Na kwa hili tunasema, hata kama watu hawakubaliani , wapinzani wana namna mbili, kufanya biashara ya ‘reja reja au jumla'Kwa Upande wa Mhe. Edward Lowassa
1. Mheshima Lowassa atambue na kukubali hadharani (publicly) makossa ambayo aliyafanya kama kiongozi na akiangalia leo kwa mwanga wa umbali wa historia aombe radhi taifa kwa sehemu yake na kuwa yuko tayari kujenga iman na kuahidi hayatotokea tena chini ya uongozi wake.
Ni lazima aoneshe unyenyekevu wa kukubali nafasi yake na makosa yoyote ambayo yalifanyika wakati wake kama kiongozi mkuu wa Serikali; haitoshi tena kutupa lawama kwa watu wengine.
Itakuwa hatua ya kwanza kuanza kuaminiana;
2. Alaani waziwazi na hadharani vitendo vya serikali kuminya upinzani na kuomba radhi kwa ukimya wake wakati wapinzani wananyanyaswa na vyombo vya dola umeacha doa kubwa sana la kuweza kumwamini;
Ahadi nyingine ambazo tungependa azitamke hadharani na tujue kuwa zitakuwa ni sehemu ya ahadi zake kama Mgombea wa Urais kupitia CDM.
Mgombea wa Urais anayebeba matamanio na ahadi za vyama vya upinzani ni lazima asimamie mambo yale ambayo Upinzani Tanzania umesimamia miaka hii yote.
Litakuwa ni kosa kubwa na usaliti wa harakati za upinzani nchini kwa mgombea wake wa Urais kutosimamia wazi, hadharani na bila utata hoja kuu za upinzani nchini.
Kwa vile Lowassa ndiye ambaye CDM na vyama washirika wamekubaliana ni muhimu na lazima kutangaza hadharani kuwa atasimamia mambo yafuatayo ambayo tayari yamepaziwa sauti na CDM na vyama vingine hasa ndani ya miaka hii mitano.Atakaposhika Madaraka ya Rais;
1. Tungependa aikane Katiba ile na kuahidi atanzisha mchakato sahihi, bora, wa wazi, na utakaokidhi matarajio ya Watanzania kuhusiana na Katiba Mpya.
Mchakato huu ujao utahakikisha baadhi ya mambo yanaamuliwa kwanza kabisa kabla ya kura ya maoni
2. Ataanzisha uchunguzi wa Kimahakama (Judicial Inquiries) ya matukio ya mauaji ambayo yametokea katika mazingira ya kisiasa – wakati uliopita na wakati huu wa kampeni za Uchaguzi - ili kuhakikisha ukweli unajulikana na sheria inafuata mkondo wake kwa wahusika;
3. Serikali yake italeta miswada ya mabadiliko ya Sheria mbalimbali au miswada ya sheria mpya ambazo zimekuwa ni tatizo kwa taifa kwa miaka hii yote.
Miswada hii italetwa katika kikao cha mapema zaidi baada ya Bunge Jipya kuapishwa. Baadhi ya Sheria ambazo miswada yake itatakiwa kuletwa mara moja ili kuliondoa taifa na masalio ya sheria mbovu za utawala wa CCM na ambayo Lowassa ataahidi hadharani na wakati wa kampeni italetwa mapema ni ile inayohusu:
- Mabadiliko ya Sheria ya Usalama wa Taifa ya 1996
- Mabadiliko ya Sheria ya Usalama wa Mitandao ya 2015
- Sheria ya Uhuru wa Habari na Ulinzi wa Wafichua Maovu (Whistleblower Protection ACT)
- Mabadiliko ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa ya 2007
- Mabadiliko ya Sheria ya Jeshi la Polisi ya 2007
- Kupitia Sheria zile au Vipengele 40 ambavyo vilioneshwa na Tume ya Jaji Kisanga kuwa vinahitaji mabadiliko.
Ndani ya Mwaka mmoja hili liwe limetimizwa ili kuondoa Sheria zote zilizopitwa na wakati vitabuni
- Na sheria nyingine ambazo zinaonekana ni kikwazo katika kutengenza utawala bora
Endapo haya yatafanyika mapema kuelekea kampeni, na tukaona kuwa kweli hawazungumzi tu bali wako tayari kutenda basi hata sisi wengine ambao tunasita kutoa mkono wetu wa pongezi au kudandia treni la Lowassa tutakuwa tayari kuwaunga mkono na kufanya kila jitihada kuhakikisha kuwa Lowassa anachaguliwa kuwa Rais kwani atakuwa ametujengea imani kidogo na viongozi wa CDM nao watakuwa wametupa mwanga kuwa kweli wanaamini katika hii "nafasi ya pekee".
Kinyume cha hapo wengine bado tuna mioyo ya kusita sita. Hatujaona sababu au vitendo vya kutuaminisha kuwa pande hizi mbili kwel zinaamini katika kuiondoa CCM madarakani mwaka huu. Kama kweli wanaamini basi ramani ya kuunganisha fikra za wapinzani ndiyo hii.
Umoja wa Kweli Ndio Ushindi wa Kweli
MBINU NA CHANGAMOTO ZA CHAGUZI
Chaguzi huambatana na mbinu , mikakati na changamoto
Chaguzi huwa na makundi ya wapiga kura. Kwa hali ya kisiasa yapomakundi yafuatayo
(1) Kundi linalopiga kura ya hasira- hili ni lile lisilo naupande, lilichoshwa na hali iliyopo
(2)Kundi la wanachama watiifu, hili linachagua tu kutokanana vyama iwe ni CCM, UKAWA au kingine
(3) Kundi lenye mashaka- hili halina uhakika lisimame wapi namara nyingi huangalia hoja ingawa si jambo linalotazamwa sana ukilinganisha na personality
CCM inategemea makundi 2 na 3 kwasababu tayari ni mwathirika wa kundi la 1
Wapinzani wana ‘advantage' ya makundi yote. Ushindani upo kundi la 3 litakaloamua nani anashinda majimbo au dola
Wapinzani kama ilivyo kwa CCM, wana ‘disadvantage'.
Kwanza, uwezowa kufikia jamii una vikwazo tukijua CCM ina mtandao wa wakuu wa mikoa na wilaya na rasilimali za umma.
Pili,CCM wanaserikali inayomiliki vyombo muhimu.
Mfano, zipo taasisi za nishati zinazolalamikiwa kutotenda haki kwa maagizo ya serikali ili kuwanyima wananchi habari
Vyombo vya habari vinavyoegemea CCM, na vyombo vya dola kutumika vibaya
Ushindi hautaamuliwa kwa hesabu za kura, yapo mengine ambayo kama hayataangaliwa yatabadili mwenendo wa uchaguzi
Kwa mfano,hatujawahi kupata majibu ya kwanini watu wajiandikishe kwa asilimia 70 , wapiga kura wawe asilimia 30.
Kuna nini kinaendelea ambacho serikali au tume ya uchaguzi imeshindwa kubaini?
Mfumo wa pili , BVR, je, umehakikiwa kufanya kazi kamailivyokusudiwa?
Kukiwa na matatizo ya kifundi au ‘kufundwa' itakuwa ni kwa maumivu ya wapinzani
Lipo suala la ‘voters suppression' kusudio ni kuzuia watu wasitumie haki ya kura kwa udanganyifu kama ule wa 1995 watu walipoambiwa siku ya kwanza ni CCM na ya pili wapinzani
Au inaweza kuwa vitisho kwa wapiga kura (2010) kwa jeshi kutoa tamko, au kutumika nguvu za dola kwa namna yoyote.
CCM wanakiri hali ngumu inayowakabili. Istegemewe CCM itatoa dola au bunge au vyote katika kisahani cha dhahabu.
Itapigana hadi tone la mwisho ikitambua kuwa KANU imetoweka kama ilivyo UNIP
Kitakachosaidia wapinzani ni ushindi usio na shaka ‘decisive victory'.
Itawezekana wakijiweka vema kupambana na hila, kukabiliana na hoja, kujenga hoja na kujibu hoja.
