fdizzle
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 1,891
- 2,367
Mpaka sasa kuna idadi kubwa ya Wabunge walioondoka CHADEMA kwa sababu mbalimbali. Lakini ni ukweli ulio wazi kabisa mpaka sasa chama kinadhoofu (Ikumbukwe kuondoka kwa hao wabunge haimaanishi kuwa wanaondoka na wanachama ila inasababisha sintofahamu kwa wanachama).
Unganiko lenu na ACT WAZALENDO ndio suluhu ya kukiokoa chama kisizame. Nina uhakika awamu ya 2020-2025 ndio itakuwa kuchakaa rasmi kwa CHADEMA na kuundwa chama kingine kikuu cha upinzani.
NCCR Mageuzi haiwezi kuwa tishio kwa CHADEMA. Mbatia hana ushawishi katika siasa za Tanzania ukilinganisha na Zitto Kabwe.
Siasa za upinzani zinahitaji muunganiko wa Lissu, Zitto na Maalim Seif. Hawa naweza kusema ndio wanaobeba upinzani kwa sasa. Mbowe ana siasa za matukio (kwenye ukweli tuseme).
Hii "combination" ya ZItto na Lissu ni hatari maana ni watu ambao wanajua kuanzisha hoja na kuisimamia na wana ushawishi mkubwa sana.
Mpaka sasa CHADEMA ishajua wasaliti wao ni akina nani. Zitto hakuwa msaliti na ndio maana hata alipofukuzwa CHADEMA alipoteza ubunge na hakuhamia CCM akaenda kuanzisha chama na huko akapita ubunge tena kwa kuhama jimbo (kitu ambacho Mbatia hawezi; alipigwa mtama na Mdee Kawe akaenda kwa Lyatonga Vunjo-Nguvu ya UKAWA ndio ikamuweka pale alipo). Hawa wengine mliowafukuza uanachama wamerudi CCM moja kwa moja.
Ushauri wangu achaneni na kujiona ndio mnaimarika bali fahamuni ya kuwa chama kinakufa na suluhu ni kuungana na ACT-Wazalendo hata kama hamtachukua dola lakini mtajiongezea idadi ya viti bungeni na hivyo kuipunguza monopoly ya CCM bungeni.
Achaneni na propaganda za kina Yericko wao siku zote wanamuona ZItto ndio adui namba moja wa CHADEMA. Unganeni na ACT mlete upinzani kwa CCM tofauti na hapo hiyo October mtapata wakati mgumu na mnaweza hata msipate wabunge (Sio kwa sababu watapigia kura CCM bali morale ya wanachama wenu itapungua sana na uwezekano wa wanachama wenu kutopiga kura ukawa mkubwa kutokana na kile kinachoendelea sasa).
Nawasilisha!