CHADEMA sasa ni kama chama cha rufaa Tanzania:

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,398
3,244
Hakika kutoka nchi ya watu waoga mpaka nchi ya watu wataka mabadiliko si kazi nyepesi. Elimu hiyo hutolewa na watu makini wasioogopa vitisho.

Mabadiliko yana changamoto zake hivo kuhitaji CHAMA CHA RUFAA CHA SIASA. Taka usitake sasa CHADEMA kimekuwa si chama kikuu cha upinzani bali CHAMA SIASA CHA RUFAA TANZANIA.

Hii ni kwa sababu wanachama wa vyama vingine pamoja na CCM wameungana na wananchi kuijenga CDM kimkakati na mawazo ya kuikomboa TANZANIA.

Hatua kwa hatua pamoja na vikwazo vingi lakini bado chama kimedumu na kujipatia nafasi kubwa katika duru za siasa Tanzania.

Kupanda kwa CHADEMA kumesababisha ama kufa au kudumaa kwa vyama vingne vya siasa hususani kutishia mustakabali wa CCM kwa siku za usoni kama si sasa. Hii hupelekea CDM kuwa kimbilio la majeruhi wa kiuchumi, kifikra, haki za watu kukandamizwa na sheria mbovu.

Hii yote ni sababu ya siasa za maji taka zilizoasisiwa na CCM kwa manufaa yao wenyewe. Wito wangu ni kwamba tuiunge mkono CDM kwa mawazo mema na tuwashauri pale wanapokosea.

Hakika mabingwa wa siasa wapo CDM na wengine wanaiga kwao.

KUINUKA CHADEMA NI ANGUKO KWA CCM NA MATAWI YAKE.
 
CDM wanaenda vizuri mambo yakiendelea hivi 2015 tutaongea mengine.
 
Naombea Chadema wawe makini,watanzania tulio wengi tunaamini ndio kimbilio letu.!
 
hakika jamii forum imevamiwa
 
Kumbe ukweli unauma jamani kama cdm imeweza kuibua ufisadi, kuibana serikali kila kona, kupunguza kura za kikwete mpaka kuitisha vikao kutafuta mchawi, kumchanganya nape mpaka asijue pa kuanzia na kumalizia tusitoe heko jaman! Au tuisifu ccm wasiopenda ukweli? Kumbuka enzi za MZEE WA VIWANGO NA KASI pale bungeni ccm hawakupenda. Huu moto wa cdm mtaupenda kweli?
 
hakika hakia ya mtu huwa hainyimwi ila inacheleweshwa tu kila lakheri cdm katika mipango yenu ila kumbukeni napo kwenye msafara wa mamba kenge wamo!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Umenena vema kama watu makini watasoma vizuri habari yako na kuilewa nadhani watakubaliana na wewe!
 
Peoples power!! Chadema ndo kimbilio la wanyonge Tanzania. CCM ndo kichaka cha mafisadi Tanzania
 
Atakaye kwenda kinyume na mawazo haya bila shaka atakuwa gamba
 
Unategemea nini katika nchi ambayo Serekaliyake ya CCM inaongoza kwa Mkono wa Chuma kama ile ya Gadafi.
 
Uhohehahe hamna kitu ! BASI TU waTanzania hawana la kufanya ,wanahudhuria mikutano kwa wingi wakifananisha na wakati ule wa senema za bure .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…