CHADEMA wagawa bendera za UKUTA

CHADEMA wagawa bendera za UKUTA

Huyu mwananchi huyu!!! Ngoja tu yule kiongozi wa mambo ya news ajipange. Maana najua ameshawawekea mtego. Muda si mrefu gazeti pekee litakaloruhusiwa ni FREEDOM
 
Mafisadi si wakamatwe kelele kelele tu unanyima watu haki ya kikatiba kisingizio ufisadi fisadi gani umemkamata na kumuhukumu?
Nafurahi sana kama watanzania wameanza kufunguka nakupuuza propaganda za kijinga.
 
View attachment 380858
View attachment 380859
Timu UKUTA kuna kofia truk suti miwani mifuko na mambo mengine



swissme



Ni wazo zuri la kulinda demokrasia.

Nchi hii yenye makabila 125 na madhehebu ya dini zaidi ya 50 + haitawezekana kamwe kutawaliwa na mawazo ya mtu mmoja.

Ni bora sasa watu waanze kupewa elimu na kuandaliwa kisaikolojia kwani CCM inamiliki majukwaa ya kisiasa na vyombo vya habari kwa propaganda za kuwadanganya watanzania kuwa UKUTA unafanya maadamano ya kutetea mafisadi.

Najiuliza wale walioingia mkataba tata na Lugumi wako wapi?
Au leo ndio wanatumia nguvu kuvunja UKUTA ?
Je,hawa ndio waliolifanyia mema na kuwa na nia njema kwa taifa hili?
Wale waliotuhumiwa na gazeti la Dira ya mtanzania kumiliki nyumba za kifahari zaidi ya 40 ndani ya jiji la Dsm wameshakamatwa au ndio hao hao wanaoelekeza makamanda wa polisi wawashughulikie UKUTA?
Je , maagizo ya Rais ya kuwakamata walioagiza makontena feki ya nguo za vijana wetu wameshakamatwa au ndio hao wanaotoa amri za kuwakamata wanaotoa maoni?
Je ,hapa nani anayelinda maslahi mapana na ya siri ya Mafisadi?

Chadema na vyama vingine vyenye nia ya kuleta demokrasia na kujenga uadilifu kwa taifa letu ni lazima wapiganie demokrasia ya kukosoana na kuonyana na hata kuwamulika viongozi wasiofaa.

Najiuliza kuna siri gani imejificha kwa serikali ya Magufuli na Jeshi la polisi kuamua kupambana kwa nguvu zote na wapinzani wanaotekeleza majukumu yao kikatiba?
Kwa nini serikali inapambana kwa nguvu kubwa kwa kutumia mabomu ,bunduki na kila anina ya nguvu kupambana na watu wanaokosoa na kumulika watendaji wasiofaa?
Je, wapinzani wanakusanya wapi kodi au wao ndio walioajiri watumishi hewa.? Kwa nini wakuu wa wilaya wakurugenzi naaafsa utumishi wasiendelee kubanwa kwa kukiuka taratibu za utumishi? Hapa wapinzani kwa nini waumizwa kwa makosa ya makada wa CCM waliyofanya?

Kwa nini waliohujumu taifa hili wasikamatwe?
Kwa nini anasumbuliwa Tundu Lisu ambaye hajawahi kuingia mkataba wowote wa kuuza rasilimali za nchi yetu kwa wanyonyaji?
Kwa nini ubaya wa makada wa CCM uishe kichama chama wakati wamehujumu taifa hili kwa mikatiaba ya kisheria ?

Kwa nini waliokiuka sheria na kujiingiza kwenye ufisadi na uhujumu uchumi wanatumika tena kama silaha ya kuwaangamiza wapenda demokrasia.

Kwa nini wezi,majipu na mafisadi hawapelekwi gerezani badala yake wale wanapigania demokrasia ndio wanaandaliwa na kufunguliwa milango ya magereza?
Kwa nini jeshi la polisi limepolea kwa mikono miwili mapambano dhidi ya wapenda demokrasia kuliko mapambano dhidi ya mafisadi kama akina Lugumi?

Maelekezo aliyotoa Rais kwa Jeshi la polisi ni mengi ikiwemo kuwakamata mafisadi ndani ya Jeshi hilo ambao wapo na wamepoteza mabilioni ya fedha za umma.
Cha ajabu maelekezo yanayotekelezwa kwa haraka ni za wapinzani ambao hawana adhari zozote za kuzuia ukuaji wa uchumi. Wanakamatwa maraoja na kukimbizwa mahakamani bila hata kupata taarifa za kina na za uchunguzi.