Kuzuia uharibifu kwakushambulia na si kujilinda ni muhimu kwao.
Kuwepo na uthubutu ‘courage' ya kupambana na changamoto si chaguo ni lazima kwa wapinzani
Tusemezane
Kama kuna kitu ambacho upinzani unapaswa kukipigania kufa na kupona ni kuhakikisha wote waliojiandikisha kupiga kura wanajitokeza tarehe 25 na wanapiga kura bila mizengwe yoyote. Ushindi wa 62% alioupata JK mwaka 2010 huku voters turnout ikiwa ni 42% pekee inatoa ujumbe kwamba endapo turnout ingekuwa 70% au hata 80% pengine tungekuwa tunaongea lugha nyingine sasa hivi!
Na hili wanapaswa kulisimamia kwa umakini sana hususani sasa tunapotumia huu mfumo wa BVR! Kwa matukio yaliyoripotiwa hivi karibuni ya baadhi ya viongozi kukamatwa wakikusanya kadi za kupigia kura kutoka kwa wananchi na kuzinakili namba ni dalili mbaya juu ya mambo yatakayotokea tarehe 25.
Hili la BVR ni muhimu sanaKama kuna kitu ambacho upinzani unapaswa kukipigania kufa na kupona ni kuhakikisha wote waliojiandikisha kupiga kura wanajitokeza tarehe 25 na wanapiga kura bila mizengwe yoyote. Ushindi wa 62% alioupata JK mwaka 2010 huku voters turnout ikiwa ni 42% pekee inatoa ujumbe kwamba endapo turnout ingekuwa 70% au hata 80% pengine tungekuwa tunaongea lugha nyingine sasa hivi!
Na hili wanapaswa kulisimamia kwa umakini sana hususani sasa tunapotumia huu mfumo wa BVR! Kwa matukio yaliyoripotiwa hivi karibuni ya baadhi ya viongozi kukamatwa wakikusanya kadi za kupigia kura kutoka kwa wananchi na kuzinakili namba ni dalili mbaya juu ya mambo yatakayotokea tarehe 25.
The Intelligent, sijui unafuatilia kwa ukaribu kiasi gani takwimu zinazotolewa wakati wa Uchaguzi Mkuu na mwitikio wa wananchi kila baada ya miaka mitano. Ukweli ni kwamba idadi ya wanaojiandikisha kupiga kura imekuwa ikiongezeka kila uchaguzi ila yaliyotokea mwaka 2010 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaweza kutolewa ni kweli yalizua maswali kuliko majibu. Ni mwaka huo pekee ambapo idadi ya wapiga wanaodaiwa kujitokeza ilikuwa asilimia chini ya hamsini ya idadi ya waliojiandikisha tofauti kabisa na miaka ya nyuma. Hebu tafakari hili jedwali hapa chini;Hili la kuhakikisha watu wote waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ni gumu kutokana na mfumo wa uchumi,kijamii na kusiasa ulipo Tanzania na mwamko mdogo wa kisiasa kwa watanzania walio wengi.
Wakati wa mchakato wa uandikishaji wa vitambulisho vya kupigia kura niliwahi kufanya uchunguzi wangu mdogo kubaini ni kwanini mwaka awamu hii watu waliojitokeza ni wengi kuliko 2010, wengi walionekana kuhitaji vitambulisho tu kwa kuwa vinatolewa bure na mfumo mpya wa kutumia mashine(BVR) umechangia kuongezeka kwa idadi ya watu wakitaka kuona tofauti ya sasa na kipindi kilichopita, hii inaweza kuonekana kama ni kushangaa tu kama ilivyo hulka ya walio wengi wetu huku wengine wakisema wanavihitaji kwa ajili ya shughuli ndogo ndogo kama usajiri wa laini za simu na kupata dhamana kwenye taasisi za fedha nk.
