CHADEMA wanakimbia kivuli chao?!

CHADEMA wanakimbia kivuli chao?!

bhikola

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,133
Reaction score
1,668
Hello peopleee
Nimemis sana siasa za CHADEMA ya Dr Slaa. Kipindi kile kila mtu alikuwa kamanda. Wasaliti wakawa wanafukuzwa chama bila kujali kama uchaguzi utaharibu hela za walipa kodi. Nani hakuwa shocked chadema walipofukuza madiwani wanne kwa mpigo kule Arusha? wakaja wakafukuza madiwani 2 Mwanza. Mwisho wa siku wakafukuza mpaka Mbunge kwa tatizo la usaliti. na walikuwa tayari kabisa chaguzi zifanyike bila kujali kuwa pesa nyingi za walipa kodi zingetumia. Walisema hiyo ndiyo demkrasia.
Miaka kadhaa baadaye, ni wasaliti wale wale wameamua kukisaliti chama na "kuhamia" au "kununuliwa" call it anyhow!! hawa wasaliti hawajataka kusubiri kufukuzwa chama. Sasa jambo la ajabu, chadema wanakuja na huruma ya kutumika kwa pesa nyingi kwenye chaguzi za marudio. wanakuja na swaga za kukanyagwa kwa demokrasia wakati watu wametumia uhuru wao wa "kuhama/kununuliwa".
Swali, chagadema wanakimbia kivuli chao? kwa sasa wanawataka wasaliti wa chama wabaki?
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WA TAIFA WA CCM

PEOPLEEEEEEEEEEEESSSSSSS!! POWERRRRR
MABADIRIKOOOOOO - LOWASAAAAAA: LOWASA - MABADIRIKOOOOOO

jamani mimi nimeandika tu, siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa, lakini napenda na nafatilia siasa
 
Subiri mvua ya matusi sasa badala ya hoja

Nawakaribisha tu mkuu, hakunaga tusi jipya duniani. "Hata ambayo sijafanya nisha yasikia" by Mwana FA, wimbo: Dume suruali
 
Ukiwa kichwa panzi unategemea nini??
Lazima usahau kila kitu na kuanza kuhubiri ya jana.!!
 
Ukiwa kichwa panzi unategemea nini??
Lazima usahau kila kitu na kuanza kuhubiri ya jana.!!


kichwa cha panzi kina features gani mkuu
miye najua tatu muhimu: compound eyes, vipapasio 2. na mdomo wa kukatia na kuafunia
usisahau lakini kuwa panzi ni kati ya wanyama wenye mifupa ya nje (exoskeleton animal)
 
Ingawa hata ccm Wanaboronga ila chadema ya kipindi hiki ndo hata siielewi kabisa. Hawana hoja kabisa kazi kudandia dandia hoja na matusi. Sitapiga kula tena katika maisha yangu kwani nilikua nawaamini upinzani ila nimeumbuka.

Over!
 
Ndo maana wanapata shida kwasababu wanaangalia walipo tu, mambo ya waliko toka na waendako hayawahusu
 
HAKUWA Wa kuwatukana mnajitukana wenyewe nani kuzuia Siasa, mikutano ? Ni CUF?
 
Hivi chadema ndo nini, mnikumbushe jamani huku kusahausahau nahisi nimesahau, kama nakumbuka marehemu alikuwa maarufu sana, aliugua tokea 2015 na akagoma kunywa dawa sasa nahisi alishakufa ila mazishi yanaandaliwa possibly atazikwa 2020. Mnisahihishe maka nimesahau tena.
 
Hivi chadema ndo nini, mnikumbushe jamani huku kusahausahau nahisi nimesahau, kama nakumbuka marehemu alikuwa maarufu sana, aliugua tokea 2015 na akagoma kunywa dawa sasa nahisi alishakufa ila mazishi yanaandaliwa possibly atazikwa 2020. Mnisahihishe maka nimesahau tena.

naomba mnisamehe kama nakosea maana mimi siyo mwanasiasa
hahahaha. hatare sanaaaa
 
Back
Top Bottom