CHADEMA wajipange kufanya km walivyoishinda CCM Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu Kusini

George Maige Nhigula Jr.

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
470
149
Ndugu Wana JF,

Napenda kutoa changamoto kwa chama chetu cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na sisi wapenda mageuzi wote, Ni dhahiri kuwa uchaguzi umekwisha na chama cha Demokrasia na maendeleo kinabeba matumaini na ndoto za watanzania wengi hapo baadae kwani CHADEMA ni future ya nchi yetu.

CHADEMA kimepata mtaji mkubwa sana wa kisiasa kubeba agenda ya mabadiliko hususani kanda ya ziwa inayobeba mikoa mikubwa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, na Kagera na mikoa ya Nyanda za juu kusini yaani Mbeya, Iringa na Ruvuma, hali kadhalika mikoa ya Kazikazini yaani Kilimanjaro, Arusha na Manyara

Mikoa hii inawapiga kura zaidi ya 60% ya wapiga kura Tanzania nzima, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha mikoa hii inabaki kuwa ngome kuu ya upinzani kwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu, viwanda, madini, ardhi na maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja. hivyo ni wakati wa kuchapa kazi na kuwa prove ccm wrong kuwa Tanzania yenye neema tele inawezekana, na kwa kutimiza ndoto hizo za watanzania wengi kwenye majimbo yaliyodiliki hatuna budi sisi sote kushiriki kukisaidia chama chetu ili kiweze kujijenga na kuwapa imani watanzania wengi ambao bado hawaja elewa agenda ya mabadiliko.

Hivyo basi changamoto yangu ya kwanza ni kwa viongozi wa chama hususani Dr W. SLAA, Mabere Marando, Wabunge wote, madiwani na viongozi wote wa chama, DR SLAA atakuwa na mda mwingi wa kutosha hivi sasa kuratibu miradi ya maendeleo kwenye majimbo yote na halimashauri zote zinazoendeshwa na CHADEMA kwa kutushirikisha sisi wananchi,

Kuna kundi la vijana wengi wasomi na baadhi ya wazalendo wasomi ambao wana mapenzi na chadema, na Wako tayali kushiriki kwa namna moja au nyingine kuleta hayo mabadiliko na yatakayotia chachu ya ukombozi na kuaminika kwa chadema kama chama makini na mbadala kwa kuliongoza taifa letu katika karne hii ya 21.

Vile vile Chadema inatakiwa kutumia nguvu, ujuzi na mtaji wa watanzania waishio nje ya nchi yaani DIASPORA, Kundi hili limeongoza kwa kufanya na kuratibu kampeni za Chadema online na ni kundi muhimu linaloweza kutumiwa kutafuta wafadhili na investors ambao wataweza kuwekeza kwenye miradi mbalimbali itakayo ratibiwa na CHADEMA,

Hivyo, CHADEMA hawatakiwi kupoteza mda hivi sasa , viongozi wetu wanatakiwa kutangaza utaratibu ulio wazi wa kuwawezesha watanzania walio ndani na nje ya nchi kuchangia kuleta mabadiliko tunayoyahitaji, ni dhahiri kuna miradi mingi ya kusaidia hospitali zetu kuwa na vifaa muhimu kama vitanda, magodoro etc, shule zetu kuwa na vifaa vya maabara, madawati, vitabu haya ni mambo rahisi kama viongozi wetu watakuwa na utaratibu wa wazi na wa kueleweka na kuwashirikisha wananchi.

Kama watu wanaweza kuchangia political campaign hali kadhalika harambee zifanyike kuchangia kusomesha watoto wetu ndani na nje ya nchi.

Kuhusu kusaidia vijana wengi ambao wanataka mabadiliko CHADEMA ije na miradi kama ya kuanzisha chuo cha ujasiliamari na ufundi cha chama ambacho kitasaidia kutoa mafunzo kwa vijana wengi na kuwasaidia kupata mitaji yenye masharti nafuu ndani na nje ya nchi na kuzitumia fursa mbalimbali za kibiashara kama AGOA kwa manufaa ya watanzania wazalendo na wazawa ambazo fursa kama za AGOA zinatumiwa na watanzania wengi wenye asili ya kiasia.

Chadema, inabidi ije na miradi endelevu kama nilivyosema hapo juu kufungua chuo cha ujasilia mali na ufundi kwa kila kanda, na kutilia mkazo katika ujasiliamali wa kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili tuweze kujikomboa kwa kuzalisha baadhi ya bidhaa nchini kwetu badala ya kuagiza toka nje ya nchi.