Nikiangalia kwenye mfumo wetu wa kimaisha/kiuchumi ni kwamba mtu hawezi kuacha shughuli yake ambayo ndio inamuingizia kipato cha kulisha familia na kwenda kupanga foleni kwa ajili ya kitu kisicho na faida ya siku hiyo na matokeo yanayoweza kupimika kwa wakati huo, pia ikumbukwe kuwa watanzania walio wengi wanafanya kazi binafsi ambazo kama hawatafanya basi siku itakuwa imeenda vibaya...
...Hayo mambo niliyoyataja yanaweza kuonekana sio muhimu ila ndio yanayochangia ushiriki wa wananchi kwenye kupiga kura kuwa hafifu.
The Intelligent, sijui unafuatilia kwa ukaribu kiasi gani takwimu zinazotolewa wakati wa Uchaguzi Mkuu na mwitikio wa wananchi kila baada ya miaka mitano. Ukweli ni kwamba idadi ya wanaojiandikisha kupiga kura imekuwa ikiongezeka kila uchaguzi ila yaliyotokea mwaka 2010 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaweza kutolewa ni kweli yalizua maswali kuliko majibu. Ni mwaka huo pekee ambapo idadi ya wapiga wanaodaiwa kujitokeza ilikuwa asilimia chini ya hamsini ya idadi ya waliojiandikisha tofauti kabisa na miaka ya nyuma. Hebu tafakari hili jedwali hapa chini;
[TABLE="class: cms_table"]
[TR]
[TD="align: center"]Mwaka[/TD]
[TD="align: center"]Waliojiandikisha[/TD]
[TD="align: center"]Waliopiga kura[/TD]
[TD="align: center"]Asilimia[/TD]
[TD="align: center"]Kura halali[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"]8,928,826[/TD]
[TD="align: center"]6,846,681[/TD]
[TD="align: center"]77%[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]2000[/TD]
[TD="align: center"]10,088,484[/TD]
[TD="align: center"]8,517,598[/TD]
[TD="align: center"]84.43%[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]2005[/TD]
[TD="align: center"]16,407,318[/TD]
[TD="align: center"]11,365,477[/TD]
[TD="align: center"]72.4%[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]2010[/TD]
[TD="align: center"]20,137,303[/TD]
[TD="align: center"]8,397,963[/TD]
[TD="align: center"]42.8%[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Linaloleta hofu kuliko hata hayo matokeo ya mwaka 2010 ni kukosekana kwa tathmini ya hali kama hiyo ilivyoweza kujitokeza; si Tume ya Uchaguzi, si serikali, si bunge, si vyama vya siasa, si wanaharakati, si wasomi...hakuna kikundi chochote kilichoweza kukaa kujadili, kutafakari na kutoa tathmini ya uchaguzi huo na kutoa sababu kwa nini hali kama hiyo ilijitokeza.
Kama ni kweli kuwa walioweza kujiandikisha mpaka sasa kupitia BVR ni zaidi ya milioni 22, hiyo ni sawa kabisa kwani inaendana na takwimu za nyuma na ilitegemewa iwe hivyo. Dai lako la watu kujiandikisha tu eti kwa lengo la kupata kitambulisho halina mantiki na si sahihi. Unaelezaje waliojitokeza kujiandikisha kabla ya BVR huko nyuma? Mbona siku ya kura waliojitokeza walikuwa ni wengi tu?
Kama alivyosema Mwalimu tuzidi tu kuwashawishi wote waliojiandikisha wajitokeze kwa wingi siku ya upigaji kura na kwa technolojia ilipon tuhakikishe kwamba hiyo idadi haitachakachuliwa. Tupange namna ya kuhakiki kwamba taarifa zinazofikishwa Tume ni sahihi kwa kila kituo cha kupigia kura, kila jimbo, kila mkoa ili kuziba kabisa mianya ya wezi wetu hawa waliokubuhu.
Tunafuatilia kwa ukaribu sana kura za maoni za CCM.Mpo sawa wakuu,
Ila mm kuna jambo linanipa hofu kubwa sana kuhusu kura, nimeangalia cheating manipulation za kura kwenye kura za maoni za wabunge na madiwani wa CCM nimeogopa mno, nimemsikia Chegeni analalamika kuwa Kamani alikua anaongeza kura hadi manne kwa kituo, nikasema dah!!!! Kwenye chama ni haya je general election itakuaje?
