CHADEMA Wamkanya Mwakyembe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Wamkanya Mwakyembe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Oct 14, 2009.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Oct 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  • Wafananisha malumbano yake na kundi la Ze Komedi!

  na Gordon Kalulunga, Kyela

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mbeya, kimemtaka Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe kuacha mara moja kulumbana na wale anaowaona ni kikwazo kwake badala yake akae na wananchi waliomchagua kupanga mipango ya maendeleo.
  Ushauri huo ulitolewa na viongozi wa chama hicho mkoani Mbeya katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Soko Jipya mjini hapa, baada ya kufungua tawi la chama hicho eneo la Ndandalo, Kata ya Mpakani.

  Wakizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Kyela, viongozi hao wa CHADEMA walioongozwa na mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa, Edo Makata, walisema inashangaza kuona
  jimbo hilo linajipatia umaarufu kutokana na viongozi wao kulumbana kwenye vyombo vya habari, huku wakisahau majukumu waliyokabidhiwa na wananchi waliowachagua.

  Makata alisema Jimbo la Kyela lina rasilimali nyingi ikiwa ni pamoja na Ziwa Nyasa ambalo lingeweza kuwanufaisha wananchi, lakini kutokana na viongozi waliopo kutojali maendeleo na mustakabali wa jimbo hilo, wamebakiwa na kazi ya kulumbana kwenye vyombo vya habari.

  “Viongozi mliowapa dhamana ili mshirikiane nao kwa ajili ya mustakabali wa Wilaya ya Kyela, wamebakiwa na kazi ya kulumbana kwenye vyombo vya habari badala ya kukaa nanyi kujadili maendeleo, hivyo mnapaswa kuwakataa wakija tena kuomba kura kwenu maana wanaoufanya ni utoto.

  “Tulikuwa tunawategemea kuwa tumewachagua kwa ajili ya kuzungumzia maendeleo ya Wilaya ya Kyela, lakini wamebaki kusingiziana utoto na huu ni msiba kwa wana Kyela, na hatupaswi kulishangilia hili, kwani watoto wetu hawana hata madawati na mipango ya maendeleo ya wilaya ikiendelea kuzorota,” alisema Makata.

  Sanjari na hayo, alisema
  Dk. Mwakyembe hapaswi kuendelea kuongoza jimbo hilo kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi zake na kuimba pambio za ufisadi huku akishindwa kuwataja kwa majina mafisadi hao, jambo ambalo linaonekana kuwa kama mchezo wa kuigiza wa kundi la Ze Orijino Komedi.

  Makata alisema CHADEMA haina ubaguzi wowote, lakini hali inayoonyeshwa na watu walioko ndani ya CCM kuwa wanapambana na ufisadi si kweli na kwamba kama kweli wao si washiriki wa ufisadi huo,
  wanapaswa kuwataja kwa majina kuliko kuendelea kulalamika kwenye majukwaa huku wakiwa wamesahau majukumu yao.

  Naye mwanachama wa CHADEMA aliyewahi kulitikisa Jimbo la Mbeya Vijijini, Sambwee Shitambala, ambaye pia ni wakili wa kujitegemea jijini Mbeya, alisema umefika wakati wa wananchi wa Kyela kukasirika kwa kuchezewa na viongozi wao ambao wameshindwa kujadili nao masuala ya maendeleo.

  “Mahitaji muhimu ya nchi ni pamoja na uongozi bora, lakini viongozi wenu wanashindwa kujadili nanyi maendeleo kwa sababu si viongozi bora, na Kyela imekuwa maarufu sana na viongozi wenu ni maarufu kuliko hata Rais Obama (Rais wa Marekani), lakini umaarufu wao ni mabishano na kusemana, si maendeleo,” alisema Shitambala.

  Aidha, alieleza kuwa kila kukicha viongozi waliowachagua wanawaza kujitafutia umaarufu wao binafsi badala ya kushirikiana na wananchi waliowachagua kujiletea maendeleo na badala yake wamekuwa mabingwa wa kusemana.

