[/QUOTE]CHADEMA kama mnasikia, bila kuwa na Mpango-mkakati wa kulinda Kura, harakati zote zitakwenda na maji.
Nimeweka title kali kidogo kwa sababu nataka kudraw attention ya wadau wa CHADEMA. Actually mi ni mdau wa CHADEMA na niko huku jimboni, bega kwa bega na mgombea ubunge tunapambana na mwarabu mmoja.
Pamoja na umuhimu na juhudi tunazofanya katika kampeni zetu, naomba, timu za wagombea udiwani, ubunge, na rais, zifikirie kutoa muda (pengine kwa kusimamisha kampeni), na kujipanga jinsi ya kuzuia wizi wa kura. Nimegundua kuwa inaweza kuwa ni sawa na mtu unapita ukipanga miche bora, kumbe nyuma yako shetani anapita akizingoa na kupanda magugu. Mwisho wa siku ukigeuka nyuma huna kitu.
Yafuatayo (naamini yamefanyiwa kazi), naomba tuyape majibu yake
Tutahakikishaje kura zetu zinalindwa katika maeneo ambayo hamna wagombea ubunge na/au udiwani? Hii Tanzania ni kubwa aisee, tusi assume tu kuwa kuna watu watakuwa mawakala, CCM are very smart in that. Ni nani atakayepita na kuhakiki majina na idadi ya wapiga kura katika maeneo haya ya pembezoni yatakapobandikwa hizo cku 8 kabla ya uchaguzi? Yapo mengi ambayo inabidi tuyaangalie...
Naomba pamoja na mbinu nyingine, tuangalie kama hizi zitatusaidia; Kuweka mawakala zaidi ya mmoja kila kituo (kwa ticket ya vyama vingine vidogo vinavyoshiriki uchaguzi) ili kupunguza urahisi wa kununuliwa, kuanza kuunda timu za mawakala kila jimbo, na pengine Dr Slaa anapopita aseme sentensi chache kuwapa moyo na hamasa (ikiwezekana hata kukutana na baadhi yao wakati wa mapumziko), kuwasiliana na wagombea wote wa ubunge na kuwaelekeza namna ya kuomba kopi ya daftari la wapiga kura kwa maeneo yao, ili kulikagua na kujipanga kutokana na kila kituo kinavyoonekena (huku kwetu tunafanya juhudi, karibia tunalipata), wanaCHADEMA naomba muongeze mbinu hapa...
Mugo"The Great";1108786 said:Ninaiunga mkono hoja. Mwaka 2000 nilishududia kwa macho yangu majulimsho ya Kura katika jimbo la Uchaguzi. Siku kura zilipojulimshwa na kwa mabishano makali, Prof. Lipumba alimzidi Mkapa kwa kura zaidi ya 500. lakini kesho asubuhi yalipobandikwa kwenye mbao za matangazo, Mkapa alimzidi Prof. Lipumba kwa zaidi ya kura 2000.
CHADEMA kama mnasikia, bila kuwa na Mpango-mkakati wa kulinda Kura, harakati zote zitakwenda na maji.
Tupo wote kwenye hilo lakini karata turufu ya CCM ni kuwanunua mawakala wa Chadema ili wasaini matokeo ya mezani badala ya kuhesabu kura.
Chadema wakiweza hilo basi ushindi hauna utata hata kidogo.
Wameanza kuandikisha shahada za kupigia kura siku zote sikujua kwamba hii kazi inafanyika jana usiku mnamo saa nne nilitembelewa na mjumbe wa nyumba kumi kwa sababu wanajua mimi ni mwana CCM wakaniambia wanataka kujua kama shahada yangu niliihakiki wakati tume ilipita kuandikisha upya daftari la wapiga kura ,nikawambia sikuhakiki kwa sababu niliwasikia tume kama huna tatizo na kipande chako huna sababu ya kwenda huko wakasema basi tunataka kuandikisha wanachama wetu ili tuone wangapi watatupigia kura ,mimi nikawambia mwaka huu mimi nitapigia upinzani kwa sababu naipenda sana nchi yangu siwezi kuiweka rehani kwa miaka mingine mitano
Basi wakaniambia eti watakuja kuongea tena na mimi leo kwani wanaona labda nilikuwa na uchovu wa Kazi kwa hiyo haukuwa muda mwa faka wa kuongea wakiondoka waliataka kuacha chupa ya mvinyo
nikajiuliza hivi kweli kura yangu naweza nikaiiuza kwa chupa ya mvinyo
Lazima mkakati thabiti ufanyike wa kuhakikisha tunalinda kura wenzetu wa pinzani wanaweza kuandikisha watu watakao jitolea hata bila kulipwa na vyama na kushirikiana na wananchi wenye mapenzi mema kuhakikisha haki inatendeka leo nimetayarisha maji ya pilipili wakija nawamwagia ha ha
Unaishi Mbezi ama Kimara? :becky: