CHADEMA- umulikeni mkoa wa Tabora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA- umulikeni mkoa wa Tabora

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpevu, Feb 28, 2011.

 1. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  HESHIMA KWENU WADAU WOTE,

  TABORA;
  SI VIBAYA UKIITA... 'TAA BORA'
  Ni mkoa ulio nyuma kimaendeleo,
  Watu wake wamejikatia tamaa kuutegemea utawala,
  Mkoa umemezwa na CCM,
  Ni mkoa uliobeba utaifa na harakati zote za Tanganyika,
  Ni mkoa uliojaaliwa ardhi nzuri yenye rutuba na misitu mizito ya asili,
  Ni mkoa uliotoa wasomi wengi kulitumikia taifa hili,
  Ni mkoa uliotelekezwa na watawala kwa miongo yote hiyo,
  Ni mkoa unaotegema mabwawa ya Igombe na Kazima kutupatia maji,
  Zao la tumbaku ni kitovu kikuu cha uchumi na fedha za kigeni kwa taifa hili,
  Ni mkoa usio na mawasiliano ya kiuhakika ya barabara,
  Ni mkoa ikiwa jitihada zikifanyika za mageuzi ya kisiasa...VYAMA VITAJIVUNIA,
  Ni mkoa ambao watu wake bado wana elements za chama kimoja kitukufu CCM,
  Ni mkoa ambao mwenyekiti wa CUF amezaliwa lakini hakubaliki,
  Ni mkoa unaoweza kutekwa na CHADEMA iwapo wataliona na kulihitaji hilo.
  Tunakihitaji CHADEMA, tunahitaji mabadiliko,
  Enyi wakuu wa CHADEMA, mmesahau asili ya aliposomea baba wa taifa? Basi na muurejee mkoa huo, iwapo juzi mmetoka Butiama basi fikeni pale na mkutano ufanyike CHIPUKIZI SQUARE.

  NAAM...huu ndio mkoa wa Tabora, mkoa wenye kitovu cha HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA. Wapi kama Tabora?

  Nawasilisha,
   
 2. magessa78

  magessa78 JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tunafika huko kote.usihofu
   
 3. c

  carefree JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Cuf hamkuwakubali kwa nini? Na nini kitakachowafanya muikubali chadema?
   
 4. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Seriousness on issues,
   
 5. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Kwa nyongeza tu ni kwamba mie natoka TARAFA moja na mh.Lipumba, yeye yupo tarafani (Ilolangulu)nasi tupo kwenye kata (Ibiri) si mbali saana toka Ndono/Mbiti/Mabama ni takriban km 20 vile. Tunapaza mbiu ili jambo lijongee...
   
 6. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naunga mkono hoja, mwaka 1995 tabora ilikuwa mkoa machachari uliounga mkono sana NCCR mageuzi. Na ndo maana waliweza mchangua mbunge wa nccr mageuzi jimbo ya URAMBO mashariki Mhe. MSINA kipindi hicho na kumuangusha Mhe. SIttta. Lakini baada ya magomvi ya marando na mrema, wananchi waliupoteza moto wa mageuzi na kupoa kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!! Hivyo inahitajika mbiu mpya na moto mpya kwa sasa hususan wa CHADEMA kusimika chama hicho katika wilaya na matawi yote. Naamini CDM mtakubalika na mkifanya vema mtateka TBR na kuunganisha na mkoa wa KIGOMA vema. Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  sauti zipazwe zaidi! pamoja twaweza
   
 8. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni kweli nakumbuka Mhe. MSINA aliwahi kumbwaga aliyekuwa Spika wa Bunge la 9 mwaka 1995 huko urambo. Lakini kitu muhimu hapa kujiuliza ni ile hali ya Wa-tabora kuwa wanyamazifu kama watu waliomwagiwa maji ya baridi. Je, ni kutokana na magomvi baina ya Marando na Mrema au kipo kitu kingine kilichowafumba akili, midomo na vitendo? Iko haja sasa ya kubaini sababu halisi ili CDM iweze kuuteka TABORA kama inavyo fanya kwingineko. Hawa jamaaaa CDM nawaaminia na kuwapa bigup kwa saaaaaaaaana.
   
 9. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Tabora wamekata tamaa kabisa, hasa vijana.. Kinachochangia kudumaa ni hali mbaya ya miundombinu ya mkuo wa Tabora, pamekua kama kisiwa, wananchi wake hawana uwezo wa kwenda mkoa mwingine kwa urahisi, barabara kuu zote hazina lami..
  Pia hali ya maji ni mbaya sana.. Hata wakazi wa mijini wanatumia maji machafu kwa matumizi ya kila siku..
  Pia vyanzo vya ajira mkoani hapo ni haba, kwani hakuna kiwanda hata kimoja, ukiondoa nyuzi kilichokufa...
  Mawasiliamo ya redio na tv pia ni haba, kwani wanasikiliza tbc, rfa, vot, na cg fm, zote zinatoa fever kwa CCM, pia tv inayopatikana hapo ni tbc tu..
  Magazeti yanafika baada ya siku mbili..
  Vijana wamejiajiri kwa kuendesha baiskeli na pikipiki...
  Upande wa elimu, mkoa upo nyuma sanaa.. Vijana wengi wanaishia darasa la saba, na sasa kata...
  Upande wa utamaduni, mkoa wa tabora umetekwa sana na mwarabu, tangu enzi za utumwa, na dini yenye watu weng ni uislamu..
  Wananchi wake wanaamini sana ushirikina ili kuleta utajiri..
  Me kama mkazi wa Tabora ninasisitiza pia Chadema waje na operation Sangara ya tarafa kwa tarafa..
  Namkumbuka kwenye kampeni za mwaka jana, Dr Slaa alichelewa sana kuanza kampeni, na wananchi wengi wakazira na kuondoka, nakumbuka alifika mkutanoni saa 12:40 za jioni na akamwaga sera haraka haraka, bila watu kumwelewa..
  KARIBUNI CHADEMA MKOANI KWETU TABORA vijana tunataka mabadiliko..
   
 10. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Twaja muda c mrefu na mambo yote yatabadilika. Hatuogopi ushirikana wao mungu ndo nguvu ya chadema. Na tutawasambaza wazee wote hao wanaoshinda wana cheza bao nakunywa kahawa vivulini na kupika majungu, na hao ndo wanaurudisha nyuma mji wa Tabora, inasikitisha Mkoa kuzidiwa na wilaya zake.
   
 11. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu heshima kwako,
  Kweli wewe ni mwenyeji wa TBR, yote uliyoyatoa ni sahihi kabisa. Kiukweli kunahitajika mageuzi, nakumbuka mwaka 1995 Dr. Mrema akiambatana na Masumbuko Lamwai waliiteka Tabora kwa mkutano wao uliofanyika pale viwanja vya shule ya sekondari Kazima, mji ulichangamka haswaaaa na kumpata mbunge wa upinzani kwa kumuangusha mzee SIX ambaye wakati huo alikuwa ni waziri wa sheria.
  Shime wadau, tuungane kuupigania mkoa huu ili kujiwekea himaya nzuri ya kimageuzi.
  SHIME.
   
 12. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Safi kabisa,
   
 13. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Chadema songa mbele, tunahitaji mabidiliko ya kweli tanganyika yoote, kama mmefika shinyanga naamini hata tabora mtafika tu, kaza buti taifa linawahitaji
   
 14. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Redio na TV hizi wakati wa mgao tunakaka kimya kabisa. Hamna haja ya kuwa na redio za betri
   
Loading...