CHADEMA Tulichokosea Ni Hiki...

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
854
CHADEMA Tulichokosea Ni Hiki.....

Kwanza ieleweke kuwa, siku zote chama cha siasa objective yake kuu huwa ni kushika dola. Na katika mazingira haya, mbinu yoyote inaweza kutumika iwe halali au hata haramu, kubali usikubali.

Wote tunakumbuka ule upepo uliokuwa ukivuma kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge wa mwaka 2015. Katika kipindi hiki tulishuhudia wanasiasa wengi kutoka CCM wakihamia CHADEMA. Tulishuhudia mawaziri wakuu wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye wakihamia CCM, pia tulishuhudia Kingunge Ngombale Mwiru, Masha, Saidi Nkumba, na wanasiasa wengi sana wakihamia CHADEMA wakitokea huko CCM. Wote tulifurahi sana, hata mimi nilifurahi sana kwa sababu niliamini mwisho wa CCM ndiyo umefika.

Lakini wakati tukifurahia immigration hiyo ya wana CCM kuja CHADEMA, kuna kitu tulijisahau ambacho leo hii kinatugharimu. Kwamba, tulimuamini kila mtu aliyehamia CHADEMA akitokea CCM...mbaya zaidi tuliwapa kipa umbele cha kupeperusha bendera kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CHADEMA na kuwapa kisogo waliokijenga chama hadi kufikia hapa kilipo--hili ni kosa kubwa sana tulilolifanya. Kwa Amerika, ili mtu au raia agombee nafasi ya Urais katika nchi ile, sharti mtu huyo awe ameishi nchini humo miaka isiyopungua 14 ndipo anaweza kugombea nafasi ya Urais. Hii ina maana ya kuwa kwa kipindi hicho cha miaka 14 ni rahisi kumjua mtu nyendo zake zote; sasa sisi mtu kaondoka CCM leo na kuja CHADEMA kesho tunampa bendera aipeperushe kwa maana ya kugombea nafasi fulani ndani ya CHADEMA. This is a big mistake!

Pamoja na hayo, tujipongeze kwa kumnyima Saidi Nkumba kule Sikonge mwaka ule wa uchaguzi, kwa sababu tungemruhusu kugombea ubunge halafu akashinda, si ajabu naye leo hii tungemsikia anaongea ya hovyo hovyo ya kuhama CHADEMA kwa madai ya kumuunga mkono sijui nani nani vile.

HITIMISHO: Ili ku-get rid of this situation, lazima tuwe na kanuni zetu ili kukiboresha chama chetu pendwa na ambacho kinapendwa kwa dhati na wananchi walala hoi mimi nikiwa miongoni mwao.

Kwanza, ili mwanachama agombee nafasi yoyote basi lazima awe mwanachama kwa kipindi kisichopungua miaka miwili tangu kujiunga kwake uanachama. Hii itasaidia kwa kiasi fulani kuwa-screen watu sahihi kwa nafasi sahihi.

Pili, watu waliokijenga chama na walio na sifa zote kwa nafasi fulani ndiyo wawe kipaumbele au wapewe upendeleo kugombea nafasi fulani ndani ya chama. Tukifanya hili, tutaondokana na mijitu inayoimba wimbo ambao hauendani na beat kwa chorus inayosema 'tunahama CHADEMA ili kumuunga mkono sijui nani nani'.

Tatu, paragraph yangu ya kwanza inazungumzia objective ya chama cha siasa, ila tuwe makini maana kuna watu wapo kazini. Tusimuamini kila mtu, tuwapokee kujiunga na chama chetu, tuwapende kama Watanzania wenzetu ila tusiwaamini.

We always learn from the mistakes.
Kwa uwezo wake Mungu tutashinda, na tumeshaanza kushinda kwa kupitia kipenzi chetu Tundu Antipas Lissu.

Nawasilisha.
 
Kwenye msafara wa mamba kenge anakosaje kwa mfano?!!
 
Mtindo wa siku hizi ni pesa tu hata ccm walikua na kasumba ya kuthamini wenye pesa zaid kuliko waliowalea ndani ya chama.sasa imekuwakinyume huku wanaacha kule wanawatafuta
 
Kazi iliyopo ni kujenga chadema mpya,kwa maana watu wenye malengo hasa.
Hawa wanaounga mkono juhudi,huyu mwenye juhudi akibadilika kutokana na ninyi mloounga mkono kutaka mabadiliko nini kitatokea.
Au mtakaa kimya mpaka juhudi zizae matunda?
Siku mkitaka kurudi mkumbuke mikia yenu ilipokatikia.
 
Kama chadema haitaliangalia hili kwa makini litaendelea kuwagharimu.
 
Sasa,hilo pia kama ni kweli,si litatokea kwa CCM?Siasa hizi ngumu sana. Bora kuwa Neutral!
 
Kuwa rais wa Marekani siyo kuishi tu, lazima uwe mzawa.
Sorry, labda sikuweka ufafanuzi vizuri, ila pia wako umejazia pale palipopungua kwenye maelezo yangu. Hiyo miaka 14 ni moja ya qualifications za kugombea Urais, sijazitaja zote. Ila asante tunajengana kwa namna hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…