Chadema wamkataa Chenge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wamkataa Chenge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 6, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=2][/h]


  Na Mashaka Mgeta  6th June 2012  [​IMG]
  John Mnyika


  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, hana mamlaka ya kimaadili kuingoza Kamatiya Bunge ya Fedha na Uchumi.

  “Chadema tumeshangazwa kwa kuchaguliwa kwa aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi,” alisema Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika.

  Mnyika aliyekuwa anazungumza kwenye mikutano ya hadhara katika vijiji mbalimbali vya Kata za Lumesule na Napacho, wilayani Nanyumbu juzi na alisema kwa vile Chenge ni miongoni mwa watu wanaotajwa katika tuhuma nzito za ufisadi, anakosa mamlaka ya kimaadili kushika wadhifa nyeti kwa taifa kama huo.

  Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, alidai kuwa kuchaguliwa kwa Chenge kuiongoza kamati hiyo kuna athari kubwa kwa taifa kutokana na kuongeza idadi ya watuhumiwa wa ufisadi wanaozingoza Kamati za Bunge.

  “Walianza kukiteka chama chao cha CCM, ambacho kimeshindwa kuwachukulia hatua, badala yake kinapiga kelele za kupinga ufisadi barabarani, huku watuhumiwa wakiendelea kutamba kwa kushika nafasi mbalimbali serikalini na bungeni, sasa wanaingia bungeni,” alisema.

  “Jamani Watanzania wenzangu, wananchi wa Lumesule mnajua kuwa CCM kimeshatekwa na mafisadi, kwanza tulipotangaza orodha ya mafisadi na ufisadi wao pale Mwembeyanga walikataa kuwa ndani ya chama chao hakuna mafisadi. Baadaye wakakiri wao wenyewe wakisema wanajivua magamba, yaani watuhumiwa wa ufisadi waondoke ama watawafukuza,” alisema.

  “Chenge yule mnayemfahamu kama mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi nchini, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi, moja ya kamati nyeti kabisa katika bunge letu,” alisema na kuongeza:

  “Sasa hii ni hatari, watuhumiwa wa ufisadi walianza kuiteka serikali ya CCM kwanza, kisha wakakiteka kabisa chama chao.”

  Mnyika alisema Kamati ya Fedha na Uchumi ni nyeti inayoisimamia serikali katika masuala muhimu ya uchumi, ikiwemo maandalizi ya bajeti ya nchi kabla haijafikishwa mbele ya Bunge zima, hivyo kuchaguliwa kwake kunatoa tafsiri ya kukabidhiwa mikoba ya kusimamia fedha za Watanzania kupitia kamati hiyo.

  Alisema Chenge ataongoza jukumu la kusimamia ‘chenji’ zinazotokana na kashfa ya ununuzi wa rada, ambayo yeye pia ni mtuhumiwa.

  NIPASHE jana lilimtafuta Chenge kuzungumzia tuhuma hizo hakutapikana kutokana na simu yake ya kiganjani kuzimwa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu hadi tunakwenda mitamboni.

  MBOWE ‘KUWAVAA’ MEMBE, GHASIA


  Wakati Mnyika akielekeza ‘mashambulizi’ ya chama hicho kwa Chenge, Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe, amejitwisha ‘zigo’ la kumbana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, kutokana na viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na madiwani, kutoitisha mikutano ili kuwasomea wananchi hesabu za mapato na matumizi ya fedha za umma.

  Alisema usomaji wa hesabu hizo unaopaswa kufanyika kila baada ya miezi mitatu ni kwa mujibu wa sheria za nchi.

  Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, alitoa kauli hiyo juzi katika mkutano wa hadhara wa Operesheni Okoa Kusini uliofanyika Makanga wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.

  Alisema pamoja na kuibana serikali kuhusu sakata la serikali kuwakopa korosho wakulima wa Mtwara, atahakikisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Ghasia wanatoa jawabu la kero zilizotolewa na wananchi wa maeneo tofauti mkoani humo.

  Mbowe alisema kero zilizowasilishwa kwake na wakazi wa Nanyumbu wilayani Masasi kuhusu kero wanazozipata wanapoingia Msumbiji ni matokeo ya sera mbovu za uhusiano wa kimataifa ambazo zinawafanya Watanzania kunyanyaswa tofauti na wageni wanapoingia nchini.

