CHADEMA wako tayari kumpokea Lowassa



Nimekusoma hapo mkuu, lakini unatakiwa kujiuliza kwanini Lowasa asiende chama kingine ila CDM?

Kwanini tuangaike na mtu ambae atatughalimu!? Usisahau hata mimi na wewe tumepata kufahamu Lowasa ufisadi wake baada ya kutajwa/kuchafuliwa na CDM, iweje leo hii mtu tuliyemtuhumu tuangaike kumsafisha!?
Hakika nakwambia madhara ya kumpokea EL ni makubwa kuliko faida!! Na kama unasema EL tuhuma zile hazikuwa zake inamaana huna imani na Dr. Slaa kwenye ile list of shame!! Yaani kwamba Dr. aliitoa bila uchunguzi!!

Ooh, eti akitubu asamehewe!! Si aende kanisani? Atubu nini wakati roho za ndugu zetu zimeishaondoka!!?

Nakuhakikishia ikitokea EL akaja CDM, ujue CDM KWISHA!!!
 
This is a foolish topic to discuss, be aware Lowasa kubaki CCM ni faida kwa chadema, na huenda akienda chama tofauti cdm ita step up
 
Lowassa ana mengi ya kusema kuhusu CCM ambayo hawezi kuyasemea huko CCM. Anatafuta venue. Na hataki kufanya kazi ya bure, angependa akiyafichua hayo yamfaidishe yeye na watakaokubaliana naye. Hatari ninayoiona hapo ya kumpokea CDM ni kuiambukiza ugonjwa wa 'umtandao' unaoinyonga CCM sasa hivi. Kete aliyonayo Lowassa ina nguvu za kuiua CCM lakini haitasaidia kile ambacho Chadema inapigania. Kete ya Lowassa inaweza kuingiza Chadema madarakani through blackmailing watawala wa sasa, kwa kuweka hadharani maovu yote aliyoshiriki, lakini Chadema ile itakayoshinda kwa msaada wa Lowassa haitakuwa Chadema hii hii tunayoizungumzia sasa, itakuwa Chadema mpya yenye ugonjwa wa 'umtandao' ambayo itakufa kifo cha haraka sana na kuwaachia wapiga kura majuto makuu.
 


Tuko pamoja mkuu, lakini hayo mengine hayana tija labda namba 1 na 5 na pia mkuu, kama anahitaji kustahafu akiwa clean si asitaafu akiwa hukohuko?
 
"Kumkaribisha Lowasa CDM ni sawa na kuiangamiza CDM!!"
Hivi wanachama wa kujiunga CDM watakuwa wameisha hadi kumkaribisha Lowasa!!??
Very pathetic!! Poor Mwigamba!!!

"Cost of Democracy"
Sioni tatizo hapo, mtu kama akitubu anastahili msamaha. Hapa tunazungumzia kama akiamua kujiunga na kuwa mwanachama wa CDM na sio kuwa mgombea urahisi..,
"Cost of Democracy"
 
Hivi mimi mbona siwaelewi hapa wadau!!? Eti EL anayo mengi ya kuongea akiingia CDM!! Yapi ambayo hamyajui??
EL ni dhahili anahitaji Urais, kwanini asijioshe akiwa CCM, hadi ahamie CDM!!? Jamani tutafakarini kwa kina!!
 
Hawa Jamaa Wamekubaliana kuanzisha chama chao........Wagombanao ndiyo wapatanano!stay tune

 
Kaazi kweli kweli, makanisani imeshindikana kutakaswa sasa wakimbilia CDM, haya nanyi mpokeeni then msikilizie muziki wake, kwani baada ya hapo ndipo mtapowafahamu Watanzania wa leo!!

 
"Cost of Democracy"
Sioni tatizo hapo, mtu kama akitubu anastahili msamaha. Hapa tunazungumzia kama akiamua kujiunga na kuwa mwanachama wa CDM na sio kuwa mgombea urahisi..,
"Cost of Democracy"


Kutubu aende kanisani sio CDM!! "Cost of Democracy", what a shame!!? Mkuu fikiria ndani ya box baada ya EL kuhamia CDM kutakuwepo na hasara ama faida gani!!
 
STIDE nakuelewa na naelewa faida na hasara za EL kujiunga CDM. Kikubwa kinachotakiwa ni kuiondoa CCM madarakani by any means ili tuanze upya haijalishi tunatumia silaha gani. Kitu kingine unachotakiwa kujua ni kuwa CCM imekuwa madarakani kwa miaka 50 kwa hiyo kuiondoa si kazi ya lelemama, inatakiwa watu wenye nguvu narudia tena wenye nguvu kutoka within wasaidie otherwise labda yatokee kama ya Kenya.

List of shame haijabadilika na ndio maana Mwigamba alisema akija ataulizwa atuambie yote tusiporizika ndio utakuwa mwisho wake kisiasa. Akiyaweka wazi madudu yote wewe huoni hiyo trick itakuwa knock out kick kwa serikali ya Kikwete na faida kwa wananchi?
 
