukiongoni baada ya kutofautiana na vijana wao kuhusu kuilipa kampuni hiyo hewa ambayo ilirithi mkataba wa Richmond, na kwamba ndani ya Chama hicho kuna watu wenye uchungu kwa kuona Samuel Sita na Dkt. Harrison Mwakyembe wanaangamizwa.

  Wakati huo huo, mwandishi Wetu Cresensia Kapinga, Songea anaripoti kuwa watu wanne wametiwa mbaroni na polosi mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa vocha 459 za ruzuku za pembejeo za kilimo zenye thamani ya sh. 21,114,000.

  Waliokamatwa ni maofisa wawili waandamizi wa Idara ya Kilimo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, mhasibu msaidizi pamoja na wakala mmoja wa pembejeo za kilimo.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda alisema kuwa watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi, wanadaiwa kuwa walishirikiana na mawakala hao kuiba vocha hizo.

  Alieleza kuwa vocha zilizoibwa ni za mbolea ya kukuzia mahindi ambazo zilipaswa kusambazwa kwenye kata za halmashauri ya manispaa ya Songea lakini wakazi wengi wamezikosa, jambo ambalo lilisababisha kero kubwa kwa mkuu wa wilaya ya Songea, Bw. Thomas Ole Sabaya.

  Alifafanua zaidi kuwa vocha hizo hapo awali ilidaiwa kuwa zimepelekwa vijijini ambako wakazi wa Manispaa ya Songea wanakolima, lakini baada ya kufuatilia kwa makini imebainika kuwa hazikuwafikia wakulima hao.

  Bw. Kamuhanda alisema polisi inaendelea na uchunguzi wa kina katika maeneo mengine ya vijiji ambayo yanadaiwa kukumbwa na wizi huo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Maandamano ya mbolea yawe ni mwanzo tu wa kudai kung'olewa kwa serikali ya kifisadi ya JK.vinginevyo taifa linakoelekea ni kubaya mno.......................
   
 3. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Tuandamane kupinga mgawo wa umeme. inaonekana serikali imelala usingizi wa pono. mimi nitakuwa wa kwanza kushiriki. mgawo wa umeme haukubaliki.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kupanda ndege kwenda nje na kufanya shopping kutamu sana kwa wakuu! hayo ya mbolea ni madogo sana wacha yashughulikiwe na wakuu wa wilaya na watendaji wa vijiji, teh, tehe
   
Loading...