Miradi hii inawezekana kwa kuwashirikisha watanzania DIASPORA ambao wana access kubwa ya kuweza kupata wafadhili au kutoa mchango wa utaalamu wao na uratibu wa programme hizo, nchi kama china zimefanikiwa sana katika maendeleo ya viwanda vidogovidogo kutokana na kutumia uwezo wa vijana wake walikwenda nje ya nchi kujifunza na kupata ujuzi ambao umeifaidisha china na kupiga hatua kubwa ya maendeleo ya viwanda.

Hivyo basi huu ni wakati muafaka wa kujenga ngome iliyo imara ya chadema, ambayo ni Kanda ya Ziwa, Nyanda za juu kusini, na kanda ya kazikazini na baadhi ya maeneo ambayo ni ngome ya upinzani kama, Dar es laam, Kigoma na Rukwa.

Nashukuru sana ndugu zangu, Napenda kuwakilisha hoja.
 
kipipili

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
1,590
182
Mkuu umeleta kitu cha msingi sana katika kujipanga kwa chama chetu kuelekea 2015. Nilikuwa nije na sredi inayofanana na hii. Hii ni baada ya kutafakari jinsi uchaguzi mkuu ulivyofanyika.

Kwa kweli lazima tukubali chama chetu kimepata mafanikio makubwa sana ukijumlisha vigezo vyote. Kikubwa hasa ambacho mimi binafsi nilikuwa napendekeza kwa uongozi wa chadema ni kuunda kurugenzi ya serikali za mitaa. Mkurugenzi wake afanane kabisa na waziri kwa maana ya kufuatilia na kusimamia halmashauri zote zilizoko chini ya chadema (10?) ili basi halmashauri hizo ziwe mfano wa kuigwa katika masuala yote ikiwemo utawala bora, ukusanyaji mapato, matumizi mazuri ya mapato, kuanzisha miradi endelevu nk.

Pendekezo langu kwa mkurugenzi huyo ni kuwa awe aidha mmoja wa wabunge ambao hawatoki kwenye halmashauri zinazoongozwa na chadema au mwanachama yeyote msomi na mweledi katika masuala ya utawala na fedha. Pia ingewezekana awe muajiriwa rasmi kwa ajili ya kazi hiyo kwa maana ya kufuatilia kwa karibu utendaji wa halmashauri husika. Hakika awe waziri kabisa wa serikali za mitaa za chadema.

I have no more to say.
 
kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,021
364
Na mimi naomba kuchangia kidogo..

Nimefarijika kuona watu mnakuja na positive ideas za niini kifanyike ikiwa ni mkakati wa kuelekea 2015.. wengi wanaweza kudhani bado mapema, lakini ni lazima kuanza kufanya SWOT analysis mapema kujua wapi kuna nguvu, wapi kuna mapungufu. aidha ni muhimu kujua wapi kuna opportunity na wapi kuna hatari au threats.

Mleta mada kaeleza vizuri. Kikubwa ni kwa wabunge kuelewa matatizo ya wananchi na kuyatetea katika ngazi mbalimbali-- inabidi kuhakikisha wanafanya kazi kwa ukaribu sana na wananchi, madiwani pamoja na halmashauri.. halitakuwa jambo jema kurudi Dar es salaam na kuendelea na shughuli binafsi wakati unatakiwa uwepo jimboni kwako... Napendekeza CHADEMA wawe na utaratibu wa ku-monitor utendaji kazi wa wabunge wao.. ikiwewezekana wawekeane performance targets mfano.. idadi ya mikutano watakayofanya katika majimbo yao kwa muda fulani, idadi ya miradi ya maendeleo iliyoibuliwa kwa kushirikiana na wananchi.

Najua mojawapo ya THREAT itakayowakabili ni serikali kupunguza financial support kwa majimbo yaliyo na wapinzani ili ionekane hawajafanya kitu.. lakini hima tafadhali jitahidini sana kuwa ngangali na halmashauri za wilaya, miji, manispaa na jiji.

Lastly, naomba CHADEMA, muwe mnawapa msasa wabunge wenu as part of Capacity building strategy.. kwa mfano Zitto kabwe ana uwezo katika nyanja fulani.. basi atoe somo kwa wabunge wenzie.. au Mbowe, Mnyika etc katika eneo fulani basi mzidi kufundishana.. na inapowezekana mshirikishe taasisi za elimu au consultancy firm kwa ajili ya kufanya surveys mbalimbali na Capacity building..

Nawasilisha kwa sasa.
 
George Maige Nhigula Jr.

