CHADEMA, tunaweza kuitumia The Hague au Brussels? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, tunaweza kuitumia The Hague au Brussels?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Sep 3, 2012.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Huko Nyuma niliwahi kuomba ushauri wa jinsi ya kumshitaki Mkapa the Hague baada ya mauwaji ya Pemba. Ushauri mzuri niliopewa ilikuwa ni kupeleka mashitaka Ubelgiji ambao wana sheria ya kumukamata mtu yeyote toka Dunia yoyote anapopatikana na makosa ya saizi hii ya mauwaji ya makusudi wakati wakilindwa na sheria za nchi husika.

  Ras Bashir kisha takiwa kukamatwa na nchi za Ulaya ndo maana haweki mguu wake ulaya yote.

  Kwa hili la Polisi wetu hapa nchini sasa limekuwa gumu. Kama RPC anaweza kuamuru kupiga bomu na halafu IGP anaishia kufanya mkutano na kuunda tume, si mara moja wala mara mbili! Ni tatizo!

  CHADEMA, kwa ufahamu wa wanasheria wenu na kuaminika kwenu sasa hivi, hamuwezi kuichukuwa njia hii? Tumpate Mwanasheria mmoja huko Brussels aisimamie kwa ushahidi huu wa video na waliokuwepo. Kama itawezekana basi washitakiwa iwe ni RPC Moro, RPC Iringa, IGP na Rais wa JMT.

  Kesi hii ikifishwa mapema Brussels na ikaamuliwa wakamatwe ni safi sana maana hata safari za Ulaya na msururu wa watu kwa Rais huyu zitakoma kabisa. sijui atakimbilia India?
   
 2. g

  gnm Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  ushauri ni mzuri ila utekelezaji wake ni gharama kubwa na je mfumo uko tayari kuliachia hilo lifanyike?
   
 3. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Imani yangu ni kwamba hatuna mfumo, tuna wahuni ambao kama kawaida sasa wataanza kufungua kesi na kusema suala liko mahakamani. Hili litakaa kwa miaka 10 bila hukumu kama zile kesi za waliokutwa na madawa ya kulevya kwenye maiti.

  Labda kama gharama ni kubwa hapo kweli ni tatizo. Kama siyo vigumu kiasi hicho, ikifunguliwa tu naamini heshima itakuja hata kabla ya hukumu.
   
 4. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Ni wazo zuri! Hata Desmond Tutu wa SA amesema kuwa Bush na Blair wanapaswa wakamatwe wakajibu mashitaka ya kuivamia Iraq (huko the Hague ) bila sababu na kusababisha vifo vya maelfu ya raia bila makosa.
   
Loading...