Kuna watu wamehujumu tangu Richmond , UDA ,Escrow, Lugumi vyama vya ushirika lakini jeshi la polisi linasuasua kuwakamata pamoja na kuwa Rais alishasema wakamatwe wote. Lakini cha ajabu jeshi hilo hilo linaacha hao wezi kutokana na tu na kujificha nyuma ya vyama vya siasa hasa CCM na kukimbizana kwa mapambanao makali na akina Lisu amabao hawajawahi kuiba hata karatasi ya ofisi ya umma.
Hapa kuna tatizo la kutokujua nani hasa adui wa maendeleo ya taifa letu.

UKUTA sasa ni wakati wa kufanya kila mkakati kwa umahiri, ummakini na tahadhari kubwa ili kuepuka umwagaji wa damu za watu wasio na hatia. Waandaeni watu kwa mapambano ya kifikra kwanza bila kutumia nguvu.
Watu wakikosa maendeleo na wakinyimwa nafasi ya kukosoa na wakichukia kukandamizwa na kuminywa kwa uhuru wao watatoka wenyewe barabarani bila hata kuambiwa. Cha msingi ni kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kuwa na viongozi wanajenga taifa la watu wenye kuvumilia mawazo ya wengine hata kama hawayapendi.

MTU asiyependa mawazo ya wengine hawezi kamwe kukwepa hulka za UDINI, UKABILA, UCHAMA ,RANGI na UJINSIA.
Mtu asiyependa mawazo yanayotofautiana na ya kwake ana hulka ya kupenda vile alivyo navyo tu na si vinginevyo. Lazima atakua na hulka ya kupenda zaidi dini yake na hapendi ikosolewe, atapenda zidi dini yake na dhehebu lake na hapendi likosolewe, atapenda zaidi labila lake na ukanda wake na hapendi aambiwe kitu juu ya kabila lake, atapenda zaidi chama chake na hatataka vyama vingine viwe na ushindani ulo sawa wa kisiasa dhidi ya chama chake. Atapendelea wazi wazi wale wa chama chake hata kama hawana uwezo na maona juu ya taifa hili.

Hapa ndipo mapambana dhidi ya ufisadi yanaposimamia kwenye Udini,ukabila ,uchama na rangi. Utaitwa fisadi na mwizi kwa sababu tu haupo kwenye kundi lake au utaitwa mtu safi kwa sababu tu unatokana na ama dini yake au Kabila lake au chama chake au ukanda wake.

Tukifikia hapa taifa haliwezi kuwa moja.
Tunataka kuona kila mtu anafuata sheria tulizojiwekea.
Kila mtu awajibishwe pale anapokosea na yule asiye na kosa asibambikiwe kosa ili tu kutoa uhalali wa kumshughulikia.

Mtu anafanya mkutano wa siasa au anafanya mahafali matokeo yake anabambikiwa kosa la uchochezi ili tu pawepo na ubalali wa kumshughulikia kinyama.
 
1471095345168.jpg
Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kuonyesha kukaidi katazo la Serikali kuhusu uamuzi wao kuendesha operesheni UKUTA September 1 mwaka huu, ambapo wameanza kusambaza bendera maalum za operesheni hiyo.

Katibu wa CHADEMA kanda ya Pwani, Casimir Mabina amesema kuwa wameamua kugawa bendera hizo kama sehemu ya kuonesha uungwaji mkono wa operesheni ya chama hicho.

Alisema kuwa wafuasi wa chama hicho wanaweza kupeperusha bendera hizo kwenye magari, ofisi Maduka, na hata nyumba zao.
 
Endeleeni kumshika Simba Sharubu zake ...kuna kitu mnataka nyie .
 
Muulize pia Mbowe amefika wapi na aliyemuita fisadi Lowassa.
hadi sasa naanza kuamini kama lowasa ni mtu flan iv cjui nimwitaje maana hakuna thread yenye mambo ya siasa likakosa jina lake hakuna mkutano wa siasa ambao lowasa hatajwii !!
waz ama kwa mafumbo hasa mikutan ya ccm hadi leo cna jibu kamili kua lowasa ana nn ndan yake
 
hadi sasa naanza kuamini kama lowasa ni mtu flan iv cjui nimwitaje maana hakuna thread yenye mambo ya siasa likakosa jina lake hakuna mkutano wa siasa ambao lowasa hatajwii !!
waz ama kwa mafumbo hasa mikutan ya ccm hadi leo cna jibu kamili kua lowasa ana nn ndan yake
Hakuna aliyekukataza kuamini hivyo.
 
Back
Top Bottom