ccm mmepata msaidizi wenu zito, mbona mnaongea hovyo? shukruni kumpata lakini cdm haitatetereka. ukimzomea zito umezomea mafisadi wa ccm. shukuruni mna msaidizi!!CHADEMA WANAWEWESEKA
Baada ya ziara ya ACT Mbeya chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema chazidi kuweweseka huku ngome zao zikiwa zinavunjwa kwa siasa na hotuba safi za wana ACT.
Chadema wametengeneza kipande cha video kinachoonesha watu kuzomea, ila hakioneshi anazomewa nani ingawa wao wanadai ni Zitto.
Kwa mujibu wa Afande Sele ni kwamba hawakuwa na ratiba ya mkutano Tunduma hivyo yeye na Zzk hawakushuka ndani ya gari, kauli ambayo imethibitishwa na wana ACT wengine waliokuwa katika msafara huo.
Mwanahabari wetu aliamua kuwatafuta wakazi wa Tunduma mkoani mbeya na kuwahoji juu ya hili.
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Mahenge Regan anadai wao ndio waliosimamisha msafara na kuomba wapatiwe hata neno moja, ndipo mwenyekiti wa ACT na katibu mkuu waliposhuka na kuongea machache kisha wakaondoka. Alipoulizwa kuhusu zomea zomea anasema kuna vijana wachache wa Chadema wakiongozwa na kada maarufu wa Chadema anayejulikana sana kwa jina Mdude Chadema ndio waliokuja na kutaka kuharibu ila Msafara ulikua ushaanza kuondoka.
Ikumbukwe mkakati wa zomea zomea Mbeya uliratibiwa na Mbunge wa Mbeya mjini Mbilinyi akisirikiana na Mary Mwanjerwa wa viti maalumu Ccm.
Kiongozi wa chama ACT Zitto amedai kutokushuka Tunduma na video hizozinazosambazwa ni muendelezo wa siasa chafu za Chadema.
Ikumbukwe pia moja ya mtihani waliopewa watangaza nia na wabunge wa Chadema ni kuhakikisha Ziara za ACT hazifanikiwi ili wapitishwe na chama kuelekea Uchaguzi mkuu, hili limeelezwa na kada mmoja wa Chadema aliyeombwa kuhifadhiwa jina kwa usalama wake.
Wananchi wa mkoani Mbeya wamesikitishwa sana kuhusishwa na uhuni huu unaoratibiwa na mbunge wao na kuonesha kuchoshwa na tabia zake za kuwafanya vijana wao misukule huku yeye anatengeneza pesa.
Mwandishi Huru
Mbeya
SUGU ameshindwa kumuongoza mke, mpaka wanapelekana mahakamani ataweza kuongoza MBEYA MJINI?
Sugu hawezi uongozi hata wa yeye na rafiki yake wa kike hvyo kuzomea ni mahalhp pake.
aibu kubwa mtaipata mtwara kwa wana CUF.
Hapa kwa Mary Mwanjelwa sikubaliani na wewe.
Mary Mwanjelwa hafanyi hizo siasa chafu, huyu ndiye mbunge mteule wa Mbeya Mjini.
Mwanjerwa aliye kuwa analilia kupewa uwaziri?
Kwa hiyo ACT mnavunja ngome za Chadema kwa hotuba "safi" za kiongozi wenu mkuu na sio ngome za CCM? Kweli nyie mahayawani wakubwa na bado mnajiita chama cha upinzani.
Huo ni upinzani gani kwa wapinzani na sio watawala? Majitu makubwa na akili za kushikiwa ni shida sana.
mtoa mada anaweweseka sana kuliko hao aliowataja...
Mkuu sio lazima niwe Mbunge ili kuona udhaifu wa hawa wawakilishi wetu!
Unaweza kuthibitisha kuwa sugu hawezi uoongozi? Au kutibitisha tukio hilo limeratibiwa na yeye? Kipi sahihi za kutengenezwa au vijana walitumwa?
Wamejidanganya kwa kufuata huruma ya uislam mtwara na lindi,kumbe wamebugi sana watu sasa hivi wamesahau udini na sasa ni kitu kimoja wakristu na waislam.
Dkt Kilembwe
Naomba ufafanuzi ziara za mikoani amekuwa akienda sambamba na viongozi wale, ilipofika zamu ya Arusha na moshi kagawa makundi mawili moja lake na moja la mwenyekiti, la kwake linaenda kusini lkn la mama linakuja Arusha, Why?? Au baada ya zomeazomea alihisi na Arusha atazomewa?
Kwa hiyo ACT mnavunja ngome za Chadema kwa hotuba "safi" za kiongozi wenu mkuu na sio ngome za CCM? Kweli nyie mahayawani wakubwa na bado mnajiita chama cha upinzani.
Huo ni upinzani gani kwa wapinzani na sio watawala? Majitu makubwa na akili za kushikiwa ni shida sana.
zitto aache kuitaja chadema huenda akaepuka kadhia hiyo! cdm mpango wa mungu.