CHADEMA sasa mmekomaa, walivyotegemea sivyo

CHADEMA sasa mmekomaa, walivyotegemea sivyo

Mkuu inawezekana wameambiwa watikise kiberiti, possibly wamekuwa kimejaa, ndio maana nikasema Chadema wamekomaa hawatikisiki.

Ni kweli mkuu kiberiti kimejaa na wameshapagwa tayari.
 
Ben yupo wapi hilo ndo la msingi...ngonjera zingne hatuzitaki..chadema walibidi watoe tamko kuwa MTU wao amepotea..kama PA wa Chair wamekaa kimya je wewe mwanachama wa Nzega watakukumbuka hawa watu..! Usitake kujitetea kwa ujinga..km kweli Ben amepotea na mmekuwa kimya tumewadharau..

Pasco andika chochote
Hovyo kabisa akili yako. Kwa hiyo wewe huwezi fikisha ujumbe mpaka @Pasco aandike ndio utaona ujumbe umefika?

Ama kweli ccm ni ugonjwa mbaya sana, unaua (akili) kuliko malaria.
 
Kwa hvo hata ukilawitiwa nyamaza ili kuilinda nafsi yako, naomba usiisome biblia kinyumenyume hata Yesu alijua anaipoteza nafsi yake kwa kuwaambia iliyo kweli masadukayo na mafarisayo
Kama umekubali kulawitiwa mwenyewe unamwambia nani tena?
 
Kweli CHADEMA mmebadilika, hongera Katibu Mkuu Mashinji kwa kuja na strategies mpya.

Mwanzo sikuelewa kwanini mko kimya. Vijana wa Lumumba walikuwa wanataka CHADEMA kitoe tamko, walipoona business as usual wakaanza kudai kwanini Mbowe amesafiri eti akatishe ziara arudi kutoa tamko. Kumbe walitaka muingie kingi washangilie.

Ingekuwa enzi zile za daktari leo mngekuwa barabarani wengine wangekuwa Muhimbili wamevunjwa miguu wengine sentro polisi, Sirro angepanda cheo, Makonda angekuwa anashinda Clouds. Mmeshinda.

Good strategy, keep low profile talk less act more, waacheni wenyewe ndio wahangaike wasijue kesho mmepanga nini. Msiombe kukutana nao barabarani mkutane mahakamani au bungeni.

Mwenye akili ameelewa.

Wewe huzungumzii siasa, unazungumzia ushindani wa kibiashara. Siasa u keep low profile si unataka kujipeleka kaburini mwenyewe?
 
Quinine umeandika jambo jema na zuri ajabu lakini litawaduwaza hata "watu wetu" ingawa kwa "wale" utakuwa ni ukweli mchungu wasiotaka kuumeza!!
 
Wewe huzungumzii siasa, unazungumzia ushindani wa kibiashara. Siasa u keep low profile si unataka kujipeleka kaburini mwenyewe?
Siasa za leo sio za kupayuka ni strategy, kwa sasa chama kama Chadema hakina haja ya kupoteza muda na nguvu nyingi kuelezea kushindwa kwa sera za CCM watu wenyewe wanaona.
 
Ben yupo wapi hilo ndo la msingi...ngonjera zingne hatuzitaki..chadema walibidi watoe tamko kuwa MTU wao amepotea..kama PA wa Chair wamekaa kimya je wewe mwanachama wa Nzega watakukumbuka hawa watu..! Usitake kujitetea kwa ujinga..km kweli Ben amepotea na mmekuwa kimya tumewadharau..

Pasco andika chochote

Mbona yupo. Kwani mtu akikaa kimya inakuwa amepotea?
 
Quinine umeandika jambo jema na zuri ajabu lakini litawaduwaza hata "watu wetu" ingawa kwa "wale" utakuwa ni ukweli mchungu wasiotaka kuumeza!!
Mkuu yanini kwenda barabarani kuandamana huku ukijua polisi inasubiri uweke mguu serikali ipate sababu ya kukupotezea muda kukuhangaisha mahakamani, kwanini huo muda usiutumie kujenga chama.

Mashinji na Chadema waliliona hilo, Mbowe aliwatahadhalisha mapema kuwa wajiandae utawala huu ni tofauti na uliopita hauna maridhiano.
 
Chadema ni kama mchwa sasa hv, wanashambulia kote kote~ ughaibuni na mikoani bila kusahau kwenye mashina.

Kuja Kutahamaki Loo! Nchi ishakombolewa. Nzi wa kijani chali...!!
 
Sasa hivi Mtukufu anatamani kupiga marufuku mikutano ya ndani na ile ya nje ya Nchi.
 
Naunga mkono chadema kama taasisi kutopayuka payuka juu ya kupotea kwa ben kwani suala hilo ni zito linaweza hata kuchafua amani ya nchi.Hivyo waachiwe serikali na vyombo vyake vya usalama ndio walitolee matamko.Wakishindwa kufanya hivyo ndipo chama kitoe tamko juu ya nini kimeendelea wakiwa na ushahidi kamili
 
Binafsi sikuipenda CDM ya Dr. Slaa... Ilikua ni ya kiharakati kuliko kimkakati...

Ndio maana operesheni sangara na M4C hazikuzaa matunda waliishia kupata kata tatu kwa chopa tatu!!

Ukweli usemwe pamoja na yote mazuri ya Dr Slaa alikua na udhaifu Mkubwa sana kiutendaji.

Ninyi hamuaminiki leo hii ni kauli ya cdm?? kwakweli napata wasiwasi Magufuli akistaafu akihamia kwenu mtamnadi kwa mbwembwe kali yaani msimamo hakuna kabisa.
 
Usingeweza kuipenda maana kipindi hicho ulikuwa CCM ulikuwa unaimba nyimbo za kuisifu serikali na kutukana wapinzani mpaka ulipoletwa na mafuriko ya ULIPO TUPO
 
Ninyi hamuaminiki leo hii ni kauli ya cdm?? kwakweli napata wasiwasi Magufuli akistaafu akihamia kwenu mtamnadi kwa mbwembwe kali yaani msimamo hakuna kabisa.
Chama cha siasa ni dynamic kinabadilika kutokana na mazingira, hata CCM ya leo sio ile ya akina Kawawa, leo ukimfufua Sokoine na kumwambia hii ndio CCM hatokubali.

Juzi Chadema walikuwa wanaimba Lowassa ni fisadi leo ni kiongozi wao, huwezi kuwahukumu wana sababu zao, same as CCM walivyowaacha wakulima na wafanyakazi na kukumbatia wafanyabiashara wanasababu zao.
 
Back
Top Bottom