  “Viongozi wenu wamekuwa bize kusingiziana kwa kusema huyu anajipendekeza kwa mafisadi na wengine wanasema huyu anajipendekeza kwa CHADEMA, maana hoja ya kukemea ufisadi ni yetu CHADEMA, hivyo mnatakiwa kukasirika wananchi wa Kyela na kuwakataa wakati wa uchaguzi.

  “Wale mliowachagua hawasimamii maendeleo mliyowaambia kuwa mnayahitaji katika wilaya yenu ya Kyela, bali wamebaki kusimamia mambo yao, na ujumbe huu muufikishe kuwa waache kutangatanga huko Arusha, Singida na kwingineko, wanapaswa kuwa Kyela na kujadili masuala ya maendeleo ya Kyela,” aliongeza Shitambala.

  Huku akishangiliwa na wananchi waliokuwa wamehudhuria mkutano huo, Shitambala aliendelea kuwa, umefika wakati wa kuwakataa viongozi hao kwa sababu tayari wamewasaliti kwa kutotimiza ahadi zao na kubaki kujitafutia umaarufu wakati maendeleo jimboni kwao yakibaki kudidimia.

  “Mmekuwa mkihongwa mashati ya kijani na kofia kwenye chaguzi mbalimbali jambo ambalo linatia hasira sana, yaani mnaambiwa kuwa hamna uwezo wa kujinunulia nguo jambo ambalo linatia hasira sana, hivyo wananchi mnapaswa kuwachukia viongozi hawa na kuwakasirikia, na hili ni onyo la mwisho wasipojirekebisha wakataeni na hapa sichochei vurugu maana tumechoshwa kuona wananchi wa Kyela wakiendelea kuchezewa,” alisema Shitambala.

  Mkutano huo umefanyika wiki moja baada ya viongozi hao kuimarisha chama chao katika Wilaya ya Mbozi, eneo la mji mdogo wa Tunduma ambako walivuna wanachama wapya 175 na sasa viongozi hao wanatarajia kwenda kuhutubia katika mikoa ya Mara, Singida na kwingineko kwa ajili ya kuimarisha chama chao. Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kyela, Erick Sata, alisema chama chake kinazidi kuimarika kutokana na wananchi wengi kuchoshwa na ubabaishaji unaofanywa na viongozi waliopewa dhamana ya kuwaongoza.


  Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=9421
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Oct 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Siasa za Kyela, mmmh, tuwaachie wenyewe!
   
 3. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hivi chadema walikuwa na ubia na Mwakyembe?
   
 4. S

  Samwel JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2007
  Messages: 224
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndiyo,walikuwa na ubia naye,
  Hauoni jinsi anavyowasaidia kuwatangazia sera zao?
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sijakupata hapo!! Ubia gani tena huo?
   
 6. b

  bambumbile Senior Member

  #6
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Engineer alipowaambieni juu ya habari hii mkadai majungu, sasa wameandika Tanzania Daima labda ndio mtaamini.

  Mkuu Engineer, lete zingine za huku Konyumba!

  Vijana wa Ipinda nasikia wanamwambia mbunge kafulia?
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Oct 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ukiondoa umaarufu uliotokana na suala la Richmond, Jimboni kwake Mwakyembe kafanya nini specifically ukiacha mambo ya kawaida ambayo yamefanywa na Serikali kupitia Halmashauri, Ofisi ya DC na idara nyingine za Serikali ambazo hata asingekuwepo Mwakyembe yangefanyika tu?
   
 8. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2009
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  Hivi mbunge anaweza kufanya nini bila ya kupitia Halmashauri, Ofisi Ya DC na idara nyingine za serikali?Na ni nini kingefanyika bila ya mbunge?. Hivi kazi ya mbunge ni nini? ninafikiri kuwa unataka jibu la kuwa hakuna alichofanya. Quality ya swali inadetermine quality ya jibu.
   