Watu wengine wanapuuza haya mambo yanayoendelea kwenye kura za maoni za chama tawala na mauza uza yake, lakini ukiangalia kwa jichola tatu kuna cha kujifunza kinachoreflect General elections, hapo ndio namkubalia Nguruvi3 kwamba uchaguzi nizaidi ya kuhamasisha kupiga kura tu bali ni kujipanga kwa mikakati na mbinu. Ushindi hauji kiuwepesi kama wengine wanavyodhania. Bt hayo ngoja tuwaachie Elections strategists watuambie hizo mbinu na ufundi mwingine.
sehemu ya I
KUELEKEA UCHAGUZI
Wapinzani wanapaswa kuwa na busara kuelekea uchaguz
Hali kwa upande wa CCM si njema, hata hivyo, wameapa kutumia kila njia na goli la mkono kufikia malengo yao
Maswali, je polisi walitumia nguvu zao kwa busara? Jibu ni ndio na hapana
Ni ndio kwasababu, kwa mtazamo wetu eneo la msiba haliwezi kuwa eneo la siasa. Si kimaadili, kiutamaduni au kibinadamu.
Jibu la pili ni Hapana. Kwa maelezo yao, sababu walizotoa hazikidhi haja ya zuio.
Ni nyepesi zisizo na mashiko. Hivyo, kama lipo zuri, hilo lilitokea kwa bahati mbaya inayoweza kuonekana ni nzuri.
Je, Lowassa alipaswa kuhudhuria mazishi.
Jibu ni Ndiyo, akiwa raia ana haki hiyo. Akiwa ‘mwakilishi' kama ilikuwa ni hivyo ana haki hiyo
Je, Lowassa na timu yake walifanya jambo jema?
Kuhudhuria msiba ni jambo la faraja na la kibinadamu.
Msiba haupaswi kuwa sehemu ya siasa kwa kiwango kilichoonekana.
Ingawa hakuna kosa, kuna kukosekana kwa busara
WASHAURI
Tatizo la Lowassa kuambatana na timu yenye mavazi linaweza kuchangiwa na kukosekana ushauri.
Ombwe la ushauri ni hatari kuelekea uchaguzi. Tumesema uchaguzi si kuhesababu kura bali mahesabu ya kupata kura.
Katika mazingira yetu, unyenyekevu na busara ni sehemu ya kushinda nyoyo.
Lakini pia wapinzani watambue, vyombo vya dola vinatafuta sababu kuzuia nguvu inayoonekana kuielemea CCM
Hivyo, ni muhimu kutumia busara, kinyume chake wapinzani wanaweza kuwa katika wakati mgumu
Tumesikia tangazo la jeshi la Polisi kuzuia misafara,tumesikia tangazo la kamisheni ya mawasiliano dhidi ya ITV na Radio one
Hayo tutayajadili kwa kina, kwa ufupi,tujiulize. je, kile kinachoitwa Machinery of Governemnet (MoG) kimeanza kazi???
Tuajadili
Tusemezane
Nguruvi3,
..tatizo ccm huanzisha jambo au utaratibu fulani. Sasha wengine wakiiga na kuanza kuwazidi malaria basi ccm huleta vyombo cya dola kuzuia jambo hilo.
..ccm ndiyo waasisi wa utaratibu wa mazishi ya "kichama ". Wao ndiyo walioanzisha utaratibu wa kuvaa sare za chama kwenye misiba na kuvika majeneza bendera za ccm na vijana wa chama kuteka nyara shughuli za misiba.
..Kama ccm wanavaa sare zao kwenye misiba kwanini iwe makosa kwa waombolezaji wanachama wa vyama vingine kuvaa sare za vyama vyao?
..mimi simlaumu lowassa kwa kusindikizwa na umati wa watu kila anapokwenda. Hulu ni wakati wa uchaguzi, what do u expect??! Nitamlaumu na kumdharau kama atashindwa kuwafanya hawa wasindikizaji wawe wapiga kura.
