Chadema waendelea kujizolea wanachama wapya.

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

FRIDAY, AUGUST 10, 2012

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbarali.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),kimeendelea kujizolea wanachama wapya baada ya kufanya mkutano wa hadhara Agosti 8 mwaka huu katika Kijiji cha Kongoro Mswisi,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya.

Mkutano huo ulifunguliwa na Mwenyekiti wa chama hicho wilaya Bwana Peter Mwashite wakiwa na nia ya kutoa shukrani kwa wananchi wa kijiji hicho waliokipigia kura chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 wa kuchangua Rais,Wabunge na Madiwani,licha ya kura kutotosha kukiwezesha chama hicho kuibuka na ushindi.

Aidha,katika mkutano huo viongozi kadhaa wa chama hicho walipanda jukwaani na kunadi sera za chama akiwemo aliyewahi kugombea nafasi ya ubunge wa Jimbo la Mbarali Bwana Gidawaya Kazamoyo,Diwani wa viti maalumu Lucy Ngonde,Diwani wa Kata ya Kiwira,Wilaya ya Rungwe Bwana Julius Laurent Mwakalibule,Mwenyekiti wa Vijana mkoa Bwana Julius Kasambala na Bi.Agatha John ambaye ni mwenyekiti wa wanawake Wilaya ya Mbeya Mjini.

Katika mkutano huo kadi za wanachama zaidi ya 74 kutokea Chama Cha Mapinduzi(CCM) walijiunga na chama cha CHADEMA.

Akihutubia mkutano huo Diwani wa Viti Maalumu wa wilaya ya Mbarali Bi, Lucy Ngonde,amesema kuwa zaidi ya bilioni 1.4 pesa za Halmashauri ya wilaya hiyo zimefujwa ba kusababisha miradi ya maendeleo kukwama na kwamba pesa hizo ni tofauti ya shilingi milioni 87 zimefujwa na Mweka Hazina wa halmashauri hiyo.

Wakat huohuo amemtaka Mkurugenzi wa wilaya hiyo kutenga bajeti ya fedha kwa ajili ya chaguzi za vitongoji,ambapo imebainika kuwa baadhi ya vijiji vina makaimu wenyeviti kikiwemo Kijiji cha Mswiswi,kitongoji cha Uswafwani hakina mwenyekiti kwa takribani mwezi mmoja mpaka sasa,Majengo Mapya miaka miwili,Mshikamano miaka mitatu na Maendeleo miaka miwili,hali inayopelekea kuzorota kwa maendeleo wilayani humo.

SOURCE: MBEYA YETU

Inazidi kupunguza ule mtaji wa magamba wa wanachama milioni 5 mpaka 2015 magamba watakuwa na wanachama 200 ambao wote ni familia za mafisadi wanao wafuga
 
Ni ngumu kwa mtanzania masikini mwenye akili timamu kuendelea kuwa ccm. Wanachama zaidi kutoka ccm watahamia upinzani as we go along.
 
Inazidi kupunguza ule mtaji wa magamba wa wanachama milioni 5 mpaka 2015 magamba watakuwa na wanachama 200 ambao wote ni familia za mafisadi wanao wafuga
Nape alikwishaeleza kuwa hata wanachama wakitoka wengine wote akabaki peke yake CCM haitakufa!
 
Nape alikwishaeleza kuwa hata wanachama wakitoka wengine wote akabaki peke yake CCM haitakufa!

aaah! wapi, huyu mnafiki tu. hachelewi kubadilika, wewe hujagundua sasa hivi kaanza kumlamba miguu yule nywele nyeupe EL, wakati juzi alikuwa anamuita fisadi??? kwa kifupi huyu jamaa hana msimamo. NJAA sometimes inamfanya dogo nape anakuwa mropokaji.
 
sie magamba presha inapanda presha inashuka.........mtatuua kwa presha mwaka huu nyie CDM...............
 
Nape alikwishaeleza kuwa hata wanachama wakitoka wengine wote akabaki peke yake CCM haitakufa!

Mkuu Dabudee, katika chama cha Mangamba, namwaminia Nape pekee kwa sababu katika hilo chama dhulumati likifa yeye pekee atabaki nakuifanya ccm iendendelee kuwahai.
 
aaah! wapi, huyu mnafiki tu. hachelewi kubadilika, wewe hujagundua sasa hivi kaanza kumlamba miguu yule nywele nyeupe EL, wakati juzi alikuwa anamuita fisadi??? kwa kifupi huyu jamaa hana msimamo. NJAA sometimes inamfanya dogo nape anakuwa mropokaji.

Nilimwaminia sana huyu dogo, kumbe ni tapeli wa maneno!!!!
 
Nilimwaminia sana huyu dogo, kumbe ni tapeli wa maneno!!!!

pole,wewe mchezaji kapiga chenga 1 tu unamsifia.nape mwenyewe kila siku anahangaika kukarabati mwili na vipodozi hivi unategemea nini?
 
Back
Top Bottom