"Kumkaribisha Lowasa CDM ni sawa na kuiangamiza CDM!!"
Hivi wanachama wa kujiunga CDM watakuwa wameisha hadi kumkaribisha Lowasa!!??
Very pathetic!! Poor Mwigamba!!!

lowassa siku atakapoingia chadema tutapishana naye mlangoni mimi nikitokea chadema kwenda kuanzisha chama kingine
 
Feedback, well said if so!! Lakini mkuu wewe unadhani EL ni mpumbavu kiasi hicho, yaani "upewe kwanza kombe alafu ndo mcheze fainal?"
Hakika lowasa akitua tu CDM utashuhudia makubwa kuanzia ndani ya chama hadi mtaani, hili halina ubishi Feedback!!

Kwanza ukae ukijua kwamba bado wananchi hawana imani na CDM 100% kulingana na yaliyowahi kutokea kwenye vyama vingine (nccr na cuf), hivo kitendo cha kumkaribisha EL wananchi tutajua ndo walewalee!! Alafu mkuu kwanini tuhangaike na mtu ambaye faida zake zinasoma below20?
 
imagine uko kwenye upande wowote wa haya makundi hapa chini....

1. wewe ni mkristo au muislam....changudoa anapoamua kumtumikia MUNGU. unasemaje?
2. wewe ni muumini wa assemblies of GOD...muislamu anaamua kuokoka. naomba opinion yako!
3. wewe ni muislamu swafi.....mkatoliki anaamua kusilimu. what's your take?
4. wewe ni mkristo au muislam....jambazi sugu anaamua kumtumikia MUNGU. niambie!
5. wewe ni ccm....dr slaa anaamua kujiunga ccm. sema sasa!
6. wewe ni chadema....chenge anaamua kuvua gamba na kuvaa gwanda. am listening...

what more can i say?
 
Jf sasa tunakwenda kusipo tutaonekana sio great thinker,1 ebu mwenye uhakika wa ufisadi wa lowasa auweke hadharani na lini alifanya,2 mwigamba kama mwenyekiti wa mkoa anahaki zote za kupokea yeyote ila tu kama wakiridhika na maelezo yake kama mtu ni fisadi itabidi wa muhoji na wamwaleze atoke hadharani kukanusha hayo mambo zaidi ya hapo mbona kina sitta, mwakyembe walio ficha ukweli hamsemi? au kwasababu kaharisha bata basi shida Je akihara kuku itakuwaje? hiyo heshima cdm walioipata haita shuka kwani wakimpokea atakuwa mwanachama kama wengine sio kiongozi kwani magamba walipo mpokea wassira au mzimu toka nccr walishuka hadhi? mbona aliapa akirudi afe?Hebu tujadili kwa busara na tumwogope mungu mwigamba ana haki kikatiba kufanya hivyo je wewe unajua katiba ya cdm?
 
Hivi mimi mbona siwaelewi hapa wadau!!? Eti EL anayo mengi ya kuongea akiingia CDM!! Yapi ambayo hamyajui??
EL ni dhahili anahitaji Urais, kwanini asijioshe akiwa CCM, hadi ahamie CDM!!? Jamani tutafakarini kwa kina!!

Umesahau au labda hujasikia jinsi alivyomtolea JK kwenye kikao cha halmashauri kuu yao Dodoma, akimkumbusha jinsi walivyoshirikiana kwenye Richmond hatua kwa hatua, JK hakujibu neno na hajakanusha hadi leo. Yapo mengine, ile ilikuwa trailer tu. Na sasa anawatishia, blackmailing, kwamba kuna mawili: wamteue kugombea urais, la sivyo ataenda Chadema kuyamwaga yote ya siri sirini yawe hadharani kweupe CCM ishindwe potelea mbali. Na haitaishia CCM kushindwa tu, hayo masuala mengi ni ya kijinai, watu wataenda lupango kwa mafungu wakati yeye atakuwa either na amnesty kwa kushiriki kufichua, au akifanikiwa kushawishi Chadema si ajabu akawa hata yeye ndiyo rais au akarejeshewa cheo chake cha PM.
 


Mimi binafsi nimeshamsamehe Lowasa baada ya kutafakari nimegundua Lowasa ni kiongozi kwa shupavu na hizi kashfa anazopewa zinatokana na ubovu wa viongozi waliokuwa wanamzunguka. Alwajibika kuonyesha ukomavu wa kiuongozi. Kashfa ya Richmond kama hamjui mhusika mkuu ni JK na swahiba Rostam. Kwanza Lowasa afanye maamuzi mengine magumu mapema ahamie Chadema na akishafanya hivyo awaeleze watanzania ukweli wa kilichotokea. najua mkimsikiliza mtajua mbivu na mbichi. Aliahidi siku moja kwamba muda ukifika atazungumza kuhusu Richmond aka Richmrisho aka Richaziz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…