CHADEMA unganeni na ACT Wazalendo

fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,554
2,000
Mpaka sasa kuna idadi kubwa ya Wabunge walioondoka CHADEMA kwa sababu mbalimbali. Lakini ni ukweli ulio wazi kabisa mpaka sasa chama kinadhoofu (Ikumbukwe kuondoka kwa hao wabunge haimaanishi kuwa wanaondoka na wanachama ila inasababisha sintofahamu kwa wanachama).

Unganiko lenu na ACT WAZALENDO ndio suluhu ya kukiokoa chama kisizame. Nina uhakika awamu ya 2020-2025 ndio itakuwa kuchakaa rasmi kwa CHADEMA na kuundwa chama kingine kikuu cha upinzani.

NCCR Mageuzi haiwezi kuwa tishio kwa CHADEMA. Mbatia hana ushawishi katika siasa za Tanzania ukilinganisha na Zitto Kabwe.
Siasa za upinzani zinahitaji muunganiko wa Lissu, Zitto na Maalim Seif. Hawa naweza kusema ndio wanaobeba upinzani kwa sasa. Mbowe ana siasa za matukio (kwenye ukweli tuseme).

Hii "combination" ya ZItto na Lissu ni hatari maana ni watu ambao wanajua kuanzisha hoja na kuisimamia na wana ushawishi mkubwa sana.

Mpaka sasa CHADEMA ishajua wasaliti wao ni akina nani. Zitto hakuwa msaliti na ndio maana hata alipofukuzwa CHADEMA alipoteza ubunge na hakuhamia CCM akaenda kuanzisha chama na huko akapita ubunge tena kwa kuhama jimbo (kitu ambacho Mbatia hawezi; alipigwa mtama na Mdee Kawe akaenda kwa Lyatonga Vunjo-Nguvu ya UKAWA ndio ikamuweka pale alipo). Hawa wengine mliowafukuza uanachama wamerudi CCM moja kwa moja.

Ushauri wangu achaneni na kujiona ndio mnaimarika bali fahamuni ya kuwa chama kinakufa na suluhu ni kuungana na ACT-Wazalendo hata kama hamtachukua dola lakini mtajiongezea idadi ya viti bungeni na hivyo kuipunguza monopoly ya CCM bungeni.

Achaneni na propaganda za kina Yericko wao siku zote wanamuona ZItto ndio adui namba moja wa CHADEMA. Unganeni na ACT mlete upinzani kwa CCM tofauti na hapo hiyo October mtapata wakati mgumu na mnaweza hata msipate wabunge (Sio kwa sababu watapigia kura CCM bali morale ya wanachama wenu itapungua sana na uwezekano wa wanachama wenu kutopiga kura ukawa mkubwa kutokana na kile kinachoendelea sasa).

Nawasilisha!
 
jombi95

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,186
2,000
Zitto kama akikubali kufanya hivo nitamuona hamnazo kabisa. Kwa jinsi walivyomnanga kipindi kile afu Leo watake kuungana nae tena.?
Zitto usikubali kufanya huo ujinga hao wote walitaka upotee lakini ulipambana kiume sana hadi leo hii heshima imeanza kurudi.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
29,083
2,000
Bila kujali malengo ya uzi wako, kwanza tumegundua muunganiko wa vyama ni tatizo sana kwa sasa kwani vyama vinaribunika kirahisi na kuishia kuchafua taswira ya chama kingine. Hiyo October wengi hatutashiriki uchaguzi maana tume ya uchaguzi sio huru, hivyo hoja kuwa cdm waungane na cdm ili cdm isife ni hoja mfu. Iwapo cdm itakufa kwa kukosa kura zetu hapo utakuwa na hoja, sio kufa kwa kufanyiwa hujuma.

