Naunga Mkono Hoja
Bila kujali malengo ya uzi wako, kwanza tumegundua muunganiko wa vyama ni tatizo sana kwa sasa kwani vyama vinaribunika kirahisi na kuishia kuchafua taswira ya chama kingine. Hiyo October wengi hatutashiriki uchaguzi maana tume ya uchaguzi sio huru, hivyo hoja kuwa cdm waungane na cdm ili cdm isife ni hoja mfu. Iwapo cdm itakufa kwa kukosa kura zetu hapo utakuwa na hoja, sio kufa kwa kufanyiwa hujuma.
Cdm na ACT kila mmoja apambane kivyake, sio umoja usio na mwisho mwema. Kitakachofanyika hiyo October unayotishia nayo watu sio uchaguzi, bali ujinga wa mtu mweusi kwenye kusaka madaraka. Wananchi tunajitambua na hatuko tayari kushiriki uhuni wowote uitwao uchaguzi, eti kisa tunaogopa cdm itakufa. Bila tume huru ya uchaguzi hatushiriki uhuni wowote. Waambie ACT wakaungane na NCCR maana wameahidiwa na rais kuhongwa kuwa chama kikuu cha upinzani.
Hapo hatafutwi mwenyekiti mkuu.Wanaweza kukubaliana kila kitu lkn lazima washindane linapokuja suala la uenyekiti
Acha kushawishi watu wasipige kura mkuu, Kupambana ni muhimu kivyovyote vile.
Fahamu hili kuwa haitatokea kamwe CCM kuweka tume huru. Ni kupambana nao tu mpaka kieleweke
ACT ina nguvu mkuu. Kilichopunguza spidi ya ACT ni hili janga la corona ila ni chama ambacho kinakuja juu sanaChombo cha kuzama siku zote huwa hakina usukani!
Watatapatapa mwishowe wataungana hadi na CCM,ACT yenyewe ni Zanzibar tu bara imesimamia mguu mmoja kama jini.
tatizo CHADEMA mkuu. Zitto alishakubali kuungana nao na akiamini mgombea ataoka CHADEMA. Ukiangalia kwa jicho la tatu ZItto kashaona upinzani hauwezi kuisumbua CCM endapo kila chama kitafanya au kusimamisha mgombea wake.Kuungana inawezekana kwenye kumchagua mgombea urais ndo kibembe
CHADEMA waache kiburi, kwa kweli kwa sasa wanaihitaji ACT kuliko wakati wowote.
Hiyo ni past mkuu.Zitto kama akikubali kufanya hivo nitamuona hamnazo kabisa. Kwa jinsi walivyomnanga kipindi kile afu Leo watake kuungana nae tena.?
Zitto usikubali kufanya huo ujinga hao wote walitaka upotee lakini ulipambana kiume sana hadi leo hii heshima imeanza kurudi.