CHADEMA wajichimbia kunoa makali

CHADEMA wajichimbia kunoa makali

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,458
SEKRETARIETI ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),imejichimbia mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kutengeneza mpango mkakati wanamna ya kuendesha shughuli zao kwa mwaka huu.

Itakumbuka kuwa moja yamaazimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jijini Dar es Salaam mwishonimwa mwaka jana, iliazimiwa kuwa mwaka 2013 ni wa kutumia nguvu ya ummakuishinikiza serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kuwajibika kwa wananachi.

Akizungumza na Tanzania Daimajana, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema mpango huo ni sehemuya mpango mkubwa wa miaka mitano wa chama hicho ulioanza mwaka 2011 nakuendelea hadi 2016.

Alifafanua kuwa kulikuwa naminon'gono kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa baadhi ya wajumbe wakiwamowabunge wa chama hicho, hawakualikwa kwenye kikao hicho, jambo alilodai kuwa niuzushi.

Dk. Slaa alisema kuwa wajumbewasiotokana na sekretarieti walioalikwa ni wale wenye majukumu maalumu ndani yachama.
"Sisi tuna wabunge 49 na katikakikao hiki wabunge waliohudhuria ni sita, ukimuacha Mwenyekiti wetu, FreemanMbowe na hawa wabunge wameingia kwa kofia za nafasi zao katika chama,"alifafanua.

Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwamkakati wanaoupanga utafika katika ngazi nyingine za chama hicho kwa uamuzikabla ya kutekelezwa.

Kwa sasa CHADEMA imejizatitikwa kile inachokieleza kuwa ni mikakati maalumu ya kuchukua dola kutoka kwaChama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015.
Katika kudhibiti hilo, chamakimewataka wanachama wake kuacha kupoteza muda kwa kulumbana juu ya nani awemgombea urais na badala yake utatengenezwa utaratibu maalumu wa wanachamakutangaza nia.

Hivi karibuni Mwenyekiti wachama hicho, Mbowe, aliweka bayana kuwa hana mpango wa kuwania wadhifa huo waurais na badala yake atakuwa na jukumu la kuwafunda wagombea makiniwatakaopeperusha bendera ya chama hicho kwa nafasi zote za uongozi wa vijiji namitaa, udiwani, ubunge na urais
 
Back
Top Bottom