Huko Nyuma niliwahi kuomba ushauri wa jinsi ya kumshitaki Mkapa the Hague baada ya mauwaji ya Pemba. Ushauri mzuri niliopewa ilikuwa ni kupeleka mashitaka Ubelgiji ambao wana sheria ya kumukamata mtu yeyote toka Dunia yoyote anapopatikana na makosa ya saizi hii ya mauwaji ya makusudi wakati wakilindwa na sheria za nchi husika.
Ras Bashir kisha takiwa kukamatwa na nchi za Ulaya ndo maana haweki mguu wake ulaya yote.
Kwa hili la Polisi wetu hapa nchini sasa limekuwa gumu. Kama RPC anaweza kuamuru kupiga bomu na halafu IGP anaishia kufanya mkutano na kuunda tume, si mara moja wala mara mbili! Ni tatizo!
CHADEMA, kwa ufahamu wa wanasheria wenu na kuaminika kwenu sasa hivi, hamuwezi kuichukuwa njia hii? Tumpate Mwanasheria mmoja huko Brussels aisimamie kwa ushahidi huu wa video na waliokuwepo. Kama itawezekana basi washitakiwa iwe ni RPC Moro, RPC Iringa, IGP na Rais wa JMT.
Kesi hii ikifishwa mapema Brussels na ikaamuliwa wakamatwe ni safi sana maana hata safari za Ulaya na msururu wa watu kwa Rais huyu zitakoma kabisa. sijui atakimbilia India?