  Azma ya Mbowe ilitokana na kauli ya mkazi wa kata ya Makanga, Mkapura Omary, aliyedai kuwa kumekuwepo unyanyasaji unaofanywa na maofisa wa Uhamiaji kwa Watanzania wanaoingia nchini humo, licha ya kufuata sheria na taratibu zilizopo.

  “Tunakuomba utusaidie kwa maana tunaonewa kila tunapovuka kwenda Msumbiji kupitia daraja la Umoja,” alidai na kutoa mfano kuwa aliwahi kunyang’anywa mali zake akiwa nchini Msumbiji, lakini hakupata msaada ambao ungemwwezesha kuzirejesha.

  Omary alidai kuwa ingawa alifanikiwa kurejea nchini baada ya sakata hilo, wenzake watatu aliokuwa nao na ambao hakuwataja kwa majina, wamekwama nchini humo wakiendelea kutaabika.

  Hata hivyo, akijibu hoja hiyo, Mbowe alisema vitendo hivyo na vingine vya aina hiyo ni matokeo ya nchi kuwa na sera mbovu zinazohusiana na masuala ya ushirikiano wa kimataifa, kiasi cha kuwakumbatia wageni na kushindwa kuzishughulikia kero za raia wanapokuwa nje ya nchi.

  “Nitakwenda bungeni na kumhoji Membe kuhusu suala hilo ili kuona namna sisi kama taifa tunavyopaswa kuchukua hatua,” alisema.

  Akizungumzia suala la viongozi wa vijiji, mitaa na madiwani kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi ya fedha za umma, Mbowe alisema atalielekeza suala hilo kwa Ghasia.

  “Nitataka Waziri wa Tamisemi atueleze ni hatua gani anachukua dhidi ya viongozi hao, ama nini anajua kuhusiana na viongozi kutofanya mikutano na kuwasomea wananchi mapato na matumizi ya vijiji na kata zao wakati ni haki ya msingi kwa mujibu wa sheria,” alisema.

  AMGOMEA OCD

  Katika hatua nyingine, Mbowe alijikuta akipinga hoja ya ofisa wa polisi aliyesemekana kuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nanyumbu, alipomtaka ashuke jukwaani kwa madai kuwa muda wa kuhutubia ulikuwa umepiga.

  Ofisa huyo alimtuma mmoja wa viongozi wa Chadema amfikishie ujumbe Mbowe, kwamba alitakiwa kukatisha hotuba yake na kushuka jukwaani, ndipo Mbowe aliposema na kuhoji:

  “Mimi ni Mbunge na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, OCD sikiliza usitutishe, tumetembea maelfu ya kilomita kwa ajili ya kuwaokoa Watanzania wakiwemo watoto wako…unakuja kuniambia funga mkutano?”
  Kwa mujibu wa Mbowe, muda wa kuhutubia mkutano huo ulikuwa bado unampa fursa ya kuzungumza na wananchi wa Nanyumba, jimbo lililowahi kuwakilishwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

  Hivyo, aliendelea kuhutubia na mwishowe kuuza kadi na kuorodhesha majina ya wanachama wapya, wakiwemo waliojitokeza kuyaongoza matawi ya Chadema kwa muda, kabla ya kufanyika uchaguzi baadaye mwaka huu.

  Chadema ilimaliza mikutano yake ya Operesheni Okoa Kusini iliyofanyika mkoani Mtwara jana na leo wanaanza mikutano kama hiyo kwenye vijiji, kata na wilaya za mkoa wa Lindi.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana katibu mkuu mtarajiwa CHADEMA-JJMnyika, Mungu akulinde na hao magamba ili yasikumalize kama shibuda.
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ukisoma habari za CDM huchoki kwasababu unaona kama maendeleo hayapo mbali sijawahi kufika USA lakini hotuba zao zinanifanya nikifunga macho 2015-2020 nione kama nipo USA
   
 4. FIDIVIN

  FIDIVIN Senior Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hahaha, too naive! kupenda kweli ni upofu.

  Ndg kuongea maneno mazuri ni rahisi saaaaaaaaana hasa kwenye siasa. Kutenda ni jambo lingine kabisaaaa.
  Tafakari!
   
