Chadema waitunishia Polisi misuli


Negotiator

Negotiator

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2010
Messages
303
Likes
3
Points
0
Negotiator

Negotiator

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2010
303 3 0
Chadema waitunishia Polisi misuli Send to a friend Monday, 29 November 2010 09:01 0diggsdigg


chadematundu.jpg
Mkurugenzi wa Sheria Katiba na Haki za Binadamu wa chadema Tundu Lisu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kitendo cha Polisi kuzuia mikutano ya wabunge wa chama hicho nchi nzima.Picha na Fidelis Felix

Mussa Mkama na Geofrey Nyang’oro
WIGO wa mvutano kati ya Jeshi la Polisi na Chadema unaotokana na chombo hicho cha dola kukizuia chama hicho kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima, 'hadi hapo hali itakapotengemaa' umezi kupanuka huku Chadema ikitishia kufikisha suala hilo bungeni na ikishindikana, itashawishi wanachama wake majimboni kutafanya mikutano, ili wakamatwe.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sheria Katiba na Haki za Binadamu, Tundu Lisu, alisema kitendo cha polisi kuzuia mikutano ya wabunge wa Chadema ni cha kuingilia kinga na mamlaka ya Bunge, zinazotambulika kimataifa.

Ijumaa iliyopita, Kamanda Clodwig Mtweve, ambaye mara kadhaa amekuwa akikaimu shughuli za Mkuu wa Jeshi la Polisi, alikiri kuwepo kwa agizo la kukizuia chama hicho, kuendesha mikutano ya hadhara.

Kamishna Mtweve, ambaye ana dhamana ya mambo ya utawala na rasilimali katika jeshi hilo, alisema 'maombi ya Chadema ambayo tumeyapokea yanaambatana na maandamano na wanasema ni maandamano ya kuhitimishwa kwa sherehe za mikutano ya hadhara ya kupongezana kwa ushindi."

"Sasa sisi tumeyakataa na kama ni sherehe za kupongezana, tunasema zifanyike ukumbini. Na hii si kwa Chadema tu, bali hata kwa chama tawala," alisisitiza.

Chadema iliweka rekodi ya kutwaa majimbo mengi ya Tanzania Bara katia uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita.

Katika baadhi ya majimbo, chama hicho chenye nguvu kubwa ya upinzani dhidi ya sehemu, kilishindwa kwa tofauti ya ndogo ya kura, jambo lililosababisha kuibuka kwa vurugu zilizotokana na wananchi kudai matokeo yatangazwe mapema.

Katika mazungumzo yake ya jana, Lisu alisema sheria ya kinga, mamlaka na haki za Bunge ya mwaka 1988 chini ya kifungu cha nne cha sheria hiyo, mbunge atakuwa na haki ya kufanya mikutano ya hadhara na mamlaka zote husika zitatakiwa kuwezesha mikutano hiyo kufanyika kwa namna itakayomfaa mbunge na kadri inavyowezekana kwa mazingira yaliyopo.

Alisema kwa msingi huo, ni kosa la jinai chini ya sheria hiyo kwa mtu yeyote kuzuia mikutano hiyo na kwamba mtu huyo, anaweza kushtakiwa na mamlaka husika kwa mujibu wa sheria.

Lisu alisema lengo la polisi ni kuwakamata wabunge wa chama hicho, watafanya mkikutano yao ili wakamatwe, na kwamba wabunge hawaweza kukaa bila kuzungumza na wananchi wao waliowapa mamlaka na nguvu kisheria, kuingia katika chombo nyeti cha kutunga sheria za nchi.

"Tunajua wao lengo lao si kutukamata, sasa sisi tutafanya mikutano ili watukamate, lakini hatuwezi kuvumilia kuona wananchi wananyimwa haki ya kukusanyika na kuwasikiliza wabunge wao. Tutaachana na mambo mengine kwanza, ili tuipeleke hoja hii bungeni, hicho ndicho kitakuwa kitu cha kwanza kabla ya yote," alisema Lisu.

Lisu alisema vitendo vya polisi vinaashiria hatari kubwa kwa uhai wa demokrasia, katiba na sheria za nchi hasa inapofikia hatua ya kupiga marufuku wananchi kujumuika katika mikutano ya hadhara.

"Huo ni mwanzo wa kuielekeza nchi katika dola ya kipolisi mithili ya Zimbabwe ya Robert Mugabe, Kenya ya zamani ya Daniel arap Moi na Afrika Kusini ya wakati wa makaburu," alisema.

"Jeshi la Polisi linapopiga marufuku mikutano ya wabunge majimboni kwao ni mwanzo wa kupiga marufuku mijadala huru bungeni na kuielekeza nchi katika utawala wa kiimla kama siyo udikteta wa kijeshi," alisisitiza Lisu.

Alisema Chadema kama chama kikuu cha upinzani kilichobeba matumaini ya mabadiliko ya Watanzania wengi, hakiwezi kukubali nchi kugeuzwa kuwa Zimbabwe ya Afrika Mashariki.

