Chadema sasa haikamatiki,Ccm tumbo joto. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema sasa haikamatiki,Ccm tumbo joto.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Mar 4, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  • Slaa atiwa mbaroni, aachiwa, apokewa kama rais Bukoba

  na Sitta Tuma na Janet Josiah, Bukoba


  [​IMG]
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kuitikisa nchi kwa maandamano na mikutano yake ya hadhara kuzidi kuungwa mkono na umati mkubwa wa watu katika kila mkoa kinakopita.
  Baada ya kuiteka mikoa ya Mwanza, Mara na Shinyanga, jana chama hicho kiliuteka kwa kishindo mji mzima wa Bukoba kwa mapokezi, maandamano na mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wingi wa watu ambao kwa mujibu wa wenyeji wa hapa, haujapata kutokea huku Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk.Willbrod Slaa, akitoa tamko la msisitizo akisema “moto wa maandamano ya kudai mabadiliko sasa hautakoma, utaendelea nchi nzima.”
  Dk. Slaa aliwataka wakazi wa mji huo kumbana waziri mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu kashfa mbalimbali za ufisadi na uzembe zinazoikabili serikali yake. Pinda anatarajiwa kuanza ziara yake mjini hapa leo.
  Alisema CHADEMA itaendelea kufanya siasa kwa kuwafuata wananchi walipo na haitabakia kutegemea Bunge kama anavyotaka rais Kikwete wafanye kwani tayari chombo hicho cha wananchi kanuni zake zimechakachuliwa ili kudhibiti wabunge wa chama hicho.
  Awali maelfu kwa maelfu ya wakazi wa mji wa Bukoba walitanda na kufunga barabara na mitaa ya mji huo kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane mchana walipoanza maandamano makubwa ya kuelekea viwanja vya mashujaa mjini hapa kulikofanyika mkutano mkubwa wa hadhara. Maandamano hayo yalifanyika katika staili ya makundi huku kila kundi likichomoza katika mitaa tofauti na lingine na kujaza watu katika uwanja huo.
  Baadhi ya waandamanaji hao walionekana wakiwa na mabango mbalimbali yaliyosheheni ujumbe wa kuilaani na kuipinga vikali serikali ya rais Jakaya Kikwete na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  Wakati mji wa Bukoba ukiwa ni moja ya maeneo yaliyoathiriwa sana na janga la ugonjwa wa Ukimwi nchini, wananchi hao walionyeshwa kukerwa kwao na serikali ya CCM na katika moja ya mabango yao walisema hivi: “Keri ya ukimwi kuliko CCM”.
  Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, alipokewa kwa nyimbo zilizokuwa zikimtaja kuwa yeye ndiye rais halali wa nchi hii.
  “Rais, rais, rais, rais….”, ulisikika umati wa watu ukiimba katika maandamano hayo.
  Dk.Slaa aliingia kwa kishindo Bukoba baada ya kuachiwa huru na polisi mjini Kahama walikokuwa wanamshikilia akidaiwa kuwa alifanya mkutano bila kupata kibali wilayani Maswa.
  Akizungumzia kukamatwa kwake katika mkutano huo wa hadhara jana, Dk. Slaa alisema “walionikamata walitumwa wanikamate kwa sababu Kikwete ananiogopa, lakini sasa hawatuwezi, CHADEMA haikamatiki”
  Kabla ya tukio la kukamatwa kwa Dk Slaa juzi usiku askari polisi waliizingira hoteli ya Panich aliyokuwa amefikia kiongozi huyo.
  Baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi Mnadhimu huyo wa polisi alimhoji Dk Slaa: kwanini jana usiku ulikataa kuja polisi kama ulivyotakiwa? Dk Slaa alijibu “Nilihofia usalama wangu kwa sababu watu waionifuata hotelini sikuwatambua kwa sababu walikuwa wamevaa nguo za kiraia”.
  Mnadhimu Kamugisha alimuuliza tena kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani kwamba kwanini juzi alifanya mkutano Imalampaka bila kibali cha polisi? Dk Slaa alijibu, “nadhani mnafahamu kwamba chadema tunafanya maandamano na mikutano mikubwa ya hadhara na kila eneo tunalokwenda majimboni kuna ratiba, halafu ninyi mnauliza mambo kama haya hapa lakini juzi kiongozi wetu alipigwa jiwe na polisi hamjawakamata wahusika” Mbali na Dk Slaa kukamatwa na kuhojiwa na polisi wa wilaya hiyo ya Kahama kwa zaidi ya saa 1:30 wabunge wengine wawili wa CHADEMA, Chiku Abwao na Rachel Mashishanga pia walishikiliwa kwa mahojiano na jeshi hilo. Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Diwani Athumani (RPC) alipoulizwa sababu za jeshi lake kumkamata Dk Slaa wilayani Kahama badala ya kumkamatia wilayani Maswa alikofanyia mkutano huo, alisema waliogopa kumtia nguvuni wilayani Maswa kwa kuhofia uvunjifu wa amani.


  [​IMG]


  juu[​IMG] [​IMG]
   
 2. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  chadema vema!
   
 3. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Poleni sana
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  abdulahsaf
   
 5. I

  Idofi JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 1,548
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  polisi wa tanzania pamoja na kulala kwenye nyumba za mabati na vibox lakini bado ni watumwa wa ccm
   
 6. whizkid

  whizkid JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 301
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Viva CHADEMA! Viva la revolution!
   
 7. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 893
  Trophy Points: 280
  huu ni mwanzo tu. salam za rambirambi kwa kifo cha ccm zitafuatia baadae.
   
Loading...