masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,410
- 14,119
Mkuu kwani yule masikini mwandishi aliitwa pale na polisi?Mkuu, nimevutika na uchambuzi wako.
Kwa hiyo marehemu Mwangosi (mwandishi wa habari) ni chama kwa maana ya CDM?
Na alizungukwa na kupigwa hadi kuuawa na polisi wapatao wanane akiwa katika kazi za chama-CDM?
Hakika kazi bado mbichi.
Unaona Mkuu Mzee Tupatupa,
Haya ndio mawazo ya washauri wengi ndani ya CCM: kusema uongo kweupe bila hata aibu wala kupepesa macho!
Twiga wa katar,pembe za ndovu chadema haoNi kauli ya kuudhi na kukata tamaa. Hutamkwa sana na viongozi-tena wa juu wa chama changu cha CCM na 'washirika' wake pale linapotokea tukio lolote,hasa lisilovutia. Wakiuawa watu na polisi,CHADEMA wanahusika;wakizomewa Mawaziri na viongozi wa CCM,CHADEMA wanahusika;wakigoma wanafunzi wa vyuo vikuu,CHADEMA wanahusika;wakiandamana waislam,CHADEMA wanahusika(?).Kila baya CHADEMA.Hizi ni siasa za kipuuzi. Hazitachelewa kuchosha. Sasa,kwahiyo CHADEMA inakubalika kuliko wengine hadi kukubaliwa mipango yao nchi nzima? Eti,CHADEMA huwanywesha watu viroba ili wazomee?! Hakuna cha viroba,magunia wala pakacha....watanzania wanabadilika. Hawasomeshwi vya kutosha shuleni lakini maisha ni shule kuu zaidi. Wanahitimu kila siku. Kama ni kweli CHADEMA inakishinda chama changu kiushawishi mashuleni,vyuoni,vijijini,masokoni,mijini na kwingineko,mbona uchaguzini hakitangazwi mshindi mara kwa mara? Kinana na wengine,kuanzia leo hatutaki kusikia kauli hii.Ikome na mpambane tumwone mshindi wa haki
Kila tukio lina specific circumstances zinazozunguka matukio hayo.
Lile la Mwangosi imebainika CHADEMA walitaka kupimana ubavu na polisi, yaliyotokea yametokea.
Mmmeambiwa kila kona kuwa at least wangetumia busara(wote CHADEMA na Polisi) kifo kile kisingetokea.
Kwa hiyo lawama zimeenda 50% polisi, na 50% CHADEMA/M4C.
Huwezi jivua lawama kama malaika, ukubali kukosolewa kama mnavyo wakosoa wengine.
Twiga wa katar,pembe za ndovu chadema hao
Hayo ndiyo mawazo yaliyokaa kichadema-chadema, kupambana na polisi badala ya sera za kuwatumikia watanzania.ndiyo mkuu ndiyo maana hata mahakamani amepelekwa polisi 1 kwa kosa la mauaji na chadema kapelekwa 1.kwa hiyo ngoma droo.
Mkuu na wewe nisaidie swali hili.
Tunaposema EL, RA na Chenge na wengine walipelekwa mahakama ipi.
Lakini ukweli unsbaki pale pale kuwa ni mafisadi.
Na nyie kubalini kukosolewa au kujikosoa.
hata kukamatwa kwa lile kontena la pembe za ndovu huko Hong Kong Chadema inahusika.
Hatari:
Weka Mbali na Tembo.
CCM hawana jipya,wao wamegeuza CHADEMA ndio kituo chao cha polisi,maovu wanatenda wao wanakimbilia kuisakama chadema.
CHADEMA haipo kiivyo,CHadema for tanzanians relief
Ni kauli ya kuudhi na kukata tamaa. Hutamkwa sana na viongozi-tena wa juu wa chama changu cha CCM na 'washirika' wake pale linapotokea tukio lolote,hasa lisilovutia. Wakiuawa watu na polisi,CHADEMA wanahusika;wakizomewa Mawaziri na viongozi wa CCM,CHADEMA wanahusika;wakigoma wanafunzi wa vyuo vikuu,CHADEMA wanahusika;wakiandamana waislam,CHADEMA wanahusika(?).Kila baya CHADEMA.
Hizi ni siasa za kipuuzi. Hazitachelewa kuchosha. Sasa,kwahiyo CHADEMA inakubalika kuliko wengine hadi kukubaliwa mipango yao nchi nzima? Eti,CHADEMA huwanywesha watu viroba ili wazomee?! Hakuna cha viroba,magunia wala pakacha....watanzania wanabadilika. Hawasomeshwi vya kutosha shuleni lakini maisha ni shule kuu zaidi. Wanahitimu kila siku.
Kama ni kweli CHADEMA inakishinda chama changu kiushawishi mashuleni,vyuoni,vijijini,masokoni,mijini na kwingineko,mbona uchaguzini hakitangazwi mshindi mara kwa mara? Kinana na wengine,kuanzia leo hatutaki kusikia kauli hii.Ikome na mpambane tumwone mshindi wa haki