[Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.
Kwa upande wa posho, Slaa analipwa mafuta sh. 1,387,500 kwa lita 750 kwa mwezi huku fedha za majukumu zikiwa ni sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. 1,000,000.
Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa ni maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.
Dk. Slaa akiungwa mkono na Mbowe anadaiwa kujipatia posho ya nyumba mara mbili kwani ilishapendekezwa alipwe sh. milioni 40 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Licha ya kupewa fedha hizo, Dk.Slaa ameendelea kupewa posho nyingine ya nyumba ya sh. 1,000,000 kila mwezi huku akiwa tayari amelipwa na chama sh. milioni 40 kumalizia nyumba yake ambayo sasa anaishi.]
Hii kama ni kweli Dr. heshima inazidi kushuka. Itakuwa ni unafiki mkubwa sana, tofauti na maneno yake. Chama kinapitisha vitu njia za panya? Huu ni uhuni wa hali ya juu bila kuangalia nani kafanya au kwa sababu zipi. Dhambi ni dhambi haijalishi utaitetea vipi. Kama kweli ndo sasa tunaanza kuwatambua vizuri. Hebu makada wa CDM kanusheni kwa data na si matusi na kejeli.