Chadema: Tupeni miaka mitano tung’oe umaskini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema: Tupeni miaka mitano tung’oe umaskini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Aug 23, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewataka wananchi kukipa madaraka ya kuongoza nchi kwa miaka mitano, ili kuwaondolea umasikini kwa kutumia rasilimali zilizopo ambazo zimekuwa zikifujwa na baadhi ya mafisadi walioko ndani ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Chadema imesema ili kufanikisha hilo, hivi sasa kimeanza kuwaunganisha Watanzania wote katika kupigania haki na kuwaondolea hofu ambayo imejazwa na watawala kwa muda mrefu huku mhimili wa mahakama ukianza kutumika vibaya.

  Akizungumza katika mikutano ya Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) inayoendelea katika vijiji mbalimbali mkoani Morogoro, Mwenyekiti wa taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema kuwa vuguvugu la mabadiliko linaloendeshwa na chama hicho kwa kuzunguka nchi nzima ni mapambano ya ukombozi wa watu wanyonge na masikini ambayo ni mapinduzi ya tabaka la watu masikini, wakulima na wafanyakazi.

  Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, alisema kuwa operesheni ya M4C ambayo kwa Mkoa wa Mororgoro itafika katika kata 180, majimbo 10, vijiji 585 na vitongoji 3,122 vya mkoa huu, ni sehemu ya mkakati wa Chadema wa kuendelea kujijenga na kujikita kwa watu nchi nzima hasa maeneo ya vijijini, ambapo moja ya kazi kubwa katika operesheni hiyo ni kuendelea kuwatia ujasiri Watanzania, kuwaunganisha na kuwaondolea hofu Watanzania ambayo wamejazwa kwa muda mrefu na watawala ili waweze kupigania haki zao.

  Tumeanzia na mkoa wenu wa Morogoro, baada ya hapa makamanda tutaitafuta Iringa, tutakwenda Dodoma, kisha tutapiga Manyara, tutamalizia na Singida," alisema Mbowe (pichani) na kuongeza:

  "Tutapumzika siku chache kisha awamu ya pili itaanza na tumeamua kutetea sauti za watu wasiokuwa na sauti, kwani Watanzania zaidi ya asilimia 95 ni masikini wasiokuwa na haki na rasilimali zao za nchi."

  Alisema kuwa mbali na vuguvugu hilo la mabadiliko kutumika kuwaunganisha Watanzania wote kudai mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutawala katika nchi yao, alisema chama hicho kinataka mchakato huo umilikiwe na wananchi wao wenyewe, ndiyo maana Chadema kimeanza mpango wa kuchangisha fedha.

  "Hivi unakwenda kuandaa mabadiliko makubwa katika nchi hii ndiyo maana tunataka mchakato huu wa vuguvugu hili umilikiwe na wananchi wenyewe. Hivi ndivyo walivyofanya akina Mwalimu Nyerere na wenzake wakati Tanu ilipokuwa ikipigania uhuru wa nchi hii, tofauti na wakati huu ambapo siasa imefanywa kuwa biashara badala ya kuwatumikia watu na kutengeneza fursa ya maendeleo ya watu," aliongeza Mbowe.

  Mbowe alisema: "Sasa tumefikia mahali pabaya, mnaona wenyewe Mahakama inavyoanza kutumika vibaya kulinda udhalimu wa CCM, wanajaribu kuzuia nguvu ya mabadiliko kwa kutumia Mahakama, wanataka kuzuia ‘Proletarian Revolution' kwa kutumia mahakama, tunawaambia hawawezi, huwezi kuzuia madai ya madaktari, walimu, wakulima, wafugaji na watu wengine wa tabaka la chini na kati kwa kutumia mahakama. Haiwezekani, tumefika hapa kwa sababu ya utawala mbovu wa CCM ambayo imeshaonyesha dalili zote za kushindwa kuongoza."

  Jana viongozi wa Chadema walianza ziara yao ya kuhutubia katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Morogoro Vijijini.


  CHANZO: NIPASHE

   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kwa miaka 20 wameshindwa kuimarisha chama, halafu kuna watu watadanganyika kuwa kwa miaka 5 wataondoa umasikini!!!
   
 3. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee baba yangu kwa miaka 50 magamba wameshindwa kutoa umaskini ngoja safari hii niwape chadema niwaone wakishindwa nawapa caf hao nao wakishindwa naamia somalia

  ngoja nipate mbege
   
 4. t

  tenende JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  gamba!.............
   
 5. johntoto2000

  johntoto2000 Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatudanganyiki ng'o .
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,125
  Trophy Points: 280
  Magamba utawajua. Hamdanganyiki nini?
   
 7. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Ina maana CHADEMA ipo kama ilivyokuwa miaka 20 iliyopita? Let's see: ina maana haina mbunge hata mmoja, haina hata halmashauri moja inayoiongoza n.k n.k

  Ingekuwa ni hivyo magamba msingekuwa mnaweweseka kiasi hiki!
   
 8. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Nakuonea huruma wewe!
   
