CHADEMA/UKAWA wamehaha

CHADEMA/UKAWA wamehaha

Huwezi ukalinganisha CHADEMA na vyama uchwara. CHADEMA ni chama imara ila sasa kinafanya mambo ambayo yatakifanya kibaki jina na kuingia kwenye kundi la CHAUMA, ACT, NCCR n.k. Tanzania inahitaji vyama imara ili tuweze kusonga mbele. Kwa sasa CHADEMA inapoteza mwelekeo.

Chadema kupoteza mwelekeo, wewe utapungukiwa nini? Hata hivyo kupoteza mwelekeo hutokea kwa mtu au chama chochote. Huwezi siku zote ukawa imara. Inafikia kipindi hata wewe unayumba kwa kukosa fedha za matumizi sembuse chama makini chadema?
 
Na kosa namba moja lilikuwa ni kumpokea Lowassa na kumfanya mgombea urais. Hapo mwelekeo wa CHADEMA, chama makini, ndipo ulianza kuyumba..
 
CHADEMA na vyama washirika wanaounda UKAWA wamejikuta kwenye wakati mgumu wa kukosa ajenda baada ya Rais John Pombe Magufuli kuanza kutekeleza ahadi ambazo alizitoa kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015. CHADEMA na vyama washirika wamekuwa wakipeta sana kwa kuibua madudu ya CCM kama rushwa na ufisadi, uzembe serikalini, uongozi mbovu, ahadi zisizotekelezeka na mambo mengi ya ovyo yalikuwa yakitendeka serikalini. Rais Magufuli kwa kiasi flani ameweza kuwashughulikia baadhi ya wala rushwa na mafisadi na kuwatumbua watumishi hewa na kusimamia serikali yake namna ambayo Watanzania hatujawahi kushuhudia kwenye awamu ya 2,3 na 4.

Ni kweli kwamba mambo ambayo yalikipa CHADEMA sifa ni kukemea rushwa na ufisadi serikalini, uongozi mbovu, ahadi hewa za CCM na kushindwa kwa serikali ya CCM kuzitumia vyema rasmali za nchi kwa manufaa ya Watanzania. Mambo haya kwa sasa ndiyo anayoyashughulikia rais Magufuli. Usugu wa matatizo haya umepungua na kuyafanya yasiwe "hot news" kisiasa na CHADEMA kushindwa kuyatumia matatizo haya kama ajenda kwenye mijadala yao. Hivyo CHADEMA/UKAWA wamejikuta hawana ajenda ya kuwafanya wasikike magazetini, redioni, TV na vijiweni.

Vipi kuhusu udikteta? CHADEMA/UKAWA walikuwa wakimnadi Mhe Lowassa kama kiongozi ambaye ataipeleka Tanzania mchakamchaka na kuondoa uzembe serikalini na kuwatumikia watanzania, kukuza uchumi na kuondoa umaskini Tanzania. Kwa tafsiri yangu mchakamchaka ni kutovumilia mambo ya ovyo kama uzembe, wafanyakazi hewa, shule bila madawati, kipindupindu, maandamano yasiyokuwa na tija, rushwa na ufisadi, kutotekeleza ahadi za serikali, ukwepaji kodi, uporaji ardhi, serikali kubaki Dar japo makao makuu yake ni Dodoma na mambo mengine mengi. Sasa inakuwaje CHADEMA wanalalamika pale ambapo Rais Magufuli anaipeleka Tanzania mchakamchaka?

RAI YANGU KWA CHADEMA: Inapaswa CHADEMA na vyama washirika wa UKAWA wajitathmini na kujipanga upya. Kama chama cha upinzani misingi yake ni ipi? Ni matatizo yapi yanaikabili Tanzania na wana njia zipi mbadala za kuyatatua matatizo haya? Ili chama kiendelee kubaki hai na kisikike (kisiwe 'dormant') je ni hoja zipi zenye mashiko zitumiwe kuikosoa serikali?
Uharo tu nilipoona tittle nikajua tu ni walewale stomach seekers and thinkers,haya kadake buku 3/7 baada ya kupoteza muda wako mkidanganywa hapa kazi tu nayo hiyo ni kazi au utumbo.
Usidai hata nyongeza endeleeni kuwa watumwa wa matumbo,go to the hell.
 
Kwa hiyo kwa uelewa wako unaona natetea riziki yangu? Tatizo kubwa la baadhi ya wanachama wa CHADEMA ni kupinga hata kile kisichopingika. Hivi inakuingia akilini pale ambapo mtu anakerwa na hatua anazozichukua JPM kuhakikisha kwamba kodi stahiki inalipwa serikalini? Wewe binafsi unauonaje utendaji wa JPM?
Anachofanya kila mtu anaweza kufanya,
 
Wajitathmini how wakati hata hamtaki wasikike popote bungeni, mikutatano mnaifanyia mizengwe, hata vyombo vya habari haziruhusiwi kutoa hoja zao labda kidogo magazeti.
Sasa hapo ulitaka wafanyeje ?! Wafanye fujo ndio ujue wana hoja ?!

Tumia hekima kabla ya kutoa hoja
Kwani kuna mtu aliwaambia wazibe midomo na karatasi?
 