..halafu huu umati na jinsi unavyokuwa mkubwa una effects zake ktk saikolojia ya wapinzani wa lowassa. Umati huu unawafanya ccm wafikirie mara mbili-'mbili kuhusu jinsi ya kukabiliana na ukawa/ccm/lowassa.
..lowassa amawatupia "chambo" ccm na polisi na wao wakakimeza. Polisi hawakupaswa kumzuia lowassa. Kitendo kile kimewafanya waonekane wanamuonea na kumuandama lowassa. Siku watakayompiga mabomu ndiyo watakuwa wamemtakasa machoni mwa wapenda mageuzi wa nchi hii na wanachama wenzake wa cdm. Kama utakumbuka mkutano mkuu wa cdm ulisheni wahanga wa ukatili wa namna mbalimbali wa polisi.
..busara ya lowassa ktk Sakata hili ni pale alipokataa agizo la polisi kwenda msibani bila washabiki wake waliokuwa wakimsindikiza. Kitendo kile kimejenga imani na ukaribu Kati yake na mashabiki wake.
Mkuu taratibu za CCM ni za kuvia nafasi. Pengine wapinzaniwangeongoza kwa kuonyesha utu misibani.Nguruvi3,
..tatizo ccm huanzisha jambo au utaratibu fulani. Sasha wengine wakiiga na kuanza kuwazidi malaria basi ccm huleta vyombo cya dola kuzuia jambo hilo.
..ccm ndiyo waasisi wa utaratibu wa mazishi ya "kichama ". Wao ndiyo walioanzisha utaratibu wa kuvaa sare za chama kwenye misiba na kuvika majeneza bendera za ccm na vijana wa chama kuteka nyara shughuli za misiba.
..Kama ccm wanavaa sare zao kwenye misiba kwanini iwe makosa kwa waombolezaji wanachama wa vyama vingine kuvaa sare za vyama vyao?
..mimi simlaumu lowassa kwa kusindikizwa na umati wa watu kila anapokwenda. Hulu ni wakati wa uchaguzi, what do u expect??! Nitamlaumu na kumdharau kama atashindwa kuwafanya hawa wasindikizaji wawe wapiga kura.
..halafu huu umati na jinsi unavyokuwa mkubwa una effects zake ktk saikolojia ya wapinzani wa lowassa. Umati huu unawafanya ccm wafikirie mara mbili-'mbili kuhusu jinsi ya kukabiliana na ukawa/ccm/lowassa.
..lowassa amawatupia "chambo" ccm na polisi na wao wakakimeza. Polisi hawakupaswa kumzuia lowassa. Kitendo kile kimewafanya waonekane wanamuonea na kumuandama lowassa. Siku watakayompiga mabomu ndiyo watakuwa wamemtakasa machoni mwa wapenda mageuzi wa nchi hii na wanachama wenzake wa cdm. Kama utakumbuka mkutano mkuu wa cdm ulisheni wahanga wa ukatili wa namna mbalimbali wa polisi.
..busara ya lowassa ktk Sakata hili ni pale alipokataa agizo la polisi kwenda msibani bila washabiki wake waliokuwa wakimsindikiza. Kitendo kile kimejenga imani na ukaribu Kati yake na mashabiki wake.
,,,Kama kuna kitu ambacho upinzani unapaswa kukipigania kufa na kupona ni kuhakikisha wote waliojiandikisha kupiga kura wanajitokeza tarehe 25 na wanapiga kura bila mizengwe yoyote. Ushindi wa 62% alioupata JK mwaka 2010 huku voters turnout ikiwa ni 42% pekee inatoa ujumbe kwamba endapo turnout ingekuwa 70% au hata 80% pengine tungekuwa tunaongea lugha nyingine sasa hivi!
Na hili wanapaswa kulisimamia kwa umakini sana hususani sasa tunapotumia huu mfumo wa BVR! Kwa matukio yaliyoripotiwa hivi karibuni ya baadhi ya viongozi kukamatwa wakikusanya kadi za kupigia kura kutoka kwa wananchi na kuzinakili namba ni dalili mbaya juu ya mambo yatakayotokea tarehe 25.