Cdm na ACT kila mmoja apambane kivyake, sio umoja usio na mwisho mwema. Kitakachofanyika hiyo October unayotishia nayo watu sio uchaguzi, bali ujinga wa mtu mweusi kwenye kusaka madaraka. Wananchi tunajitambua na hatuko tayari kushiriki uhuni wowote uitwao uchaguzi, eti kisa tunaogopa cdm itakufa. Bila tume huru ya uchaguzi hatushiriki uhuni wowote. Waambie ACT wakaungane na NCCR maana wameahidiwa na rais kuhongwa kuwa chama kikuu cha upinzani.
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
3,213

Acha kushawishi watu wasipige kura mkuu, Kupambana ni muhimu kivyovyote vile.

Fahamu hili kuwa haitatokea kamwe CCM kuweka tume huru. Ni kupambana nao tu mpaka kieleweke
 
fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,554
2,000
Wanaweza kukubaliana kila kitu lkn lazima washindane linapokuja suala la uenyekiti
Hapo hatafutwi mwenyekiti mkuu.
Kinachotafutwa ni muunganiko wa vyama ambao utaleta matokeo mazuri kwa udiwani, ubung e na hata kwenye kura za urais
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
29,083
2,000
Acha kushawishi watu wasipige kura mkuu, Kupambana ni muhimu kivyovyote vile.

Fahamu hili kuwa haitatokea kamwe CCM kuweka tume huru. Ni kupambana nao tu mpaka kieleweke
Mkuu ni wendawazimu kushawishi watu wakapige kura ambazo haziheshimiwi. Hata hivyo nani kakuambia kuwa lazima ccm watoke madarakani kwa njia ya kura? Kwani wao ccm wanategemea njia ya kura kukaa madarakani? Kwa taarifa yako sio kwamba nashawishi, bali wengi wetu tumeshachukua maamuzi kuwa bila tume huru ya uchaguzi hatushiriki huo uhuni. Kama ulitarajia watu kwenda kujazana vituoni ili ccm wajitangaze kushinda kwa kishindo, basi umeumia.
 
fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,554
2,000
Chombo cha kuzama siku zote huwa hakina usukani!

Watatapatapa mwishowe wataungana hadi na CCM,ACT yenyewe ni Zanzibar tu bara imesimamia mguu mmoja kama jini.
ACT ina nguvu mkuu. Kilichopunguza spidi ya ACT ni hili janga la corona ila ni chama ambacho kinakuja juu sana
Na ni chama ambacho kitakuja kuwa tishio sana kwa CCM endapo strategies fulani fulani wakizitumia..
 
fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,554
2,000
Kuungana inawezekana kwenye kumchagua mgombea urais ndo kibembe
tatizo CHADEMA mkuu. Zitto alishakubali kuungana nao na akiamini mgombea ataoka CHADEMA. Ukiangalia kwa jicho la tatu ZItto kashaona upinzani hauwezi kuisumbua CCM endapo kila chama kitafanya au kusimamisha mgombea wake.
Shida ipo CHADEMA wao wanaamini wanaimarika sasa huku wabunge wakiwakimbia wasichokijua wanawakatisha tamaa waoiga kura wao ilihali wale wa ccm wapo vile vile (other factors held constant).
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
29,083
2,000
CHADEMA waache kiburi, kwa kweli kwa sasa wanaihitaji ACT kuliko wakati wowote.
Kwanini cdm waungane na ACT? Kwanini msishauri ACT waungane na vyama vingine? Huo muungano sio ndio waliungana na kina NCCR na CUF, je ni kipi kinaendelea hadi sasa? Hakuna cha muungano wala nini, kila chama kipambane kivyake hata kikipata kura moja poa tu.
 
fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,554
2,000
Zitto kama akikubali kufanya hivo nitamuona hamnazo kabisa. Kwa jinsi walivyomnanga kipindi kile afu Leo watake kuungana nae tena.?
Zitto usikubali kufanya huo ujinga hao wote walitaka upotee lakini ulipambana kiume sana hadi leo hii heshima imeanza kurudi.
Hiyo ni past mkuu.
Kwenye siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu. Win Win Situation ndio inayoangaliwa katika siasa
 
Top Bottom