CHADEMA Shadow Cabinet: Jokers & Comedians!


Thanks Mheshimiwa! umemaliza.
 

Very well said!
 
 
Nakubaliana nawe mhandisi mwenzangu. Kama utakuwa mfualiaji mzuri wa siasa za vyama hapa nyumbani na hasa vikao vya bunge utagundua kuwa kama kuna chama chenye consultant wa maana basi ni CDM. Si ushabiki na si bias, kwa mtu wa uelewa wa kawaida tu anaweza kuona namna hoja inayojengwa na kichwa kimoja inavoweza kuwaendesha wapinga hoja 200,mpaka wapigwe jeki na spika. N kama unawafahamu vizuri hao watoa hoja,utagundua kuwa ni watu waliopikwa vizuri, na wanaojua kufanya homework zao vyema. Hapa ndipo CDM ilipojitofautisha na vyama vingine vya siasa.
Siasa ni sayansi kweli, na utawagundua tu wanaoindesha kisayansi hasa kama nawe ni mwanasayansi. Kwa effects tunazoziona ndani ya miezi mitano tu baada ya uchaguzi, hakuna doubts kwamba tutaona mengi miaka hii mitano. Na sidhani kama tayari huu ni wakati wa huyo independent consultant kufanya "thorogh reviews za ministries competency" ulizoelekeza hapo chini, ila la kuwajengea uwezo, yes nipo nawe.

 

Mkuu tuko pamoja.
 

SlidingRoof.Heshima mbele!

Kwanza kabisa nikushukuru na nikupongeze kwa kutoa maoni yako.

Inawezekana unadhamira njema au mbaya.Au yawezekana kama ilivyokawaida yako kupinga pinga kila kitu kama ambavyo ulivyokuwa ukitumia kwenye jina lako lingine la awali.Nilidhani ulivyokuja kivingine ungebadilika kumbe sivyo.Tuyaache hayo,ngoja nirudi kwenye hoja.

Kuhusiana na hoja yako ya kuwa Cabinet yetu kuwa namapungufu nakubaliana na wewe.Lakini ukumbuke kuwa CHADEMA ina Wabunge 48 tu na Cabinet yetu ni ya watu 39. Katika Kuunda Baraza kivuli la watu 29 isingekuwa rahisi kila mmoja kumpatia taaluma yake kwani kuna wizara wangengongana na nyingine zingekosa kabisa watu. Lakini vili vile unatakiwa kujua pia sio wabunge wote wa CHADEMA wanaelimu kama hiyo unayaoitaka wewe. Tuna Wabunge 23 wa majimbo na kati yao 22 wamepewa Wizara bila kujali elimu zao kwa kuwa kwa kufanya hivyo basi wizara nyingi zingekuwa hazina wasemaji.Kati yao 16 tu wanatoka Viti Maalumu. Kwa chama chochote cha upinzani unapounda baraza kivuli huangalii CV za watu pekee vile vile kuna suala zima la siasa,umaeneo,jinsia n.k.Hivi ni baadhi ya vigezo vilivyotumika.Ndio maana unawaona kina Joseph Mbilinyi,Lema,Regia na wengineo. Vile vile ndugu yangu lazima ujue kuwa na PHD au uzoefu fulani sio hoja katika ufanisi wa kazi duniani pote.Ndio maana pamoja na uwepo wa PHD nyingi sana Tanzania lakini bado tunamatatizo makubwa ya msingi.leo Mnyika anaweza kuperform vizuri sana kuliko maprofesa na madaktari wengi ndani ya Bunge. Elimu sio kipimo cha ufanisi kwa mtazamo wangu.


Pili. Ni mapema mno kuanza kulikosoa baraza kivuli,baraza hili limeundwa mwezi februari hata miezi miwili haijaisha wala mafunzo kwa baraza hili hayajafanyika.

Tatu. Kama kuna Mbunge wetu yuko bize na Facebook au JF huo ni uhuru wake na kila mtu ana haki ya kufanya hivyo.Kila mmoja anaratiba zake kwani kuupdate status Facebook inachukua siku nzima?Wewe unapataej muda wa kufuatilia na wenzeko Facebook na kuandika huku JF?unafikiri mwenye kazi ni waizri peke yake?hata nyinyi mnapaswa kuwa bize kwenye maeneo yenu ya kazi.Sote tunategemeana.Uwaziri ni Political post na nyie ndio watendaji wenyewe.Nchi haiendelei kwa matamko na barua.Vitendo ndio vinabdili nchi.Hata hivyo Kila mtu ana haki ya kurelax na kumake fun.Kama wewe unamatatizo yako na huwezi kuwa na muda wa kuenjoy hilo ni tatizo lako.Usifanye maisha kuwa magumu.
Nne.Mkumbuke pia si kila mtu hupenda kufanya kazi kwa kutumia vyombo vya habari.Wapo wanaofanya kazi kimya kimya sio lazima nyie mjue kila kitu. Kila waziri wa CHADEMA anajua misimamo ya Sera za chama kulingana na hata ukituamsha usiku wa maneno utapewa misimamo yetu ya kisera na wameshafanya kazi kadhaa na wengine tupo kwenye maandalizi ya hoja binafsi kuhusiana na maslahi ya wafanyakazi.
Tano.Kwenye baraza letu majority ni wanaume na wanawake wote waliopewa nafasi wanaangalau digrii maoja na kuendelea.Acha mfumo dume,bado hujabaidlika tu?usitumie akili zako kujenga hoja zinazohitaji facts.

Sita.Naomi Kaihula yuko kwenye wizara sahihi kabisa.Kwa taarifa yako ni mmoja wa waanzilishi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania na ni Mwalimu.

Saba,Binafsi nakubaliana na wewe uwezo wangu ni mdogo kupewa Wizara,sio ya kazi na Ajira tu kama unavyoona wewe,sistahili kupewa Wizara yeyote ile lakini kwa kuwa ninajitambua kwamba ni mtu wa kujifunza na kujisomea na ni mchapakazi na hata walionipendkeza wanatambua hilo naamini nitafanya vizuri kama ilivyo kawaida yangu na mtakuja kushangaa.Kuna msemo unasema usikisifu kitabu kwa gamba lake la nje.Huwa najifunza haraka na kuendana na mazingira yaliyopo.Fuatilia rekodi zangu kuanzia shule ya msingi,sekondari,chuo kikuu na hata CHADEMA.Kumbuka hapa naongea in public na kuna watu wengi tu humu wanonifahamu vizuri.Give me enough time.

It can be done play your part.
Aluta Continua
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
 
Ni jibu linalostahili. Changamoto ni mwanzo mzuri wa kufanya mambo sawa. Ahsante sana mama. Huko juu ameambiwa ametumwa na mwanaume mwezie tuendelee kumuelimisha.
 
Regina

Anafikiri nyie ni wakina sofia simba, Fyuuuuuuuuuuuuuuuuu!. Hivi kweli mtu anaweza kuhoji Regina Mtema kupewa wizara tena kivuli wakati watu kama sofia simba au mama sita wameshawahi kuwa mawaziri. Leo hii akisimama Regina na akasimama sofia au hawa Ghasia acha vigezo vingine kujieleza tu kweli mtu anahewa kuthubutu kuhoji nani ni bora?

Halafu watanzania wengi wanazani vyeti na competense muhimu ni Vyeti na ndiyo maana wate wamekazana kusoma MBA na masters lakini hata kuandika a simple submission or business case hawawezi. Wakija wakenya na diploma zao wanachukua kazi zetu. Vyeti ni muhimu lakini pia uweza wa kufanya jambo fulani ni muhimu sana.
 
Indeed, a piece for the opposition to ponder.

But I wonder... why the "wachaga this, wachaga that" line has always got to crawl into your disceptations?!!

I thought Tanzania is known as the LAND OF KILIMANJARO au?
 



I will be back.....
 
Kama mnadhani hii ndio staili ya kutoa "CRITICISM"...basi tumekwisha! Hivi Tanzania itegemee kuwa nyie ndio consultant wetu kwenye masuala ya kitaifa kwa namna hii?HApo kwenye red,you know why?:
So Kenya today thinks Kibaki will be the answer and tommorrow they understand he's not. They vote him out, he refuses and what follows is history. The same happens in Zimbabwe, Uganda, Ivory Coast and you name it. People do want CHANGE, and they want it DESPARETELY! The only difference between you (and SR for this sake) and the people out there is that when you write about the so called "criticising CDM", you are simply playing your favourite game of politics, trying to exercise your styles of writing and your analytical skills about the "wrongs" of African democracy and the "rights" about USA politics bla bla blah! And you are doing this in an Air conditioned room over a cup of coffee. On the other hand, the people of this country (and its mother land Africa), don't care about that. At all! They only care about them sitting on gold and diamond and tanzanite and still going on a single meal. They care about living in huts after 50 years of independence. They care about being blessed with the mighty Serengeti and ngorongoro and still living in life conditions just a stone-throwing-distance from the level of civilization that the wild life in serengeti are in. They want that to be adressed first. If you promise them today that you will give them a military regime that will get them out of that, count on me, the will equivocally ACCEPT that! So is the desparation and so is it understandable! Dwell in your politiking they will surely stone you!

