CHADEMA wamejiandaa vipi kwa mabadiriko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wamejiandaa vipi kwa mabadiriko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Apr 25, 2012.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na wimbi kubwa la wanachama wa CCM kuhamia CHADEMA na kuna vigeregere vingi sana vimepigwa kuwapokea.
  Naamini kuna wengi watakuja (wanachama wa CCM au kutoka vyama vingine na wasio na chama), swali langu kwa viongozi wa Chadema ni je wamejiandaa vipi kuwa na wanachama zaidi ya walio nao?

  Mwaka 2010 nilishiriki kama wakala wa John Mnyika, siku moja kabla ya uchaguzi tulikusanywa Urafiki na kwa mtazamo wangu si John Mnyika wala Chadema waliokuwa wana miundo mbinu na matayarisho ya ku-cordinate mawakala wale. Bahati nzuri ni kwamba watu walikuwa wanajitolea kwa moyo bila kujali mapungufu yaliyokuwepo, kwa mfano ilikuwa tupangiwe vituo lakini hapakuwa na cordination inayoridhisha katika kuwagawanya mawakala wale kwenye vituo (siwezi kusemea vyama vingine kwa sababu sijawahi kushiriki kwenye mambo yao).

  Zaidi ya hilo nimekuwa nikitaka kujiunga Chadema tangu mwaka 2009 lakini mpaka leo sijapata fursa kwa sababu sijui ofisi ya chama ilipo maeneo ninayoishi, hata usajiri niliofanya kwenye tovuti ya chama sijawahi kupigiwa simu wala kutumiwa e-mail nikielekezwa na uongozi wa chama hatua inayofuata. Sitaki kuamini kuwa Chama hakina pesa za kuendesha shughuli zake kwani mimi binafsi niko tayari kuchangia uendeshaji wa chama, nimefanya hivyo kwa kiwango kikubwa kwenye kampeni za 2010 na mpaka leo sijajua chama kilikusanya kiasi gani kutokana na michango yangu na watu wengine waliokuwa wanataka Chadema ishinde.

  Leo ni 2012 na miaka mitatu ijayo tutakuwa na uchaguzi mkuu ambao CHADEMA kina nafasi kubwa ya kushinda (kama upepo utaendelea kama ulivyo sasa), naomba niwe mkweli napenda CHADEMA ishinde lakini pia naogopa kuwa chama hakijajiandaa vya kutosha kuendesha serikali kwani kwa jinsi mambo yalivyo sasa ni rahisi mno kikajikuta kikiingizwa mkenge na magenge ya mafisadi ambayo wananyapiga vita kwani bila kuwa na mifumo na miundombinu iliyo wazi ya utawala na usimamizi wa wanachama ni vigumu mno kujiepusha na kuwa na kujikuta kikiwaweka kwenye utendaji wa serikali walewale kinaowapiga vita leo, wanaweza wakawa watu wengine (siyo Ngeleja, Maige, Mkulo, n.k. lakini watu wengine wenye hulka na tabia za watangulizi wao).

  Naomba mjadala wenye weledi
   
 2. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Hoja ni nzuri inazungumzia uwajibikaji wa chama na serikali zake, lakini cha ajabu mkuu wangu ni pale unaposema wewe ulikuwa wakala wa Mnyika huku hujui ofisi za chama, vile vile unaposema toka 2009 hadi leo hujapata fulsa ya kujiunga na CDM kwa vile tu hujui ofisi ya chama ilipo???, basi labda tu nikupongeze kwa kuwa wakala wa Mnyika bila kuwa mwanachama wa CDM.
   
Loading...