Lupyeee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 2,683
- 2,820
Kuna utafiti ulifanyika huko Uingereza na kubainisha kuwa Tanzania ndio nchi ya wanafiki zaidi duniani, mwanzoni nilipinga lakini tangu hili sakata la madawa ya kulevya lianze nimeamini utafiti ule ni kweli.
Tangu zamani wapinzani hasa CHADEMA ndio walikuwa wakipiga kelele kuwa serikali ichukue hatua kali dhidi ya wauza madawa ya kulevya ikiwemo kuwataja hadharani. Mbunge wa CHADEMA Ester Bulaya aliwahi kusimama na kulia bungeni kuwa Vijana wa taifa hili wanaangamia kwa mihadarati, alimtolea mfano mdogo wake ambaye yupo mwananyamala akitibiwa baada ya kuathirika vibaya na matumizi ya mihadarati.
Naama, hatimaye serikali iliitikia wito wa wapinzani na watanzania kwa ujumla, kupitia RC Makonda serikali ilianza kuchukua hatua kali ikiwemo kuwataja hadharani wauzaji na watumiaji wa mihadarati. Cha ajabu kabisa na kwa unafiki wa kiwango cha PhD chadema wameibuka na kupinga juhudi za RC Makonda.
Wabunge wa CHADEMA ikiwemo Ester Bulaya ambaye mdogo wake amekuwa zezeta sababu ya madawa ya kulevya wameibuka kupaza sauti kwamba kutokana na kupambana vikali na biashara ya dawa za kulevya basi RC Makonda atumbuliwe! Eti wanamuomba rais atengue uteuzi wake! Kama siyo mnufaika wa madawa ya kulevya kwa nini upinge na kulalamikia kukomeshwa kwa biashara ya mihadarati?
In short wote wanaolalamika ni wanufaika wa biashara ya madawa ya kulevya, ila ni unafiki tu ulikuwa unawasumbua hadi kuililia serikali ikomeshe biashara hii haramu.