I would love that you so called wasomi wa nji hii, to be in the shoes of those people. Who told you they care about the general election of CDM or CCM now? Or Obama VS Clinton politics? Bring in constructive ideas, solutions,CRITICISM yes, let's guide the people into the best way out of this mess. Telling them ah you know ...so ans so don't have good CV's...or so and so is so much into facebook...oooh...you know wazee walimweka mbowe hapo....oh unajua hata Dr Slaa hakuteuliwa kidemokrasia vizuri, kwani hakupitia zile primaries kama clinton na obama....bla bla bla...c'mon!!! Where are you living? Which part of the sky?
Na mnaongea hivi humu kwenye JF tu. Na mngeongea hivi hadharani watu wangemalizia njaa zao kwenu! Kuweni wazalendo bwana! Msitudanganye kwa lugha zanu eti mnataka kujenga CDM...It's not about CDM here! What is CDM? CDM can still betray us in the future just like the other parties did! IT SHOULD BE ABOUT THE BEST INTEREST OF THIS NATION AND THAT OF IT'S PEOPLE period! Whoever is for nation is my friend,whoever is not is my ENEMY! And I don't believe there is a neutral ground!



 

Umeeleza frustration zako ambazo ni za kweli. Hao wenye njaa wanahitaji leadership ndicho kinachojadiliwa. Sasa wewe kila chama ni kibaya wakati hoja ni "wachekeshaji na wataniaji wa Baraza kivuli" sijui unatusadia nini hapa? Au ndiyo mkakati wa kutuondoa kwenye mjadala kiaina? Anza upya.
 

Inakuwa vigumu kama umechukua muda mwingi na kuandika mada ya ccm hii kama hujaona ni hao mawaziri wa Chadema wamewaweka ccm dodoma. Dodoma mnafanya nini? Kwanini mnavuliana magwanda ni kwasababu inapenda au cdm inawapa shida? Wimbi baya la siasa zenu, magonjwa na umaskini, elimu mbaya mliotulea ya mapinduzi yasiona na mbele wala nyuma, wizi na ufisadi unafanananishwa na Gadaffi na Mubarak. Kitu gani Chadema haijawasha? Mmekufa na January hata wasaidia kuwaokoa wala Kinana, time up wazembe wakubwa na mafisadi. Chadema ndio wana-credibility na uwezo wa kuongoza Tanzania.

Endeleeni kutumia dairy news na magazeti ya serikali kwa kodi zetu na pia tbc, kimewashinda nini kama sio mnakataliwa sasa hata na babu na bibi yangu. Msicheze na maisha ya binadamu mkafanya ni opportunities zenu kutajirika, kila kitu kinamwisho na ndio huu.
 

Mara e-mail ya Chadema haifanyi kazi,mara baraza la kivuli la Chadema limejaa jokers....Huhitaji hata kozi ya dk 20 ya uchambuzi wa mambo kutambua kuwa hivi sasa nchi ni kama inaongozwa na Chadema.Hao hao unaowaita jokers and comedianis ndio waliowezesha CCM kufyata mkia na kuondoa muswada wa marekebisho ya Katiba.Na haohao unaowapuuza ndio waliopelekea CCM "kujivua magamba".

Tunafahamu sana kuwa INAWAUMA,tena INAWAUMA SANA baada ya kubaini kuwa mnalazimika kufuata matakwa ya Chadema pasipo ridhaa yenu.

A muppet is way better than a fool.
 

Mzee umemaliza kila kitu.Hicho ni mithili ya kipigo cha paka mwizi...ooops I meant fisadi sugu
 
Sasa hizo kelele mtakua mnapigiana wenyewe humu? No wonder Msekwa anasema JF mali ya CHADEMA.

Kama ni ya Chadema mbona nyie wana-Chama cha Mafisadi bado mpo?Mmekuja kupeleleza au ndio kuwashwa kwenyewe huko?
 

Wameumwa hawa.Njaa zao ndio zinawasumbua hadi kufikia hatua ya kusaliti Watanzania wenzao.Lengo lao kubwa ni kuzua mijadala ya kutuondoa kwenye focus ya mambo muhimu.Unfortunately,kuna nyakati tunalazimika kuacha kuwakalia kooni mafisadi wenyewe na kulumbana na hawa mahawara zao.
 
Either hujanielewa au Sijakuelewa. Nisome kwenye post nyingine hapo juu please.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…