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
470
149
Mkuu umeleta kitu cha msingi sana katika kujipanga kwa chama chetu kuelekea 2015. Nilikuwa nije na sredi inayofanana na hii. Hii ni baada ya kutafakari jinsi uchaguzi mkuu ulivyofanyika. Kwa kweli lazima tukubali chama chetu kimepata mafanikio makubwa sana ukijumlisha vigezo vyote. Kikubwa hasa ambacho mimi binafsi nilikuwa napendekeza kwa uongozi wa chadema ni kuunda kurugenzi ya serikali za mitaa. Mkurugenzi wake afanane kabisa na waziri kwa maana ya kufuatilia na kusimamia halmashauri zote zilizoko chini ya chadema (10?) ili basi halmashauri hizo ziwe mfano wa kuigwa katika masuala yote ikiwemo utawala bora, ukusanyaji mapato, matumizi mazuri ya mapato, kuanzisha miradi endelevu nk. Pendekezo langu kwa mkurugenzi huyo ni kuwa awe aidha mmoja wa wabunge ambao hawatoki kwenye halmashauri zinazoongozwa na chadema au mwanachama yeyote msomi na mweledi katika masuala ya utawala na fedha. Pia ingewezekana awe muajiriwa rasmi kwa ajili ya kazi hiyo kwa maana ya kufuatilia kwa karibu utendaji wa halmashauri husika. Hakika awe waziri kabisa wa serikali za mitaa za chadema. I have more to say.

Good idea mzalendo, Chadema walitakiwa wawe na msemaji wa chama ndani ya JF, kazi yake iwe ni kukusanya maoni yetu na kutupa feedback ili tuweze kujua kuwa chama kina fikra gani na mwelekeo upi kuhusuana na mapendekezo yetu hapa JF, hiyo itatutia moyo kuweza kujitoa zaidi na kukipa chama mikakati na mbinu za kisasa kuweza kujijenga zaidi.

Nimejaribu kuwasiliana na chama kwenye email zake zilizo kwenye website lakini naona CHADEMA wanatatizo kubwa la communication and feedback, kama chama makini inabidi kuimarisha mfumo wa mawasiliano kwa umma na feedback na kuhakikisha kila mwanachama au mpenzi wa chama anajibiwa kwa haraka.

Vile vile CHADEMA wanatakiwa kuzitangaza wazi wazi kwa wananchi namba za hotline, email adress ambazo zitakuwa zinaratibiwa na kupokea maoni na mapendekezo au malalamiko ya chama, hali kadhalika awepo ofisa wa chama kazi yake ni kupokea na kuratibu hayo mapendekezo na kutoa feedback haraka iwezekanavyo baada ya kupata msimamo wa chama, mtu huyu ajuulikane na contacts zake ziwe wazi kwa wananchi wote. Lazima chama kiwe na utaratibu wa kisasa wa kuweza kuwasiliana na wananchi.
 
George Maige Nhigula Jr.

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
470
149
Na mimi naomba kuchangia kidogo..

Nimefarijika kuona watu mnakuja na positive ideas za niini kifanyike ikiwa ni mkakati wa kuelekea 2015.. wengi wanaweza kudhani bado mapema, lakini ni lazima kuanza kufanya SWOT analysis mapema kujua wapi kuna nguvu, wapi kuna mapungufu. aidha ni muhimu kujua wapi kuna opportunity na wapi kuna hatari au threats.

Mleta mada kaeleza vizuri. Kikubwa ni kwa wabunge kuelewa matatizo ya wananchi na kuyatetea katika ngazi mbalimbali-- inabidi kuhakikisha wanafanya kazi kwa ukaribu sana na wananchi, madiwani pamoja na halmashauri.. halitakuwa jambo jema kurudi Dar es salaam na kuendelea na shughuli binafsi wakati unatakiwa uwepo jimboni kwako... Napendekeza CHADEMA wawe na utaratibu wa ku-monitor utendaji kazi wa wabunge wao.. ikiwewezekana wawekeane performance targets mfano.. idadi ya mikutano watakayofanya katika majimbo yao kwa muda fulani, idadi ya miradi ya maendeleo iliyoibuliwa kwa kushirikiana na wananchi.

Najua mojawapo ya THREAT itakayowakabili ni serikali kupunguza financial support kwa majimbo yaliyo na wapinzani ili ionekane hawajafanya kitu.. lakini hima tafadhali jitahidini sana kuwa ngangali na halmashauri za wilaya, miji, manispaa na jiji.

Lastly, naomba CHADEMA, muwe mnawapa msasa wabunge wenu as part of Capacity building strategy.. kwa mfano Zitto kabwe ana uwezo katika nyanja fulani.. basi atoe somo kwa wabunge wenzie.. au Mbowe, Mnyika etc katika eneo fulani basi mzidi kufundishana.. na inapowezekana mshirikishe taasisi za elimu au consultancy firm kwa ajili ya kufanya surveys mbalimbali na Capacity building..

Nawasilisha kwa sasa.

Nashukuru sana mzalendo kwa kuwa na vision nzuri ya kujenga chama chetu, tuendelee kujidhatiti na kutoa changamoto na mapendekezo ya kujenga nguvu na mtaji mkubwa wa kisiasa ambao utakuwa chachu ya kuaminika kwa chama chetu kama kitabeba agenda ya mabadiliko sasa kwa kidogo tulichonacho ili wananchi waweze kuwa na imani kubwa.

