zomba, Mkuu wangu nitazungumza kama Mkandara na mwanachama kipenzi wa chama cha Upinzani japokuwa mawazo yangu sii lazima yachukuliwe na uongozi wa Chadema.
Swala la Muungano sii swala la kuzungumzwa na Chadema isipokuwa litazungumzwa na wale wenye kero za Muungano wenyewe. Kwa maana kwamba Kama Wazanzibar wanaona kuna ubaya wa kuungana ni jukumu lao wao Wazanzibar kukaa chini na kulizungumza. Wanao viongozi wao toka vyama bunge na hata rais hivyo kama hawaridhiki na muungano ni swala lao wao kulijadili na kisha kwa kupitia viongozi wao ndipo wanaweza kutukaribisha sisi kujadili maamuzi yao. Chademna kama chama ina viongozi na wanachama wake Wazanzibar ambao kwa kuheshimu katiba ya nchi wamekubali kuulinda Muungano. Kama kuna hila yoyote kwanza tuvunje Baraza la Mapinduzi halafu ndipo tunaweza kuwa na mamlaka ya kujadili nafasi ya Zanzibar ktk muungano na jinsi ya kuuboresha..
Haiwezekani kabisa sisi bara tukae kuzungumzia Muungano wakati viongozi wao ndio viongozi ktk serikali ya Muungano na wanafanya kazi pasipo kuonyesha kero hizo isipokuwa wanazizungumzia vijiweni. Kama Dr.Shein anaona kuna kero na Mapungufu ktk Muungano na akawakilisha hoja ya Wazanzibar bado sisi tunaweza kukaa nao tukaijadili. Kama baraza la Mapinduzi limekaa na kuona haja ya Zanzibar kujitenga basi hapo tunaweza kulijadili lakini sii Jumuiya ya kundi la watu ambao wanashindwa kuwauliza viongozi wao, wanashindwa kukaa na viongozi wao kuwakilisha hoja zao lakini wanataka majibu yatoke Bara au serikali ya Jamhuri ya Muungano. Hili haliwezekani..
Na haiwezekani kwa sababu Baraza la Mapinduzi halitaki kuuvunja Muungano maana iikumbukwe ni baraza hili lilofanya Mapinduzi na kuunda serikali ya nchi mpya ya Zanzibar wala sii ile ya Uhuru wa Shamte ilomsimamisha Sultan kama mtawala. Bado kuna vijana wanafikria Zanzibar ya Sultan na uhuru wa Zanzibar ya Sultan kama vile Wazungu wa Zimbabwe wanaofikiria Uhuru wa Ian Smith na Rhodesia. Uhuru ule haupo na ulikufa kutokana na Mapinduzi hivyo ni jukumu la baraza la Mapinduzi kutoa maamuzi.
Kama wananchi wa Zanzibar hawakubaliani na maamuzi ya baraza hili basi wafanya nao Arab spring kuliondoa baraza la mapinduzi maana unaanza kwako kusafisha. Pasipo baraza la Mapinduzi hakuna muungano, huyu ndiye mama wa kuwepo kwa Zanzibar ndani ya Muungano. Nimesema sana ya kwamba hata siku moja mtoto hawezi kudai kuvunja ndoa ya baba na mama yake kwa sababu zake yeye. Wala hawezi kudai sheria ktk ndoa ya mzazi wake isipokuwa ni jukumu la mzazi mmoja kuweka madai hayo wala sii mtoto. Na kibaya zaidi ni ujinga ulioje kwa mtoto kudai kuona cheti cha ndoa cha baba na mama yake ili sijui afahamu kitu gani?..Cheti hakikuzaa wewe, kama una mashaka na wazazi wako kafanye DNA wewe mwenyewe pengine kweli wewe sii mtoto wao yaani sii Mzanzibar..