 9. b

  bambumbile Senior Member

  #9
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukisoma hiyo habari ya CHADEMA utapata majibu yako yote juu ya kazi ya mbunge.

  Kikubwa kama mtu anajua hawezi kufanya lolote la kuwaongezea maendeleo wananchi wake, kwanini aje na ahadi nyingi?

  Baadhi ya ahadi za mheshimiwa:

  Tutajenga shule za secondary za ghorofa , tutajenga kiwanda cha chocolate Kyela (marafiki zangu wajerumani wako tayari kuja kusaidia), wananchi hawawezi kunywa maji yenye mkojo wa vyura, baada ya mwaka kila kijiji kitakuwa na maji ya bomba, haiwezekani Kyela isiwe na A-level, tutajenga hizo shule baada ya mwaka, tutajenga kiwanda cha ku pack mchele na kupeleka kuuza Ulaya (Ulaya yote mchele wanaokula ni wa Kyela), tutajenga kiwanda cha mafuta ya mawese, tutajenga kiwanda cha minofu ya samaki.

  Kuna ahadi nyingi, nikizikumbuka nitakuja kuandika, katika hizo zote utekelezaji sifuri.
   
 10. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2009
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  Hapa ulitegemea Chadema wanaweza kusema vizuri kuhusu mbuge wa CCM, HIVI tangu lini kulikuwa na ndoa kati ya Paka na Panya? Ebu jaribu kupata chanzo cha habari ambacho ni neutral. kwani injinia tumemzoea kuwa upande wa mgombea mmoja. mpaka wengine wakasema anategemea kupewa laptop. ninajaribu kutafuta chanzo neutral cha habari kutoka huko kyela. japo ukiulizia kyela mambo wanayokwambia si mengi kama yanavyolipotiwa humu. ukitazama jambo kwa mtazamo hasi basi utapata majibu hasi tu. sasa ukimtazama mwakyembe huku unataka fulani awe mbunge mbadala. basi utaona mabaya tu.
  ukweli suala la kuigawa kyela sio la muhimu sana. kwani kyela ilishagawanyika kabla, kumbuka kuwa kuna moroviani mbili ile yenye asili ya kyela na ile ya rungwe, kuna waojiita wazawa na wale wanaoitwa wakuja, pia kuna wale wa ngonga ambao wamewahi kuchagua TLP na wale wa kajunjumele ambao wao ni CCM tu. kuna watu wa mjini waliomchukia mwakipesile na wale wa vijijini wanaompenda mwakipesile. sasa mgawano uliopo ni wa wa mfumo mwingine lakini kyela siku zote imegawanyika. kusema mwakyembe kaigawa kyela si hoja nzito sana. watuletee mabaya yake na mazuri yake. na hao wanaotaka kugombea watuambie sifa zao. mara nyingi tumekuwa tukichagua viongozi wanaoenda kujifunza kuongoza badala ya kutuongoza.
   
 11. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2009
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  Hapa umeonyesha uhalisia wa ahadi, hizi ahadi kweli ni kubwa hata mimi nilipomsikiliza kwenye kampeni yake nilijuakuwa hapa ilitakiwa ahaidi kwa uangalifu maana watu wa kyela ninawafahamu kwa kutaka mambo yote kwa wakati mmoja tena kwa haraka. hapa utaona kuwa huyu jamaa anavision kubwa sana. na kufika huko anafikiri si kwa siku moja. suala la advance hilo hata mimi nimejalibu kufuatilia, nimeona hapo kyela day maandalizi yamekamilika japo sijui kufungua wanasubili nini? hili lipo njiani kukamilika. hayo mengine si ya leo wala kesho yanahitaji muda sana. yeye anaweza kuanzisha na wengine wakaja kumalizia. lakini sidhani kama atayaweza kwa sasa. japo ukweli ni kwamba hata anayetakakuja hawezi hayo kwa miaka mitano. hata ungekuwa wewe bambumbile huwezi hata kwa miaka kumi. ebu tujiulize tungekuwa sisi tungeweza? kama tusingeweza kikwazo ni nini? je hii inatosha kusema hatufai kuwa kiongozi?
   
