CHADEMA Tanga wamuunga mkono Slaa

Mimi nawashangaa sana wafuasi wa ukawa na Lowassa. Kwanini hamjibu kwa hoja ba badala yake mnakimbilia matusi tuuuuuuu. Acheni hizo jibuni kwa hoja. Na lazima mkubali mawazo tofauti. Kwani ninyi UKAWA malaika kwamba hamna makosa? Mkiitwa kuwa ninyi ni kundi la wahuni tuu wa mitaani mnanung'unika. Mambo mnayoyafanya hayaoneshi ustaarabu wenu. Jifunzeni hekima.
 
ama kweli hii habari imetulia. nimejifunza kitu humu, ubarikiwe.

 
wazee wa roba na bangi mambo kama haya hawataki hata kusikia,eti mabadiliko kuliko kuweka jitu jizi hayo mabadiliko tuyasubiri miaka ijayo
 
Wapuuzi ninyi.

chadema hakimtambui mtu anayeitwa Jonathan Bahweje, msemaji wa Chama kanda ni mwenyekiti Aman Golugwa.


Peleka ushuzi wako kwako siyo chadema

Jiulize, mtu anapayuka ati Chadema Tanga waamua mkumuunga mkono Dr. Slaa, kwa lipi. Dr Slaa tangu harakati za kuchukua fomu ya Urais hajaonekana hadharani na wala hajaongea na vyombo vya habari sasa hawa watu wa Tanga wanamuunga mkono kwa lipi alilosema. Wamngoje aitishe mkutano na wanahabari, atoe duku duku lake kama lipo, atueleze msimamo wake kama alivyofanya Profesa ndipo sasa watu wamuunge mkono au waachane naye. Hii ni sawa na ile safari ya wana wa Israel kuelekea Kanan. Mimi nitamsikiliza yule tu atakayenieleza namna nzuri ya kufika Kanan lakini yule anayenivuta shati ati nirudi Misri aachane na mimi kwani hata angekuwa nani sintomsikiliza.
 
Wala haishangazi sana,watu wa tanga mbali na viwanda vingi kufa na bandari kusimama mmeendelea kuwa watiifu kwa ccm ndo maana serikali haiwazii kufufua hivyo viwanda make wanajua kura watapata tu,poleni
Sijui ni kutojua kiswahili au kukosa adabu lakini hapa umetutukana watu wa Tanga wote pamoja na wana ukawa
 
Afadhali Tanga kuna wanachadema wenye akili
 
mwaka huu mmeshikwa haswa mtaharisha sana na ikulu mahali penu tenasijui mtaenda wapi
poleni wa lumumba
 

Watanzania? sema wewe kwani aliyeandika hayupo nawe
 
watu wa chadema mbona mnashindwa kujibu hoja badala yake matusi mnatakiwa mkanushe kwa hoja kama habari hizo I za ukweli au uongo kuna gazeti liliandika habari hiyo mapema il ilionkana ni uushilakini leo imethibitika kwamba waliyoyaandika ndio yanatokea jifunzeni kujibu hoja
 
Mkuu umetisha sana!!!.
 
Mimi nachokiona kama tunataka kufanana nawatu wa Ujerumani ya 1930's, wenyewe ulikuwa wanataka mabadiliko tu hawakuangalia mabadiliko wanayapataje. Hii ni hatari sana kwani Mh. kashindwa kukanusha kabisa. Nn maanayake kitaingia madarakani chama cha wapigaji tupu.
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoni Tanga kimesema kuwa katika kuelekea uchaguzi mkuu wanamuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu Dkt Wilbroad Slaa kwa kitendo chake cha kukaa pembeni kutokana na ujio wa Edward Lowassa na kupewa nafasi ya kuwania urais.

Sisi wanachama na viongozi wa chama chetu mkoani Tanga tunaunga mkono kwa dhana kwamba kumsimamisha Lowassa kutaathiri mwenendo wa chama chetu kwa vile ndugu Lowassa haonekani vema na jamii kutokana na matendo yake Katika serikali ya CCM.

Madai kwamba Lowassa amenunua nafasi ya Urais katika chama chetu kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 10 hayajakanushwa popote hivyo na sisi tunaona ni Madai ya kweli.

Chama chetu kwa miaka kadhaa kimekuwa kikijenga kwa jamii kwa kueleza mabaya ya CCM ikiwemo suala la Katibu Mkuu kutamka majina ya watu 12 akiwemo Lowasa Kuwa siyo wasafi ni mafisadi katika list of Shame iweje leo awe mgombea wetu.

Tusitishike na mikutano kujaa watu kwani wapo vijana ambao hawana shughuli za kufanya wanapenda mikusanyiko hivyo tusijifarague kuona tunaweza kushinda na mgombea huyu ambaye kule CCM katika vigezo 13 walivyoweka hakuwa anakidhi vipi sisi tumuone anafaa?

Kwa kuwa michakato imeshafanyika kibabe na shinikizo la fedha sisi tutawapigia kura wagombea wetu wa udiwani na ubunge lakini Rais hatutampa mgombea wetu kwa kuwa hatoshi na hana sifa ya Kuwa RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwisho mwenyekiti kama una nia njema na chama kanusha suala la Lowassa kukupa fedha wewe binafsi vinginevyo huko twendako kwenye kampeni hoja hii itatumaliza na jamii iliyokuwa ikituamini kupoteza matumaini ya sisi kuwa Chama Tawala na hili tutawaumiza sana Watanzania ambao wamejenga matumaini kwa muda mrefu na sasa tumeharibu mwelekeo na matumaini yao.

Jonathan Bahweje
Afisa wa Chadema
Kanda ya Kaskazini
 
Mim naamini Ccm wamekwisha penyeza Rupia. Sasa wewe na wengine wenye mawazo mgando nendeni makamfuate huyo dr.

Lipumba ameondoka ukawa lkn hakuna hata Inzi aliyemfuata. Na wewe ondoka tu Ndooooooorobo wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…