 5. k

  kitero JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawatakia kila Lakheri kwa mkoa wa Lindi ambo ni moja ya mikoa isiyo elewa somo mapema na KIjiografia umekaa vibaya katika kufikia maeneo mengi.M4C DAIMA.
   
 6. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa ana minguvu kama EL....kusema ukweli wabunge wetu ni vipofu kama wamemchagua huyu kuwa mwenyekiti, kwasabab atakachofanya huko ni kusafisha na kulinda maslahi ya mafisadi tu...kwanza mtu mchafu hastahili kabisa kuwepo hapo, hata ubunge ni wa bariadi tu ndo wanampa kwasababu na wao ni wachafu kama yeye.
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mim nilijua 2012,,mbali kwa maneno ya jkk,,,,kigoma dubai,,,,,tanga jiji la viwanda,,,,barabara za kuruka,,,,,,acha bwana
   
 8. samstevie

  samstevie JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbowe walenge ''nchale'' chichiemu huko ''ntwala na lindi''
   
 9. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Hebu mwambie huyo mfuasi wa Chadema, eti wageuze Tz kuwa kama USA wakichukua nchi. Huyu jamaa Pangolin sijui aliandika huku anaota. All in all Chadema hata kama watachukua nchi hawatakua na tofauti na CCM.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 10. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  CCM haiachi kutuongezea chukin dhidi yao. Siku ya kufa nyani miti youe htuteleza. Kweli wanathubutu kumpa dhamana hiyo fisadi mkubwa kama C**nge. Jamani hawa Gambaz sijui kwa kweli. Huo wadhifa afadhali hata kumpa fisadi mdogo kidogo kama L****vi
   
 11. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Saa inakuja naam imekwisha fika Saa ya ukombozi kwa taifa
   
 12. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kumchagua Chenge si tu dharau kwa Watanzania bali pia dharau kwa CCM yenyewe.
  Sina haja ya kufafanua!
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mbona alivyoongea JK niliona kabisa kigoma haitakaa iwe dubai kwasababu alikuwa hasemi hela zitapatikanaje Lakini CDM wanatuelezea vyazo vya mapato kwanini nisi Imagine TANZANIA kama USA
   
 14. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu Barnabas Shadrack jaribu kubadilika hizo hela zote zinazoibwa zitashindwaje kuifanya TZ kuwa kama USA pambaf
   
 15. I

  IDIOS Member

  #15
  Jun 6, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa kweli ni maajabu makubwa kwa aerilali yetu na wbunge wake, hiki kitendo walichokifanya cha kumteua Andrew Chenge kushikanadasi ya uenyekiti wa kamati ya kudumu ya Fedha na Uchumi kweli tumekwish. Mungu okoa Tanzania yetu na tupe upeo wa kung'wmua madudu haya na piq utupe ujasiri wa kusema hapanakwa haya mambo. Tusibaki kulalamikia chinichini waungwana. Tupo pamojajamani?

  Wakati umefika ss wakusema hapana udhalimu huu uliotukuka.

  Hakikahaya madusu yanayotendeka kwa kutendwa na viongozi wetu yanatia kinyaa.

  So ni wajibu wetu kuyakataa kwa kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya.

  Nawasilishakaribu tuendelee kuyajadili.
   
 16. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Asante sana kwa kuonyesha umahiri wako wa kutukana, Mungu akubariki. Sasa hao chadema hata kama wanatoa mbinu za kupata mapato, je kwenye majimbo yao wamefanya mabadiliko gani? au hivyo vyanzo ni pale tu watakapopata Urais.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 17. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  But frankly speaking how can a person like Chenge be given a leadership of a such important parliamentary body? Hawa waliomchagua wako serious kweli? Chenge ni mchafu na hapashwi kushika wadhifa wowote na hata huo ubunge hapashwi kuwa nao. Pambaf!!!!!!!

  Tiba
   
 18. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kwani hao Chadema ndio wanakusanya kodi mkuu ? wala sio wao wameshika dola ?
   
 19. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu ni chenge yule Nape alizunguka na Mukama na Makamba Jr wakiwatangazia wananchi kwamba chama kimewapa siku tisini kujivua gamba? Siku tisini za sisim ni miaka mingapi vile? Ama ukistajabia ya Musa utaona ya Firauni.
  .
   
Loading...