Ningependa agenda zetu nyingi hapa JF zijikite katika shughuli za maendeleo na jinsi gani tunasshiriki kuisadia chadema kuweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye Halmashauri na majimbo yanayo ongozwa na CHADEMA, kuliko kuendelea kujadili hoja ambazo hazina tija kwa taifa letu na chama chetu, JF iwe chachu ya mabadiliko tunayoyataka na kutuo vision ni jinsi gani tunaweza kushiriki moja kwa moja kuwezesha CHADEMA kufikia malengo
 
MTWA

JF-Expert Member
Aug 5, 2009
1,156
160
Maombo yangu ni kuwa viongozi wa CHADEMA wajipange hata zaidi ya hapo, Kama umeshatambua kitu, utakuta kuwa |CCM sasa wamejikita sana katika kuwamaliza wabaya wao, na hawa CHADEMA hawawezi kujitoa kwa shuluba walizowapa CCM miaka hii na hasa wakati huu wa uchaguzi. Mfano mzuri ni kuwahonga au kusambaratisha vyama vya upinzani kwa hela za wananchi

Bado kuna hatari kubwa sana kuwa pesa nyingi katika kuwahonga hata baadhi ya wanaCHADEMA wenyewe. So, kama hii consolidation hawataifanya mapema, tusishangae kuona hata baadhi ya figure ndani ya chama wakajitoa eti kukosoa chama. I pray lets not happen.

Ushahidi jamani wa kuendelea kutumia fedha zetu bado tunakusanya! ila mojawapo ni fedha zilizotakiwa kufika katika sekta nyeti kudaiwa kuwa zinatumika katika uchaguzi na hali hazina washatoa kwaajili ya kazi hiyo.

Hivyo naomba kuunga mkono shughuli ya CHADEMA waanze kazi hii mapema sana na wawe pamoja na kufanya semina nyingi za kimya kimya na ikibiidi kila kabla ya mkutano wa bunge wakae kujadili kwa kina maada zao ndo waingie wakiwa wamejipanga. Japo kuna kazi ngumu sana na huyo MAKINDA WA MAFISADI
 
Far star

Senior Member
Nov 3, 2010
139
0
Good idea mzalendo, Chadema walitakiwa wawe na msemaji wa chama ndani ya JF, kazi yake iwe ni kukusanya maoni yetu na kutupa feedback ili tuweze kujua kuwa chama kina fikra gani na mwelekeo upi kuhusuana na mapendekezo yetu hapa JF, hiyo itatutia moyo kuweza kujitoa zaidi na kukipa chama mikakati na mbinu za kisasa kuweza kujijenga zaidi.

Nimejaribu kuwasiliana na chama kwenye email zake zilizo kwenye website lakini naona CHADEMA wanatatizo kubwa la communication and feedback, kama chama makini inabidi kuimarisha mfumo wa mawasiliano kwa umma na feedback na kuhakikisha kila mwanachama au mpenzi wa chama anajibiwa kwa haraka.

Vile vile CHADEMA wanatakiwa kuzitangaza wazi wazi kwa wananchi namba za hotline, email adress ambazo zitakuwa zinaratibiwa na kupokea maoni na mapendekezo au malalamiko ya chama, hali kadhalika awepo ofisa wa chama kazi yake ni kupokea na kuratibu hayo mapendekezo na kutoa feedback haraka iwezekanavyo baada ya kupata msimamo wa chama, mtu huyu ajuulikane na contacts zake ziwe wazi kwa wananchi wote. Lazima chama kiwe na utaratibu wa kisasa wa kuweza kuwasiliana na wananchi.

fungua mtandao wa chama nadhani kuna utaratibu huu ndugu yangu.
 
George Maige Nhigula Jr.

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
470
149
fungua mtandao wa chama nadhani kuna utaratibu huu ndugu yangu.

Nimejaribu kuwasiliana na chama kupitia contacts za kwenye mtandao lakini hawajawahi nipa any feedback, kuna tatizo kwenye communication and feedback na hili tatizo linaweza kuwakatisha tamaa wapenzi wengi wa chadema ambao wanataka kuwa involved kukijenga chama.
 
kipipili

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
1,590
182
Nimejaribu kuwasiliana na chama kupitia contacts za kwenye mtandao lakini hawajawahi nipa any feedback, kuna tatizo kwenye communication and feedback na hili tatizo linaweza kuwakatisha tamaa wapenzi wengi wa chadema ambao wanataka kuwa involved kukijenga chama.
ni kweli mkuu, kwenye mtandao wa chadema bado hakujakaa vizuri ndiyo maana hata online registration haiwezekani, cant we do something here, we as members and wellwishers
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom