CHADEMA sasa wazozana wao kwa wao

CHADEMA sasa wazozana wao kwa wao

CHADEMA hatuna kuogopana kama walivyo CCM, mtu akileta matatizo anaitwa kwenye vikao husika ajieleze. Mifano tunayo mingi tu na endapo atakuwa amekosea anapewa adhabu hata ikimgharimu cheo chake. Hatumuonei haya yeyote

IN CHADEMA NO FEAR OR FAVOUR
 
Urafiki wa mbwa mwitu huisha pale nyama inapokosekana
pack-african-wild-dog-pups-9333523.jpg
Na unafiki wa kula rambirambi za wajane huwa unaisha lini?
 
Mbona ishu ndogo sana hii tofauti na heading inavyosomeka? ama ndo michapo ya kishostito imeamia Raia Mwema,CDM ni chama makini na mapungufu kama haya yamekuwepo na yatakuwepo dawa ni kutrekebisha penye tatizo kisha tunawapa za uso CCM
 
Hao wengine wanne (wachaga)Tarimo,Ngowi,Kessy,Kinabo wakiandikia barua ninajisaidia haja ndogo hapa jamvini,Siwajahi kusikia mchaga yeyote mwenye tuhuma Chadema akapewa onyo wala kufukuzwa.Wachaga hawaguswi Chadema kwani Mtei ameanzisha SACCOS kwa pesa yake mwenyewe.

Wewe kama si mchawi ni mnafiki. Kuna wakati unapiga kampeni kwamba CDM ni chama cha wakaskazini, sasa msuguano wa kisiasa umetokea kaskazini tena unaowahusisha wakazi wa kaskazini wenyewe ghafla umeanza kustreamline kati ya wachaga na wapare. Kwa nini umekubuhu kwa ukabila? Unapata faida gani kwa kupandikiza chuki kwa watanzania kuwagawa kwa ukanda na makabila? Wachaga wanakupunguzia haki yako ya maisha ndani ya nchi hii? Tafakari! Siasa za maji taka unazoendesha JF inakupunguzia hadhi na utu japo unatumia ID bandia.
 
Wewe kama si mchawi ni mnafiki. Kuna wakati unapiga kampeni kwamba CDM ni chama cha wakaskazini, sasa msuguano wa kisiasa umetokea kaskazini tena unaowahusisha wakazi wa kaskazini wenyewe ghafla umeanza kustreamline kati ya wachaga na wapare. Kwa nini umekubuhu kwa ukabila? Unapata faida gani kwa kupandikiza chuki kwa watanzania kuwagawa kwa ukanda na makabila? Wachaga wanakupunguzia haki yako ya maisha ndani ya nchi hii? Tafakari! Siasa za maji taka unazoendesha JF inakupunguzia hadhi na utu japo unatumia ID bandia.
Mkuu kama unaniona mimi mchawi subiri unabii wangu ukamilike katika hili

 
Khaa!!! Mie nitakata gogo kabisa. Mbona Mbowe alifanya hivyohivyo kwa kukodisha vyombo kwa bei ya kitalii??? Hakuna asiyejua kuwa ni chagadema ni sakos tu. Wachaga wameshika nafasi karibu zote ndani ya chama. Ole wako kama siyo mchaga utamani nafasi hizo....utaundiwa zengwe lisilokuwa na kichwa wala miguu na wenye mbwa kisha mbwa wanakufukuza
Lengo lako ni Udini,saa hii mnazungumza ukabila 2015 unaamia Udini.na sio hiari yako bk7 zinawatoa sana ufahamu.watakwambia andika ni chama cha Wakrito na kwa utumwa wa bk7 utaandika.
 
HALI ya “hewa” ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoani Arusha imechafuka tena, baada ya Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Prosper Msoffe, kupitia chama hicho kuingia matatani akituhumiwa kutumia madaraka yake vibaya na kuingilia utendaji wa Halmashauri ya Jiji.Tayari chama hicho ngazi ya Wilaya ya Arusha Mjini kimemwandikia barua Msoffe ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Daraja Mbili kikimtaka ajieleze ndani ya siku saba kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya CHADEMA barua hiyo pia amenakiliwa kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa na wa Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa.
Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa pamoja na Msoffe, madiwani wengne wanne pia wameandikiwa barua za kujieleza na kujibu tuhuma za kushirikiana na Naibu Meya huyo kukihujumu chama hicho.
Madiwani wanaotajwa kuandikiwa barua ya kujieleza na Kata zao kwenye mabano ni pamoja na Crispin Tarimo (Sekei), Reyson Ngowi (Kimandolu), Emmanuel Kessy (Kaloleni) na Malance Kinabo “Kaburu” (Themi).




Madiwani hao wanatuhumiwa kuunda “genge” na kumwunga mkono Naibu Meya ambaye anatuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya na kwa kufanya biashara na Halmashauri ya Jiji la Arusha kinyume cha kanuni za viongozi wa umma.
Katika barua ya kumtaka Msoffe ajieleze ambayo Raia Mwema imeona nakala yake, Katibu wa chama hicho Wilaya ya Arusha Mjini Martin Sarungi, amemwagiza Naibu Meya huyo kujieleza ndani ya siku saba.
Katika barua hiyo yenye kumbukumbu namba CDM/MD/06/FEB/2014 ya Februari 26, Msoffe anatuhumiwa kuwa kwa nyakati tofauti ameingilia utendaji wa shughuli za Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa maslahi binafsi kinyume cha utaratibu.
Inasema barua hiyo: “Kwa nyakati tofauti umeingilia utendaji wa idara za Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa maslahi binafsi, kwa mfano, ununuzi wa mabegi na vitabu vya kumbukumbu (diary) ikiwa ni kinyume cha utaratibu”.
Tuhuma nyingine dhidi ya Naibu Meya huyo ni kutoa matamshi ya kukashifu, na kutoa lugha ya matusi na mwenendo wa kutia shaka kama Naibu Meya wa Jiji la Arusha kupitia chama cha CHADEMA.
Inaendelea barua hiyo: “Kwa nyakati tofauti umemkashifu na kumtukana Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA, Diwani wa Kata ya Ngarenaro, ndugu Isaya Doita”.
Aidha katika barua yake Sarungi anamalizia:”Barua yako ya kujieleza itakuwa utetezi wako kwenye Kamati tendaji ya Wilaya, Baraza la Mkoa, Baraza la Kanda ya Kaskazini na inatakiwa kufika ofisi ya Wilaya ndani ya siku saba”.
Kwa mujibu kwa kalenda siku saba alizopewa Naibu Meya huyo ziliisha Machi 5 mwaka huu.
Taarifa zaidi kutoka ndani ya chama hicho cha upinzani zinadai kuwa Msoffe anakabiliwa na tuhuma za muda mrefu kuhusu kujihusisha na biashara na Halmashauri ya Jiji kinyume cha sheria na kanuni za uongozi wa umma.
Inadaiwa kuwa kwa nyakati tofauti Naibu Meya huyo alipewa zabuni ndogo ya kununua mabegi maalumu ya madiwani na mwanzoni mwa mwaka huu alipewa zabuni ya kuagiza vitabu vya kumbukumbu (diary) na idara ya manunuzi.
Kanuni zinakataza Madiwani kufanya biashara na Halmashauri wanazosimamia kwa lengo la kuepuka mgongano wa kimaslahi na CHADEMA kinafahamika kwa misimamo ya kupiga vita ufisadi.
“Msoffe akitumia ushawishi na nafasi yake kama Naibu Meya, alipewa kibali cha kufanya manunuzi ya mabegi na vitabu vya kumbukumbu na maafisa wa idara ya manunuzi na ugavi kwa nyakati tofauti mwaka 2013,” kilieleza chanzo chetu.
Taarifa zinadai kuwa manunuzi hayo yalifanyika kupitia maduka mawili ya vifaa vya shule (stationary) yanayomilikiwa na Naibu Meya huyo ambayo yapo mjini Arusha.
Aidha, uamuzi wa kumwandikia barua ya kujieleza Naibu Meya huyo ulifikiwa baada ya kutokea mzozo katika kikao cha ndani ya chama mwishoni mwa mwezi Februari.
Katika kikao hicho inadaiwa baadhi ya madiwani waliibua tuhuma za ufisadi wa Msoffe ambaye anadaiwa kuwa mtu wa karibu na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.
Miongoni mwa tuhuma zilizoibuliwa ni pamoja kushiriki manunuzi ya vifaa vya Halmashauri pamoja na kushirikiana na Meya Lyimo kufanya maamuzi mbalimbali ya Halmashauri kwa maslahi yao ya kisiasa.
Aidha, kwa muda mrefu Naibu Meya huyo anatuhumiwa “kuunda ushirikiano haramu” na Meya wa Jiji la Arusha Gaudance Lyimo ambaye bado CHADEMA kama chama kinadai hakimtambui.
Katika tuhuma zinazoelekezwa kwa Msoffe zipo zinazohusiana na mgogoro wa kampuni ya Skytel iliyokuwa ikiendesha mradi wa taa za barabarani ambapo pamoja na kampuni hiyo kukiuka mkataba Msoffe alijitokeza hadharani kuitetea.
Naibu Meya huyo pia anatuhumiwa kuungana na baadhi ya viongozi wa CCM kumpiga vita aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji Zipora Liana ambaye baadaye alihamishiwa makao makuu ya Tamisemi kwa maslahi yao ya kisiasa.
Inadaiwa kuwa baada ya kuibuliwa kwa tuhuma dhidi yake katika kikao kilichofanyika ndani ya ukumbi wa Halmashauri Msoffe alimshambulia kwa lugha ya matusi Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA Isaya Doita akimshinikiza aachie nafasi hiyo.
Akizungumzia tuhuma zinazoelekezwa kwake Msoffe aliimbia Raia Mwema kuwa hajapokea barua yoyote kutoka kwa uongozi wa CHADEMA Wilaya ya Arusha.
“Kwanza sikuwepo Arusha kwa wiki mbili, nilikuwa kijijini kwangu (Wilaya ya Mwanga) lakini sijaona barua yoyote inayonitaka kujieleza kutoka chama changu nipe muda wa saa moja nipitie ofisini kwangu nitakujulisha,” alisema.
Baada ya saa moja Msoffe alipiga simu na kusisitiza kuwa hakuna barua yoyote inayomtaka ajieleze iliyopokewa ofisini kwake.
“Sijaona barua. Na kuhusu tuhuma zinazotolewa ni kwamba mimi ni Naibu Meya wa Jiji naelewa kanuni na taratibu zinanizuia kufanya biashara na Halmashauri, kwa maana hiyo sijwahi kufanyabiashara yoyote na Halmashauri ya Jiji,” alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Manunuzi na Ugavi wa Jiji la Arusha, Musa Musa, alisema ni kweli walitoa zabuni ndogo ya manunuzi hayo kwa mfanyabiashara mmoja ambaye hakumbuki jina lake.
“Ni kweli tulinunua hivyo vifaa ila siwezi kukumbuka, jina la kampuni iliyotumika na jina la mfanyabiashara huyo,” alisema Musa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Ephata Nanyaro hakuwa tayari kukanusha wala kukubali chama chake kuandika barua hiyo kwa maelezo kuwa bado ni mapema kuzungumzia suala hilo katika vyombo vya habari.
“Siwezi kusema chochote kwa sasa kwa kuwa sipo Arusha, ila masuala kama hayo ni ya kawaida katika vyama kwa watu kutofautiana mawazo na hatuwezi kusema kuna mgogoro,”alisema.
Nanyaro aliongeza kuwa atakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo wiki ijayo atakapokuwa amerudi mjini Arusha na kusisitiza kuwa CHADEMA hakiwezi kuyumbishwa na suala dogo kama hilo
source: Raia mwema

wazee wa kufukuzana,ngoja tusubiri uchaguzi mwingine mdogo
 
wewe kama si mchawi ni mnafiki. Kuna wakati unapiga kampeni kwamba cdm ni chama cha wakaskazini, sasa msuguano wa kisiasa umetokea kaskazini tena unaowahusisha wakazi wa kaskazini wenyewe ghafla umeanza kustreamline kati ya wachaga na wapare. Kwa nini umekubuhu kwa ukabila? Unapata faida gani kwa kupandikiza chuki kwa watanzania kuwagawa kwa ukanda na makabila? Wachaga wanakupunguzia haki yako ya maisha ndani ya nchi hii? Tafakari! Siasa za maji taka unazoendesha jf inakupunguzia hadhi na utu japo unatumia id bandia.
hapa ndipo maneno ya nyerere yanapotimia dhambi ya ubaguzi imewarudia wenyewe sasa wameanza kubaguana kiwilaya
 
Wewe kama si mchawi ni mnafiki. Kuna wakati unapiga kampeni kwamba CDM ni chama cha wakaskazini, sasa msuguano wa kisiasa umetokea kaskazini tena unaowahusisha wakazi wa kaskazini wenyewe ghafla umeanza kustreamline kati ya wachaga na wapare. Kwa nini umekubuhu kwa ukabila? Unapata faida gani kwa kupandikiza chuki kwa watanzania kuwagawa kwa ukanda na makabila? Wachaga wanakupunguzia haki yako ya maisha ndani ya nchi hii? Tafakari! Siasa za maji taka unazoendesha JF inakupunguzia hadhi na utu japo unatumia ID bandia.

Hizo ni ToR za kuleta uchafuzi kama walivyoandaliwa na wasaliti waliokubuhu. Watu wanakuwa tayari kuuza utu wao kwa fedha kidogo sana. Watu wa namna hii wamefanya hata hili jamvi likaanza kupuuzwa na wenye busara zao. Kuna watu ambao hawalali bila kufanya gutter politics kwani watakosa the so called b7. Shame on them.
 
Lengo lako ni Udini,saa hii mnazungumza ukabila 2015 unaamia Udini.na sio hiari yako bk7 zinawatoa sana ufahamu.watakwambia andika ni chama cha Wakrito na kwa utumwa wa bk7 utaandika.
Khaa!! nikiona maneno hayo huwa sisiti nakutia katika list yangu ya walevi wenye akili fupi na wasio na hoja:mvutaji:
 
Gazeti mpost mada mlitakiwa kuonyesha kwenye heading yenu kuwa ishu ni ya Arusha kuliko ilivyo mume i project kuwa ya kitaifa!
 
mkuu hata mimi nimeanza kuamini sasa. na imekuaje kwenye mwiji wa wameru kusiwepo na mmeru hata mmoja, halafu wawepo wachaga peke yako kwenye udiwani? I am over exhausted.

Hao wengine wanne (wachaga)Tarimo,Ngowi,Kessy,Kinabo wakiandikia barua ninajisaidia haja ndogo hapa jamvini,Siwajahi kusikia mchaga yeyote mwenye tuhuma Chadema akapewa onyo wala kufukuzwa.Wachaga hawaguswi Chadema kwani Mtei ameanzisha SACCOS kwa pesa yake mwenyewe.
 
CHADEMA hatuna kuogopana kama walivyo CCM, mtu akileta matatizo anaitwa kwenye vikao husika ajieleze. Mifano tunayo mingi tu na endapo atakuwa amekosea anapewa adhabu hata ikimgharimu cheo chake. Hatumuonei haya yeyote

IN CHADEMA NO FEAR OR FAVOUR
Acha unafiki wewe!
Kesi ya Katibu Mkuu wenu "kujikopesha" ruzuku imeishia wapi?
 
Back
Top Bottom