 9. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  achana nae magambaz huyo!
   
 10. u

  ureni JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Hebu ijaze jaze nyama hiyo hoja yako ili ieleweke vizuri,wameshindwa kuimarisha chama kivipi?
   
 11. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Lengo la chama cha siasa ni kupewa dhamana ya kuongoza dola. Chama ambacho hakijawahi kuaminiwa na wananchi kupewa dola wala hakina hata asilimia 20 ya wabunge, kikijiona kimeshakuwa imara ni alinacha ya kisiasa.

  kwa miaka 20 CDM wamekuwa wanahangaika kutafuta jinsi ya kutoka, lakini hawajafanikiwa. Wakifikisha umri wa miaka 23 watakuwa na test nyingine kama wameshaaminiwa.

  Sasa watu kama hao wanapokudanganya kuwa wanahitaji miaka mitano kuondoa umasikini, ni kama wanapima akili yako. Ukikubali watakuona mjinga.

  kama umewapenda na umeamua kuwachagua sawa, lakini usidanganyike kuwa wataondoa umasikini kwa miaka mitano.

  Kodi wanataka kufuta, na nyingine kupunguza, bidhaa za viwandani kama cement bei itapungua (cement sh. 5000!), barabara kuu zote zitawekewa rami, kila kaya itakuwa na maji safi na salama, shule bure mpaka form six, huduma za afya bure, hospitali zote zitapatiwa vifaa vya kisasa, wahitimu wote wa chuo kikuu watapatiwa ajira, na umasikini utaondoka. hivi vyote kwa miaka mitano. Kama sio kuonana wajinga ni nini?
   
 12. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180


  Kodi wanataka kufuta, na nyingine kupunguza, bidhaa za viwandani kama cement bei itapungua (cement sh. 5000!), barabara kuu zote zitawekewa rami, kila kaya itakuwa na maji safi na salama, shule bure mpaka form six, huduma za afya bure, hospitali zote zitapatiwa vifaa vya kisasa, wahitimu wote wa chuo kikuu watapatiwa ajira, na umasikini utaondoka. hivi vyote kwa miaka mitano. Kama sio kuonana wajinga ni nini?......
  [/QUOTE]

  WEWE uliyekaa miaka 50 umefanya nini zaidi ya kuuza mali za nchi kwa mafisadi leo mnaanza kuteteana wenyewe kwa wenyewe mahakamani.uzoefu wa kuiba mali za umma ndiyo deal.pambafu
   
 13. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kuna kila sababu ya kuwapa chadema a try kwenye kuongoza nchi. wakishondwa tutajua nao hawana uwezo wa kuongoza nchi. tutampa mwingine tutakayemuona anatufaa wakati huo. ila kwa vile kwa miaka 50 tumekuwa tuna-mark time kwenye umasikini chini ya CCM, hatutaki tenakuwapa kipindi kingine cha uongozi...na hata wakichakachua safari hii hawaoni ndani...!
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama ukisikia kuna watu huzama baharini na kutojulikana walikokwenda au maiti zao hazikupatikana basi WaTz hawa CDM wakifanikiwa kupata utawala wa Nchi hii basi mjue ,tutakuwa tunazama baharini na shida na tabu zitakazotufika hatutakuwa tofauti na hao wanaozama baharini na maiti zao kutopatikana.
   
 15. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Wala hakuna haja ya kuomba mmepata
   
 16. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Miaka mitano ni ya kupunguza umaskini na si kuondoa umaskini.
  Anyway,ni busara kuwapa CDM dola tuone ndani ya miaka hiyo mitano watatufikisha wapi.
   
 17. T

  Tata JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,733
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280

  Kwa hili hujawatendea haki ZeMarcopolo. Wamejitahidi sana kuimarisha chama chao katika mazingira magumu ya mfumo wa chama kimoja ambamo, kama alivyothibitisha Waziri Mkuu hivi karibuni, viongozi wa dola kama wakuu wa mikoa na wilaya wamepewa maelekezo kuhakikisha wapinzani hawakatizi.

  Tunapokwenda wanazidi kuimarika kwa kasi ya ajabu. Mimi nafurahi kwani karibu nitakwenda kufufua kadi yangu ya CCM pale tutakapokuwa wapinzani rasmi na hapo mafisadi wanaotusumbua watakapokimbia kujiunga na CHADEMA na kuanzisha vyama vingine.
   
 18. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwendo mdundo... hakuna kulala mpaka kieleweke...
   
 19. T

  Tata JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,733
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  Kumbe ndugu yangu wewe bado hujazama mpaka sasa? Wengine tulishazama baharini chini ya huu utawala fisadi ulioleta shida na tabu nyingi kwa watanzania.
   
 20. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 180
  Magamba kweli ni viazi!kwani nyie mmetuzamisha mara ngapi kwenye mamikataba feki ya nchi hii? Hiyo miaka hamsini mnayo jidai nayo ndio maisha bora haya? Hebu lione hata aibu halioni.
   
Loading...