Kama utawala wa awamu ya tano ungekuwa ni wa kidikteta huyo Lisu angeachiwa leo kwa dhamana? Hawa Chadema wanafahamu maana halisi ya udikteta?
 
Chadema wamejichanganya inakuhusu nini. Kuwa na uwezo mdogo ni kujipambanua kama ulivyofanyia wewe. Ni wewe huyohuyo unayehangaika na mambo ya Lowasa yaliyotokea miaka kumi iliyopita unaacha Escrow ya mwaka jana tu. Ujinga gani huo. Usisahau sisi wote ni wanadamu na ni watanzania jambo baya linatuhusu wote na jambo jema linatuhusu pia.
 
Na kosa namba moja lilikuwa ni kumpokea Lowassa na kumfanya mgombea urais. Hapo mwelekeo wa CHADEMA, chama makini, ndipo ulianza kuyumba..

Lowasa asipokelewe yeye siyo binadamu? au ulitaka nani apokelewe ili ulidhike? Mawazo mengine bhana!
 
Siasa ni dynamic na wakati fulani ufumbuzi wa tatizo moja huzalisha tatizo jingine, usijifungie ndani ya box,
hujajibu hoja. hapo cdm ndio imebaki kwenye box baada ya jpm kuwa preempty
 
Mtoa mada nimeona nisikuache hivihivi coz naona una uhelewa hafifu sana ni hivi hayo yote anayofanya JPM ni matunda ya kuwepo upinzani kwahivo basi ili nchi iendelee tunahitaji wapinzani wenye nguvu pengine kuliko CHADEMA
hivi nyie watu wa siku hizi mnasoma shule gani. 'uhelewa' ndio nini?
 
Kuna wapiga deal za
SUKARI TOKA NJE
MISHAHARA HEWA
MAKONTENA BANDARINI
VYETI FEKI
VYUO FEKI
WAFANYAKAZI HEWA
WAPAMBE WA LOWASA
WAKWEPA KODI, walikuwa wananufaika Sasa mambo Hayo hayapo, wanachofanya Ni kuhakikisha kuwa JPM anaonekana hafai kwa sababu ambazo hazina miguu wala kuchws
 
CHADEMA na vyama washirika wanaounda UKAWA wamejikuta kwenye wakati mgumu wa kukosa ajenda baada ya Rais John Pombe Magufuli kuanza kutekeleza ahadi ambazo alizitoa kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015. CHADEMA na vyama washirika wamekuwa wakipeta sana kwa kuibua madudu ya CCM kama rushwa na ufisadi, uzembe serikalini, uongozi mbovu, ahadi zisizotekelezeka na mambo mengi ya ovyo yalikuwa yakitendeka serikalini. Rais Magufuli kwa kiasi flani ameweza kuwashughulikia baadhi ya wala rushwa na mafisadi na kuwatumbua watumishi hewa na kusimamia serikali yake namna ambayo Watanzania hatujawahi kushuhudia kwenye awamu ya 2,3 na 4.

Ni kweli kwamba mambo ambayo yalikipa CHADEMA sifa ni kukemea rushwa na ufisadi serikalini, uongozi mbovu, ahadi hewa za CCM na kushindwa kwa serikali ya CCM kuzitumia vyema rasmali za nchi kwa manufaa ya Watanzania. Mambo haya kwa sasa ndiyo anayoyashughulikia rais Magufuli. Usugu wa matatizo haya umepungua na kuyafanya yasiwe "hot news" kisiasa na CHADEMA kushindwa kuyatumia matatizo haya kama ajenda kwenye mijadala yao. Hivyo CHADEMA/UKAWA wamejikuta hawana ajenda ya kuwafanya wasikike magazetini, redioni, TV na vijiweni.

Vipi kuhusu udikteta? CHADEMA/UKAWA walikuwa wakimnadi Mhe Lowassa kama kiongozi ambaye ataipeleka Tanzania mchakamchaka na kuondoa uzembe serikalini na kuwatumikia watanzania, kukuza uchumi na kuondoa umaskini Tanzania. Kwa tafsiri yangu mchakamchaka ni kutovumilia mambo ya ovyo kama uzembe, wafanyakazi hewa, shule bila madawati, kipindupindu, maandamano yasiyokuwa na tija, rushwa na ufisadi, kutotekeleza ahadi za serikali, ukwepaji kodi, uporaji ardhi, serikali kubaki Dar japo makao makuu yake ni Dodoma na mambo mengine mengi. Sasa inakuwaje CHADEMA wanalalamika pale ambapo Rais Magufuli anaipeleka Tanzania mchakamchaka?

RAI YANGU KWA CHADEMA: Inapaswa CHADEMA na vyama washirika wa UKAWA wajitathmini na kujipanga upya. Kama chama cha upinzani misingi yake ni ipi? Ni matatizo yapi yanaikabili Tanzania na wana njia zipi mbadala za kuyatatua matatizo haya? Ili chama kiendelee kubaki hai na kisikike (kisiwe 'dormant') je ni hoja zipi zenye mashiko zitumiwe kuikosoa serikali?
Hivi wao zile ahadi walizoahidi wanatekeleza ama ndo wanazitathimini za rais tu? watakuja kujuta mda na saa vikitaraji
 
Back
Top Bottom