Chadema wamjia juu Pinda


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,977
Likes
5,351
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,977 5,351 280
Pinda4%2828%29.jpg

Waziri Mkuu, Mizengo PindaChama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemshutumu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa amekuwa akifanya ziara za kiserikali kufanya shughuli za Chama cha Mapinduzi (CCM) na kulaani kauli yake ya kuwataka wananchi wa Jimbo la Igunga wapuuze mambo ya bunge na kumchagua tena Mbunge wa jimbo hilo, Rostam Aziz.
Taarifa iliyotolewa na Chadema kwa vyombo vya habari jana, ilisema kuwa chama hicho kimeshangazwa na taarifa zilizojitokeza katika vyombo vya habari hivi karibuni kuhusu maneno na matendo ya Waziri Mkuu katika ziara zake maeneo mbalimbali nchini.
Iliongeza kusema kuwa kitendo cha Pinda kutumia ziara za kiserikali ambazo zinagharamiwa na fedha za umma wa Watanzania wote bila kujali itikadi na kutoa kauli za kisiasa za kibaguzi, kina mwelekeo wa kukiuka katiba na sheria za nchi.
Chadema pia kimelaani kauli ya Pinda anayodaiwa kuitoa akiwa kwenye ziara ya kiserikali mkoani Tabora kwa kuwataka wananchi wa Jimbo la Igunga wasimkatae Mbunge wao Rostam Aziz wakati wa uchaguzi mkuu ujao kwa kusikia maneno yanayosemwa bungeni.
"Tunamtaka Waziri Mkuu Pinda atoe kauli iwapo kwa maneno na matendo yake alipofanya ziara ya kiserikali Jimbo la Igunga Mkoani Tabora hakukiuka misingi ya utendaji wa kiserikali kama ilivyotamkwa katika katiba na sheria za nchi yetu".
"Chadema inatafsiri maneno na matendo hayo kama ni kufanya kampeni za kumnadi mbunge wa chama chake CCM kwa kutumia cheo chake cha Uwaziri Mkuu katika ziara ya kiserikali inayogharamiwa na kodi za wananchi wote bila kujali itikadi; huu ni ubaguzi na matumizi mabaya ya madaraka kwa mujibu wa katiba na sheria" alisema.
Chama hicho kimesema kimeshangazwa na kauli hiyo ya Waziri Mkuu yenye kulidharau bunge kuwa lipuuzwe kwa kuwa linayoyajadili hayana maana kwa wananchi hivyo wasiyazingatie yanayosemwa bungeni.
"Tunaitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kutoa ufafanuzi ama kuzikanusha ama sivyo Waziri Mkuu mwenyewe awajibike kutokana na kauli hizo zenye mwelekeo wa kukiuka katiba, sheria na misingi ya utawala bora wenye demokrasia ya vyama vingi. " iliongeza kusema taarifa hiyo.
Chama hicho pia kimesema kimeshtushwa na hatua ya Waziri Mkuu kuwataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala kujua salamu za Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa kwenye ziara na mkutano wa kiserikali.
Chadema pia kimesema kimeshangazwa na kitendo cha Waziri Mkuu Pinda kwenda mkoani Kilimanjaro na kuchangia shilingi milioni tano kwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Manispaa ya Moshi, ambazo ni mahususi kwa ajili ya kambi ya vijana hao kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba.CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Kinyambiss

Kinyambiss

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2007
Messages
1,372
Likes
6
Points
135
Kinyambiss

Kinyambiss

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2007
1,372 6 135
Huyu nae ana stimu zaki Chairman Mao chini chini.. yupo ki kada zaidi siom mtendaji huyu.
 
Chapakazi

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2009
Messages
2,880
Likes
15
Points
135
Chapakazi

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2009
2,880 15 135
si wafungue mashtaka!! Au kuna kifungu kinakataza WM kufunguliwa mashtaka?
 

Forum statistics

Threads 1,238,930
Members 476,277
Posts 29,337,199