 12. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Embu tuelezee ni jinsi gani Mwakyembe amewtangazia sera zao?
  Kwa tazamo wangu huyu jamaa amepata umaarufu kipitia chama dume CHADEMA...
   
 13. S

  Samwel JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2007
  Messages: 224
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu wangu kasyabone tall,
  Suala la mwakyembe kuwagawa wana ccm,halipingiki.

  Hivi hiyo NGO yako(Mango tree), wafadhili uliwatoa wapi.

  Historia inatueleza kuwa sehemu zote alizofanya kazi mwakyembe ,hakumaliza kutokana na tabia yake..

  Mhe. Msabaha alisema na ukitaka wasiliana naye.
   
 14. S

  Samwel JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2007
  Messages: 224
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini kidume CHADEMA wanawataja majina hao mafisidi,lakini yeye Mwakyembe anawa-komedy majina,Huo ndiyo utofauti wao.
   
 15. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2009
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  hawa ni wale wale kasoro majina. kuna siku umewahi msikia msabaha kaongea positive kwa mwakyembe. anyway achana na msabaha, wewe je unasemaje? hili ndilo muhimu.
   
 16. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  wapambe wa mwakalinga kwa udaku, huu ubunge mwaka huu wataua mtu ili waupate
   
 17. S

  Samwel JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2007
  Messages: 224
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haukusikia Hotuba yake wakati anajuzuru,Pole sana kaka.
   
 18. S

  Samwel JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2007
  Messages: 224
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .

  Wewe ndiye Umefulia na Upeo wako mdogo.
  Kama unaona Halmshauri za wilaya zinafanya kazi za mbunge,basi hakuna haja ya kuwa na mbunge.

  Mwakyembe anatakiwa kuwa mbunge wa Kawe kwani muda wote yuko Dar kwake kunduchi.
   
 19. b

  bambumbile Senior Member

  #19
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaelekea wengine mna enjoy kumtaja Mwakalinga, hii habari ina uhusiano gani na Mwakalinga? Au Mwakalinga katangaza kugombea CHADEMA? Au Tanzania Daima wanamuunga mkono Mwakalinga siku hizi?

  Ndio maana wanasiasa karibu wote hawataki kuja kwa majina yao hapa maana inaelekea kuna watu ambao kazi zao ni kuchafua wengine.

  Mwafrika si tumia tu lile jina lako lingine? Hii ya huku kujifanya rafiki ya Mwakalinga huku unatumia jina lingine kukashifu ni unafiki mkubwa.
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Oct 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wananchi wa Kyela wamuulize Mwakyembe kuhusu ahadi alizotoa, kwa nini alishindwa kuzikamilisha? Hiyo Richmond yenyewe imekuja by chance tu na vita dhidi ya ufisadi ambayo inapiganwa bila kuwataja mafisadi wenyewe imekuja by chance vile vile! Hata hivyo vita hiyo inaonekana kama kulikuwa na conflict of interest (mradi wa umeme wa upepo Singida) ambayo ndio ilisukuma "mpambanaji" huyu kuonekana kama vile anapambana kweli! Vile vile mambo ambayo anadai waliyaacha ili kutokuiumbua serikali yalitia shaka kubwa juu ya nia ya dhati ya "mpambanaji" huyu dhidi ya ufisadi! Mpaka sasa tumeachwa gizani kuhusu mambo hayo yanayoiumbua serikali! Ana tofauti gani na Dk Hoseah wa TAKUKURU ambaye walimlaumu kwamba alitoa taarifa isiyo ya kweli kuhusu Richmond?
   
Loading...