George Maige Nhigula Jr.
JF-Expert Member
- Mar 14, 2008
- 470
- 149
Ndugu Wana JF,
Napenda kutoa changamoto kwa chama chetu cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na sisi wapenda mageuzi wote, Ni dhahiri kuwa uchaguzi umekwisha na chama cha Demokrasia na maendeleo kinabeba matumaini na ndoto za watanzania wengi hapo baadae kwani CHADEMA ni future ya nchi yetu.
CHADEMA kimepata mtaji mkubwa sana wa kisiasa kubeba agenda ya mabadiliko hususani kanda ya ziwa inayobeba mikoa mikubwa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, na Kagera na mikoa ya Nyanda za juu kusini yaani Mbeya, Iringa na Ruvuma, hali kadhalika mikoa ya Kazikazini yaani Kilimanjaro, Arusha na Manyara
Mikoa hii inawapiga kura zaidi ya 60% ya wapiga kura Tanzania nzima, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha mikoa hii inabaki kuwa ngome kuu ya upinzani kwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu, viwanda, madini, ardhi na maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja. hivyo ni wakati wa kuchapa kazi na kuwa prove ccm wrong kuwa Tanzania yenye neema tele inawezekana, na kwa kutimiza ndoto hizo za watanzania wengi kwenye majimbo yaliyodiliki hatuna budi sisi sote kushiriki kukisaidia chama chetu ili kiweze kujijenga na kuwapa imani watanzania wengi ambao bado hawaja elewa agenda ya mabadiliko.
Hivyo basi changamoto yangu ya kwanza ni kwa viongozi wa chama hususani Dr W. SLAA, Mabere Marando, Wabunge wote, madiwani na viongozi wote wa chama, DR SLAA atakuwa na mda mwingi wa kutosha hivi sasa kuratibu miradi ya maendeleo kwenye majimbo yote na halimashauri zote zinazoendeshwa na CHADEMA kwa kutushirikisha sisi wananchi,
Kuna kundi la vijana wengi wasomi na baadhi ya wazalendo wasomi ambao wana mapenzi na chadema, na Wako tayali kushiriki kwa namna moja au nyingine kuleta hayo mabadiliko na yatakayotia chachu ya ukombozi na kuaminika kwa chadema kama chama makini na mbadala kwa kuliongoza taifa letu katika karne hii ya 21.
Vile vile Chadema inatakiwa kutumia nguvu, ujuzi na mtaji wa watanzania waishio nje ya nchi yaani DIASPORA, Kundi hili limeongoza kwa kufanya na kuratibu kampeni za Chadema online na ni kundi muhimu linaloweza kutumiwa kutafuta wafadhili na investors ambao wataweza kuwekeza kwenye miradi mbalimbali itakayo ratibiwa na CHADEMA,
Hivyo, CHADEMA hawatakiwi kupoteza mda hivi sasa , viongozi wetu wanatakiwa kutangaza utaratibu ulio wazi wa kuwawezesha watanzania walio ndani na nje ya nchi kuchangia kuleta mabadiliko tunayoyahitaji, ni dhahiri kuna miradi mingi ya kusaidia hospitali zetu kuwa na vifaa muhimu kama vitanda, magodoro etc, shule zetu kuwa na vifaa vya maabara, madawati, vitabu haya ni mambo rahisi kama viongozi wetu watakuwa na utaratibu wa wazi na wa kueleweka na kuwashirikisha wananchi.
Kama watu wanaweza kuchangia political campaign hali kadhalika harambee zifanyike kuchangia kusomesha watoto wetu ndani na nje ya nchi.
Kuhusu kusaidia vijana wengi ambao wanataka mabadiliko CHADEMA ije na miradi kama ya kuanzisha chuo cha ujasiliamari na ufundi cha chama ambacho kitasaidia kutoa mafunzo kwa vijana wengi na kuwasaidia kupata mitaji yenye masharti nafuu ndani na nje ya nchi na kuzitumia fursa mbalimbali za kibiashara kama AGOA kwa manufaa ya watanzania wazalendo na wazawa ambazo fursa kama za AGOA zinatumiwa na watanzania wengi wenye asili ya kiasia.
Chadema, inabidi ije na miradi endelevu kama nilivyosema hapo juu kufungua chuo cha ujasilia mali na ufundi kwa kila kanda, na kutilia mkazo katika ujasiliamali wa kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili tuweze kujikomboa kwa kuzalisha baadhi ya bidhaa nchini kwetu badala ya kuagiza toka nje ya nchi.
Miradi hii inawezekana kwa kuwashirikisha watanzania DIASPORA ambao wana access kubwa ya kuweza kupata wafadhili au kutoa mchango wa utaalamu wao na uratibu wa programme hizo, nchi kama china zimefanikiwa sana katika maendeleo ya viwanda vidogovidogo kutokana na kutumia uwezo wa vijana wake walikwenda nje ya nchi kujifunza na kupata ujuzi ambao umeifaidisha china na kupiga hatua kubwa ya maendeleo ya viwanda.
Hivyo basi huu ni wakati muafaka wa kujenga ngome iliyo imara ya chadema, ambayo ni Kanda ya Ziwa, Nyanda za juu kusini, na kanda ya kazikazini na baadhi ya maeneo ambayo ni ngome ya upinzani kama, Dar es laam, Kigoma na Rukwa.
Nashukuru sana ndugu zangu, Napenda kuwakilisha hoja.