Chadema uwapi uzalendo wenu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema uwapi uzalendo wenu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Jun 26, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Chadema mmekuwa wakosoaji wazuri wa kero mbalimbali zinazoikabili jamii yetu. Mmekuwa msitari wa mbele katika kupambana na masuala ya ufisadi, hili ni jambo jema lakini msiishie hapo tunatarajia kuwasikia katika masuala mengine pengine muhimu zaidi kuliko hicho mnachokiita "ukombozi" ambayo ni dhana mfu kwani nchi hii ilishajikomboa tangu 1961 na haijatawaliwa tena, what is the essence of your liberation crusade?

  1. Chadema hamsikiki mkihamasisha vijana kufanya kazi badala yake mnawapotezea muda mwingi kwa kuwashirikisha kwenye mikutano na maandamano yasiyo na tija. Hivyo mnachangia tatizo la ajira nchini(disguised unemployment)

  2. Chadema hamjaishauri serikali ipasavyo namna ya kushughulikia kero za madaktari na walimu. Na hamjajitokeza hadharani kushawishi madaktari wasitishe mgomo wakati mazungumzo kati yao na serikali yakiendelea.

  3. Mnachangishana kugharamia mikutano na maandamano kwanini hata maramoja hamjaelekeza hamasa ya michango
  katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo kama ujenzi wa visima au majosho.

  4. Nia yenu njema ya kumhudumia mtanzania iko wapi? ikiwa hamuonyeshi umakini katika mipango na mikakati yenu ya kumnasua mtanzania katika lindi la umasikini(rejea madudu kwenye bajeti ya upinzani).

  5. Ni ipi ajenda yenu ya kiuchumi kwani mikutano na maandamano hayawezi kuwapatia watanzania huduma za afya na elimu, barabara na miundombinu mingine.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mwakidondo umenipa tafakari ya mwaka, keep it up. Ila subiri matusi kama ujuavyo tena magwanda!
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kuna haja gani ya kushughulikia kero nyingine wakati hela zote za maendeleo zinaibwa na mafisadi? suala muhimu ni kuondoa ufisadi kwahiyo hela itakuwepo nyingi ambayo ndio itatumika kwaajili ya maendeleo pambaf
   
 4. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Umechokoza nyuki!!Subiri mashambuliz!
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Matusi gani wezi wakubwa nyinyi hela mmezichimbia huko uswisi halafu mnataka CDM ilete maendeleo bila kutokomeza wizi vip Nyinyi magamba?
   
 6. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sasa CDM wahamasishe vijana wafanye kazi zipi? CDM wafanye shughuli za maendeleo, kwani wao wanakusanya kodi? sisi chadema tutaendelea kuwachangisha watanzania kwa ajili ya kujenga chama, maofisi na pia michango mingine ipelekwe kuandaa mikutano, ili tuwaambie watanzania kwamba CCM Wamekwapua bilion 300, watanzania wanahitaji kujua kodi zao, sasa hapa kosa la cdm liko wapi?
   
 7. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  mwakidondo umepotoka sana!!!! Nakuhakikishia umepotoka!!
  Hivi kwa akili yako mambo yanavyokwenda nchini mwetu emeridhika eh! Kama ndio hivyo basi unakula na mafisadi wewe!.
  > kuhusu hoja kwamba maandamano ya chadema hayana tija inaonyesha wewe ni mwenda wazimu= hivi kama si chadema kuandamana na kupiga kelele unazani leo kungekuwa na mchakato wa katiba mpya. Hivi wasiengaandamana unazani mafisadi wangejulikana na baadhi kuanza kuchukuliwa hatua?!!!
  > eti cdm hawajaishauri ipasavyo serikali hivi kweli unaangalia bunge wewe?
  > eti cdm wanabaki kuandamana bila kuchangia shughuli za maendeleo!! Hivi ulishaenda kwenye majimbo ya chadema wewe?
  > cdm wananania njema sana na ndio maana wanaandamani kupinga ufisadi na kudai mali ya nchi inayotafunwa na mafisadi wa chache! Ndio maana wamepiga kelele na sasa mchakato wa katiba mpya itakayokuwa mkombozi wa mwananchi unaendeleea wakati unajua kuwa ccm hawakutaka katiba mpya kabisa!
  > ajenda za kiuchumi kwa cdm zipo nyingi tu soma katiba ya cdm au muone kiongozi yeyote wa juu wa chadema atakufafanulia. Kwa kifupi kuna ajenda kadhaa ambazo hata mimi naweza kukuambia mathalani
  1. Kusimamia malighafi za nchi
  2. Kupandisha kima cha chini cha mshahara
  3. Kuinua uzalishaji
  4. Kujenga utawala bora
  5. Etc
   
 8. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  M4C inawatesa eh! na bado mtanyoka tu.
   
 9. Dangire

  Dangire JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hivi ukombozi upi ambao tz iliupata? ule wa kuwaondoa wakoloni? naam, hata sasa bado tuna 'wakoloni', tena ni wabaya kuliko hata wale wazungu! 'zimwi hili (ccm) linakukula na kukumaliza kabisa!' hii ni jabu.lazima wakoloni weusi tuwatimue.tunataka ukombozi part II.
   
 10. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Ni kweli. Kwani hata mtumwa hufanyakazi kwa nguvu na bidii kubwa nyumbani kwa bwana wake, lakini haishi kula makombo yadondokayo mezani kwa bwana wake, bidii na jitihada zake ni bure!
  KUFANYAKAZI KWA BIDII HALI KUNA UNYONYAJI NI UTUMWA!
  Lakini tusiache kuhoji, masikini huyuhuyu anaombwa kuchangia M4C, Vx iwekwe mafuta, helkopta iruke angani, services pia, hoja ni kutangaza ukombozi! Hata ukipatikana, masikini hawa watakuwa wameshakufa kwa kunyonywa mara mbili...na ukombozi utakuw hauna mantiki. Hata hivyo...UKOMBOZI HAUJAWAI KUISHI KWENYE BOKSI LA KURA, kwangu huu ni ULAGHAI na WIZI sawa na ule wa ccm!
  Mungu wetu anaita!
   
Loading...