Mkurugenzi huyo wa sheria katika Chadema, alisema chama hicho pia hakiwezi kukubali wabunge wake kunyamazishwa na Bunge kurudishwa kuwa kamati ya Chama Cha Mapinduzi kama ilivyokuwa katika enzi ya chama kimoja.
"Chadema haiwezi kukaa kimya wakati haki za wananchi zinazotambuliwa na kulindwa na katiba na sheria nyingine za nchi yetu, zinakanyagwa na Jeshi la Polisi kwa visingizio vya taarifa za kiintelijensia visivyokuwa na msingi wowote," alisema.

Lisu alisema jeshi hilo limezuia mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika katika uwanja wa Kwaraa, mjini Babati, kwa ajili ya kumpokea mbunge wa viti maalum wa chama hicho, Paulina Gekul na kwamba mkutano huo ulipangwa kufanyika Novemba 19 mwaka huu.

Pia alidai mkutano wa Vincent Nyerere uliopangwa kufanyka Novemba 22 mwaka huu katika uwanja wa Shula ya Msingi Mukendo, mjini Musoma nao umepiga marufuku.

Kwa mujibu wa Lisu, mikutano mingine ya wabunge wa Chadema iliyopigwa marufuku ni ya Saidi Arfi wa Mpanda Kati, Annamary Mallack wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Mchungaji Peter Msingwa wa Iringa Mjini, Joseph Mbilinyi wa Mbeya Mjini na Ezekiel Wenje wa Jimbo la Nyamagana, jijini Mwanza.

Hali kadhalika mkutano wa hadhara uliokuwa umepangwa kufanyika jana, katika jimbo la Segerea, jijini Dar es Salaam.Lisu alisema Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ukonga, Dar es Salaam amedai kuwa mikutano yote na maandamano ya kisiasa, imezuiwa kutokana na hali ya kiusalama.

“Polisi haitoi ufafanuzi wowote juu ya vyanzo vya taarifa hizo wanazodai ni za kiintelijensia wala kutaja vyama vinavyodaiwa kuwa na nia mbaya na linaelekea kuamini kuwa halina wajibu wa maelezo yoyote kuthibitisha madai hayo.
Sasa kama hivyo ndivyo, basi lina haki ya kusimamia na kuhakikisha mikutano inafanyika kwa amani kutokana na taarifa hizo walizozipata," alisema Lisu.

Wakati huo huo, suala la kuwepo kwa kambi moja ya upinzani yenye nguvu bungeni, limezidi kuwa tata baada ya viongozi wa Chadema na CUF kuendelea kutoleana matamko mazito yanayoonyesha kutoafikiana.

Jana, Chadema iliitaka CUF kutoa msimamo wake kuhusu mabadiliko ya kumi ya katiba ya Zanzibar.

Chadema ilidai kuwa mabadiliko hayo yaliyoitambulisha Zanzibar kuwa ni nchi, yamevunja katiba ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania na kuhatarisha Muungano uliodumu kwa zaidi ya miongo minne.

"Makubaliano ya nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar ilikuwa kuunda nchi moja ambayo ni Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, sasa makubalino ya CCM na CUF yanaturudisha kwenye nchi mbili ambapo katiba ya sasa ya Zanzibar inaitambua kuwa ni nchi yenye mipaka inayotambulika kikatiba, ”alisema Lisu.

Akifafanua zaidi kuhusu msimamo huo, Lisu alisema suala si kugawana vyeo vya upinzani bungeni bali kujadili na kukubalina kimsingi mambo yanayohusu mstakabali wa taifa kwa jumla.

"Tunaomba kuelezwa, kwa kuwa CCM na CUF wameshajitangazia uhuru Zanzibar, vipi kuhusu Muungano wetu, agenda ya CUF kwa Tanzania bara ni ipi hata wakataka tushirikiane nao, tunatarajia kusikia hoja ya CUF kuhusu hili kabla ya sisi kupeleka hoja yetu bungeni," alisema Lisu.

Alisema chama hicho kinatarajia kupeleka hoja binafsi bungeni kuhusu kuvunjwa kwa katiba ya nchi na sheria zake ambazo kimsingi, zinahatarisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chadema imewahakikishia Watanzania kuwa kama kitaunda kambi ya upinzani bungeni peke yake, hakutakuwa na tatizo lolote kwa kuwa kina sifa ya kufanya hivyo kwa mjibu wa sheria na kwamba hakuna sheria inayolazimisha kuungana.

Akifafanua hilo wakili wa maarufu nchini, Mabere Marando alisema hata CUF, iliwahi kunda Kambi ya Upinzani Bungeni mwaka 1995, ikiwatumiwa wabunge wache wa UDP na kuwaacha Chama cha NCCR-Mageuzi ambacho katika kipindi hicho, kilikuwa na wabunge wengi.

SOURCE; Chadema waitunishia Polisi misuli
 
L

Leonard Akaro

JF Gold Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
56
Likes
0
Points
13
L

Leonard Akaro

JF Gold Member
Joined Nov 1, 2010
56 0 13
Ndugu Viongozi wa CHADEMA. Hatima ya maendeleo ya Taifa hili yako mikononi mwenu. Tuko nyuma yenu, wakati wa kupambana ni huu. Taifa hili lilichelewa kimaendeleo, kiuchumi, kielimu, n.k. kwasababu tu CCM hawakapa challenge na wakajiendeshea nchi kama watakavyo.

Tutawapa support ya kila khali. Let we fight for our country.
 

Forum statistics

Threads 1,236,312
Members 475,050
Posts 29,253,869